Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 887
- 774
Sonona (depression) ni tatizo linalohusishwa zaidi na mtu kushindwa kuachia hasira zake kwa muda mrefu. Unapokutana na jambo linalokuumiza, halafu kwa sababu mbalimbali ukakosa namna nzuri ya kuonesha hasira zako, zipo tafiti zinaonesha unakuwa umejiweka kwenye mazingira hatari ya sonona.
Chukulia, kwa mfano, mazingira ambayo unaumizwa, unakasirika, unafedheheka kwa muda mrefu na lakini kwa sababu wewe ni mtu muungwana na usingependa matatizo na mtu unaamua kuigiza sura ya upole, uungwana, kutokukasirika, kutokuumizwa na hata kutokujiruhusu kukubali kuwa si tu umekasirishwa na kuumizwa lakini pia kupata nafasi ya kuonesha hasira na masikitiko.
Chukulia mazingira ambayo kwa muda mrefu unaumizwa kihisia na mtu unayemheshimu—mzazi, mpenzi, mwenzi, mwajiri—lakini huna mazingira salama yanayokuruhusu kujitetetea, kusimulia wala kueleza vile unavyojisikia kwa hofu ya kukataliwa, kugombezwa, kuhukumiwa au basi kuonekana mgomvi.
Jitihada za namna hii za kuzuia hasira kwa muda mrefu huweza kugeuza simulizi na kuanza kuaminisha kuwa wewe ndio tatizo, wewe ndio mkosaji na matokeo yake unaanza kujikasirikia, unaanza kujidharau, kujihuzunikia na kujiona huna thamani. Hapo ndipo mlango wa sonona unapofunguka. Unaanza kukinai kila kitu, unaanza kuchukia kila kitu. Usipopata msaada unaweza kuishia kufanya uamuzi unaokuathiri wewe mwenyewe na watu wanaokuzunguka.
Kinga ya uhakika ya sonona ni kujifunza njia sahihi za kuonesha hasira zako. Kuzungumza na aliyekuudhi na kuumiza ni udhaifu. Kumeza hasira na kuigiza ‘hakuna shida’ ili uonekane mwema asiyeudhika inaweza kuwa hatua mbaya inayoanzisha safari ya sonona. Kadhalika, pamoja na umuhimu wa dawa mtu anapofikia hatua mbaya, bado tiba ya uhakika ya sonona ni kujisikia salama kuonesha hasira zake na hisia nyingine ngumu bila hofu ya kudharaulika, kuhukumiwa na kuonekana hawezi kumeza hasira zake.