Nje ya mawazo ya Mwanadamu Mungu hayupo, hajawahi kuwepo, na hatakuwepo

Maelezo marefu ila umethibitisha tu nilichokisema, yani nashindwa kuona ile connection au sababu za msingi za mtu kuwa atheist kutokana na hayo maelezo yako na ndio maana nikasema huwa ni watu waliyokata tamaa. Wengi kama sio wote huwa mnafikiri kuonesha madhaifu au makosa ya kwenye vitabu vya hizi dini ndio kitu chenye kuwafanya ninyi kuwa sahihi kwenye hiyo misimamo yenu, mnasahau kwamba wapo watu ambao hawaamini dini kabisa ila wanakubali uwepo wa Mungu. Kuna watu wana mitizamo kama yako kuhusu vitabu vya dini ila tu ni kwamba wao wanakubali uwepo wa Mungu ila nyie mnapinga kuwepo Mungu.
Kwa mindset kama yako, sidhani kama nina mda wa kukujibu tena
kwa sababu inawezekana hata uwezo wa kuelewa ni changamoto

Nikigeuza swali, nipe sababu ambazo zinaweza kukufanya wewe uwe atheist?
 
Kwa mindset kama yako, sidhani kama nina mda wa kukujibu tena
kwa sababu inawezekana hata uwezo wa kuelewa ni changamoto

Nikigeuza swali, nipe sababu ambazo zinaweza kukufanya wewe uwe atheist?
Sioni hizo sababu za kunifanya niwe atheist na hata kwenu nyinyi sijawahi kuona hizo sababu za msingi za nyie kuwa atheist, unakuta mtu kawa atheist kisa kagundua kuwa hizi dini ni za kubuniwa tu na watu hivyo ni uongo, sasa hapo kuamua kuwa atheist ndio ukweli?
 
Sioni hizo sababu za kunifanya niwe atheist na hata kwenu nyinyi sijawahi kuona hizo sababu za msingi za nyie kuwa atheist, unakuta mtu kawa atheist kisa kagundua kuwa hizi dini ni za kubuniwa tu na watu hivyo ni uongo, sasa hapo kuamua kuwa atheist ndio ukweli?
Kwako nitapoteza mda, usha declare wazi kuwa hakuna chochote kitakacho ku convince

True definition ya 'closed'mind
Haijalishi dini au imani yako ni ya hovyo kiasi gani utabaki huko

Unasema huoni sababu ya Mtu kuwa Atheist licha ya inconsistencies,false beliefs,scientific inaccuracies, lack of evidences zilivyojaa kwenye imani zote

Sasa sababu ipi unataka upewe?
Nambie sababu 3 kubwa zinazokufanya uamini hio dini uliyopo?
 
Bro, hope na faith ni vitu viwili tofauti
Usichanganye mambo
No they're not. Kama unaweza basi andika hapa tofaiuti yake, "yaani tofauti ya hope na faith".

Huwezi kutenganisha hope na faith hata siku moja.
Sababu hope inazalisha faith simultaneously universally na ni undistinguishable.
Even kwenye dictionary faith ni synonym ya hope.

Hauwezi kuwa na hope kitu fulani kitatokea bila ya kuwa na faith kwamba kitu fulani kitatokea.

Nakuuliza hili swali jepesi tuone kama utaweza kujibu.

Wakati wewe unapomsaidia ndugu yako anayeumwa unakuwa na (hope)tumaini la nini?
 
Kwako nitapoteza mda, usha declare wazi kuwa hakuna chochote kitakacho ku convince

True definition ya 'closed'mind
Haijalishi dini au imani yako ni ya hovyo kiasi gani utabaki huko

Unasema huoni sababu ya Mtu kuwa Atheist licha ya inconsistencies,false beliefs,scientific inaccuracies, lack of evidences zilivyojaa kwenye imani zote

Sasa sababu ipi unataka upewe?
Nambie sababu 3 kubwa zinazokufanya uamini hio dini uliyopo?
Wewe bado unashambulia dini tu kitu ambacho hakikufanyi wewe kuwa sahihi na hiyo misimamo yako, nimekwambia suala la uwepo wa Mungu si issue ya wana dini tu kuna watu hawaamini dini ila wanakubali uwepo wa Mungu ila sasa wewe unataka tujadili masuala ya vitabu vya dini kitu ambacho hakiondoi ile dhana ya uwepo wa Mungu kitu ambacho ndio jambo la msingi hasa hapa. Kwa kifupi wewe hauwezi kuwa sahihi huko kudai kwako kwamba hakuna Mungu kisa tu unaonesha makosa ya kwenye vitabu vya dini.

