Nji hii..umasikini wa kujitakia?

Du
Hapana mkuu, ila mshangao wangu ni mtu kuwa na kaduka,kujinunulia pikipiki wakati nyumba ziko hoi!

Usishangae mkuu pikipiki ya kuleta bidhaa dukani- umeona dish? watu lazima tupate mlo wa akili (habari) hata kama mfukoni tuko hoi
 
oooh1 nyie vipi ilo sio dishi, iyo no rada ya hao wabibi na wababu wanao paaa na ungo usiku jamani kwenye hicho kijiji! na hiyo sio pikipiki ni fisi huyo sema masharti yanasema ukipiga picha anageuka kua pkpk, nyie hamuoni madaraja ya wachina mengine ukipiga picha haitokei.
 
hivi kama ameamua kulima akapata 1m, akaona afungue duka, then akalima na kuuza bidhaa akapata hela ya kununua bodaboda kwa 1.5m, then sasa analima, ana bodaboda na ana duka, anajipanga kuangusha mjengo.

Msiwe warahisi wa kutoa hukumu especially kama hamjui ku-hustle.
 
ccm hawapendi watu wanaopata taarifa , wanataka watu wapate taarifa za mambo yanayoendelea kwenye nchi hii kutoka kwa wakuu wa mkoa na makatibu tarafa!!

Ptuu!!!
 
Hapo sio kijiji baada ya mlima kitonga?

hivi kama ameamua kulima akapata 1m, akaona afungue duka, then akalima na kuuza bidhaa akapata hela ya kununua bodaboda kwa 1.5m, then sasa analima, ana bodaboda na ana duka, anajipanga kuangusha mjengo.

Msiwe warahisi wa kutoa hukumu especially kama hamjui ku-hustle.

Mkuu Ndahani, umepatia, hapo ni baada tu ya kamji kadogo ka Ilula, baada tu ya kupanda Kitonga.
Hapo mahala ni pa siku nyingi sana na pana wakulima lukuki wa zao la nyanya kwa mwaka mzima.
Hapo utakuta Fuso zinasheni kupakia nyanya kila siku, ukiacha zinazouzwa barabarani mwaka mzima.

Kwa msingi huo sikubaliani na observation ya Bigirita.
 
Duuh! My memory is still sharp I guess. In general mkoa wa Iringa pamoja na kulima mazao mengi ya biashara,watu wengi wako hoi kwa umaskini. Huwezi fananisha na wale tunaowaona mkoa wa Njombe na Mbeya. Kidogo Mafinga sababu ya biashara ya mbao kuna ahueni kidogo....and yet huu mkoa umetoa wasomi wengi sana maana ulikuwa na shule nyingi za wamissionary.
 
Hapo ni nyumbani kwa TAJIRI wa hiko kijiji si unaona mwenyewe kuna duka hapo hata COKE zipo, kuna dish kijiji kizima wanacheki TV hapo na bodaboda ipo.
 
Back
Top Bottom