Sijui kama tunaelewana?
 
Na ndio maana nimetanguliza kusema kua kukubali kua kitu fulani hukijui kwasababu umeshindwa kukitafiti na kupata majibu sahihi ni jambo la busara wala sio aibu. Kutokubali kushindwa na kulazimisha majibu ambayo hayajapitia uchunguzi kwa lengo la kujipa tumaini ni ujinga kabisa.

Imagine unaelewa kabisa hiki unachokisadiki sio halisi umekitunga tu lakini unaamua kufumba macho na ubongo kujidanganya kua ni cha kweli kwa ajili ya kujipa tumaini, huu si wazimu?

Kwenye swala la imani (faith) ambayo ni common kwenye dini so nimegusa imani kwenye angle ya kiroho ambayo ni universal, sikumaanisha imani ya (trust) kama kuweka confidence kwa mtu mwingine kua hatokuangusha kwa jambo fulani. Kama mimi nilivyokuwekea confidence kua hutanijibu post yangu kwa kunitukana. Trust, Believe, Faith, Hope and Love ni somo pana na ni maneno yanayo changanya sana kimatumizi kulingana na muktadha husika

Hivyo leo hii ukimuambia mkristo kwamba Thor ni mungu wa kweli basi bila shaka hawezi kukubali kisa "thor" ni "imani ya mungu hivyo hapaswi kuhoji", well lazima akatae sababu sio "Imani" yake!.

Kuna swali ambalo hujalijibu, niliuliza kama imani haitakiwi kuhoji kwanini tuna imani zaidi ya moja kuhusu mungu huku zikipingana?

Huoni wingi wa hizo imani ulikuja baada ya watu kuanza kuhoji imani iliyotangulia ambayo walikua wakiiamini na wao kuanzisha imani yao walioona inafaa?

Kitendo cha wewe kusema (nitafanya kila njia ili kuhakikisha naokoa maisha yake) ni tayari hujui kama atapona au hatopona lakini bado unafanya kila njia ili umsaidie.
Na mpaka hapo tayari umeshaweka hope, na hope tayari ni imani.
Kama ungetaka kutumia logic basi ungeshindwa kumsaidia ndugu yako sababu hauwezi kuapply logic juu ya imani.


Hiki ulichokiandika hapa nime-notice kua we ni miongoni mwa watu ambao wanasumbuliwa na matumizi haya maneno matano trust, hope, faith, love and believe. Kwa ufupi tu ni kwamba hujaelewa mantiki yangu, mantiki yangu kwanza haikua mimi kukataa kutumia imani, tatizo linakuja kwako kushindwa kujua imani gani ambayo naizungumzia hapa.

Mzee kajifunze maana ya hayo maneno na matumizi yake kwanza unaonekana kuchanganywa sana
Kila swali ninalouliza basi linakuwa na point yake.

Ngoja niende straight kwenye point.
Trust ya kuamini kama mimi sitojibu kwa matusi bila ya kujua kama nitajibu kwa matusi au lah Na
Trust ya kuamini kuna mungu bila kujua kama yupo au hayupo, ni imani mbili zisizo na tofauti yoyote.

//Nb. Kwa imani siongelei kuhusu vitabu vya dini bali naongelea imani kama imani.

[[Imagine unaelewa kabisa hiki unachokisadiki sio halisi umekitunga tu lakini unaamua kufumba macho na ubongo kujidanganya kua ni cha kweli kwa ajili ya kujipa tumaini, huu si wazimu?]]

Kwanza kabisa mimi sitegemei vitabu vya dini kuamini uwepo wa mungu bali naamini kuhusu uwepo wa mungu kutokana na observation na misingi yangu mwenyewe.
Unaweza kuamini uwepo wa mungu bila ya vitabu vya dini. Imani na vitabu vya dini ni vitu viwili tofauti.

Kama wewe ulivyo weka trust kwamba mimi sitojibu kwa matusi ilhali hujui kama nitajibu kwa matusi au lah,
Ndio vilevile au sawasawa na kuweka trust kuwa kuna mungu lakini hujui kama yupo au lah.

Sasa mimi naweza kuuliza Je ulijuaje kama fulani hatojibu kwa matusi ikiwa hujui kama atajibu kwa matusi au lah?
Je wewe utaweza kujibu hilo swali?

AU unataka kusema " kitendo cha wewe kuweka trust kwamba mimi sitojibu kwa matusi" ni Wazimu pia.
Ukikataa then utakuwa unajipinga mwenyewe.

Pia imani ya kuamini kama kuna mungu ikiwa hujui kama yupo au hayupo, haijalishi kama kweli au sio kweli bali pia ni kugorven binadamu.
Ukweli ni kwamba watu wengi hawajitambui bila ya kuwaambia wafanye nini basi watu wangekuwa vichaa zaidi na dunia ingekuwa chafu mara mia ya sasa hivi.
Ndio maana kuna serikali, sheria na kanuni vyote hivyo ili kuhakikisha watu wanakuwa kwenye mstari sahihi na vyote hivyo lengo ni kuwa na Uongozi.

Sasa imani lengo kuu ni kuhakikisha atleast watu wanakuwa kwenye mstari, Imani ndio kiongozi wa mwisho, haijalishi kama ni kweli au sio kweli.
Ni kama wewe ulivyoweka trust ya kutojibiwa matusi hukujiuliza swali lolote bali uliamini tu, the same thing ndio kinatokea kwa wanaoamini kwenye uwepo wa mungu.

Maana ya imani ni kuamini bila kuuliza sababu ukiuliza hakuna kitu ambacho kitamake anysense.

Sasa nyie jamaa mnajaribu kuhoji credibility ya Imani kitu ambacho mnajua ni impossible kupata majibu, na hiyo ndio sababu nikawauliza kwanini mnapinga uwepo wa mungu?
Well mkashindwa kujibu na sidhani kama mtakuja kujibu.
Sababu inayowafanya nyinyi kushindwa kujibu "kwanini" ndio sababu hiyohiyo inayowafanya waamini uwepo wa Mungu washindwe kujibu.

[[Kuna swali ambalo hujalijibu, niliuliza kama imani haitakiwi kuhoji kwanini tuna imani zaidi ya moja kuhusu mungu huku zikipingana?
Huoni wingi wa hizo imani ulikuja baada ya watu kuanza kuhoji imani iliyotangulia ambayo walikua wakiiamini na wao kuanzisha imani yao walioona inafaa?]]

Hapana. Imani ni kama utamaduni na kila kundi la watu lina tamaduni zake.
Kundi la watu sababu binadamu hawaishi sehemu moja wala hawakuwahi kuishi kwa pamoja hivyo wazi kupingana na kutofautiana ni kitu cha kutegemea.
Unaposema "watu kuanza kuhoji imani iliyotangulia" ni sawasawa na kusema (leo hii watu wote billion 8 tuanze kuhoji imani moja like wote tunakaa sehemu moja) kitu ambacho ni uongo.

//swali jepesi sana.

[[Hiki ulichokiandika hapa nime-notice kua we ni miongoni mwa watu ambao wanasumbuliwa na matumizi haya maneno matano trust, hope, faith, love and believe. Kwa ufupi tu ni kwamba hujaelewa mantiki yangu, mantiki yangu kwanza haikua mimi kukataa kutumia imani, tatizo linakuja kwako kushindwa kujua imani gani ambayo naizungumzia hapa.]]

Ngoja nimention hii kitu kwanza.
kwenye kiingereza neno moja linaweza kuwa na maana nyingi tofauti na maneno mengi pia yanaweza kuwa na maana moja.
mfano ukisema faith, hope, belief, trust, optimism, expectation, confidence, credence, sureness hayo maneno yote yana maana moja kwenye kiingereza except yanatumika kutegemea na situation husika. hata kwenye kiswahili pia.
Au kama unapinga basi toa maneno tofauti kwenye kiswahili yanayowakilisha hope, faith na trust huku yakiwa na maana tofauti pia...?

Hivyo kwa mfano huo bila shaka naelewa maana za maneno hayo matano.
Tatizo ni wewe kushindwa kuelewa maana za hayo maneno hivyo unajicontradict bila kujua.

Imani unayoitumia wewe kuamini ndio imani hiyohiyo wanayoitumia waamini mungu kuamini.
Narudia hapa siongelei vitabu vya dini bali naongelea imani kama imani.
 
to
Mkuu umefafanua vizuri, idea ya god ilikuja ili kuikabili hofu ya duniani ndio maana wafia dini wanaamini kuwa kuna nchi inaitwa mbinguni, huko hakuna kuugua, kufa, njaa n.k yaani huko ni full kula bata tu, huhitaji ajira wala kufanya biashara ili uishi huko vyakula vipo vya kutosha yaani kuna chipsi za kumwaga, nyama choma, piza baga n.k

Ndio maana unawaona wanapambana usiku na mchana kusali ili siku moja waingie kwenye hiyo nchi. Hata telebani nao wanapambana waingie huko lakini najiuliza hao majamaa ukiingia nao mbinguni itakuaje 😃😃😃

Hahahaha mkuu umenichekesha sana!
 
Mkuu umefafanua vizuri, idea ya god ilikuja ili kuikabili hofu ya duniani ndio maana wafia dini wanaamini kuwa kuna nchi inaitwa mbinguni, huko hakuna kuugua, kufa, njaa n.k yaani huko ni full kula bata tu, huhitaji ajira wala kufanya biashara ili uishi huko vyakula vipo vya kutosha yaani kuna chipsi za kumwaga, nyama choma, piza baga n.k

Ndio maana unawaona wanapambana usiku na mchana kusali ili siku moja waingie kwenye hiyo nchi. Hata telebani nao wanapambana waingie huko lakini najiuliza hao majamaa ukiingia nao mbinguni itakuaje
Mataleban na ma alshabab watatuchinja hata huko mbinguni tukichelewa kula piza!
 
Exactly that's why nimetumia neno "kumuombea" because I already knew lazima ufike hapa.

humuombei lakini kwanini unamsaidia?
Unamsaidia kwa nia ya "ili apone" Hujui kama atapona au lah lakini bado unamsaidia ili apone.
Na ukifikia hiyo hatua tayari umeshatengeneza hope.
Au ungeshindwa kumsaidia ndugu yako kama ungetaka kuapply logic kwenye hope, sababu hope ni imani already.
Na huwezi kutumia logic kwenye imani.

You see you don't have to apply logic in everthing in oder to make it real au kumake sense out of it. na hiyo ndio maana ya kuwa binadamu, na ndio maana unatumia Imani bila kujua sababu it's in your nature.
Au wewe usingekuwa unasaidia ndugu zako au kutoa misaada kwa yoyote, sababu What's the point of helping?

Kama unakataa, basi nakuuliza je unaweza kuniamba nini kimekufanya umsaidie ndugu yako?
Na unaweza kudefine hicho kilichokufanya umsaidie ndugu yako?

Unasema unatoa misaada pale unapopata nafasi sababu kwako wewe hiyo ni "symbol of humanity" unadhani hiyo ni sensible point?
Now nakuuliza swali : kwanini unatoa misaada and what's the point?
Symbol of humanity?. Why does symbol of humanity matters to you?
Kuna logic gani nyuma ya "symbol of humanity?

To assure you nipo responsible na maisha yangu kwa 100%. sababu I've been there it's just too dark lakini tayari nimeshajifunza mengi.

The point is kuwa atheist au kutokuwa haimaanishi utaa"achieve" au utashidwa "kuachieve" chochote walichoachieve wengine it doesn't matter who they were nor who they are.
Sababu deepdown again sisi wote ni Binadamu.

Kwangu mimi kuwa atheist au kutokuwa it just doesn't matter lakini ni vizuri kufikiria nje ya box kama unaweza kutolerate kilichopo nje.

Please nitajie njia moja tu ambayo itakufanya uishi maisha yenye maana?

Swali la mwisho sio la kipumbavu bali hujui kwanini unapinga uwepo wa mungu now una tofauti gani na anayeamini uwepo wa mungu?
Swali lako la mwisho naamini wapingaji ndo wafuasi wa ibilisi atimize ahadi yake.
 
habari great thinkers.

Uwepo wa mungu ni matokea ya maendeleo ya binadamu katika kuupata ustaarabu.Men create the god in their own imagination.Ndo mana wale miungu ya kale kabla ya hizi dini mpya za kisasa walikuwa na maumbo ya kibinadamu(human look_like) hata sifa walikuwa kama binadmu.
Walikuwa na sifa za kulia, kukasirika,wivu, njaa n.k.

Lakini hizi dini za kileo ni maboresho ya dini za kale so that hata miungu ya dini hizi wamepewa sifa nyingi kidogo kuliko wale wa kale,ikiwemo kutoonekana,ana uwezo wote, yupo kila sehemu n.k.
Nadhani wote tunajuwa kuwa binadamu alikuwa anaishi pamoja na wanyama wengine hapo kale kabla ya kuanza kujitenga na kuanzisha ustaarabu wake,katika kipindi hiki cha maisha binadamu alikuwa hana tofauti na wanyama wengine.Ilimchukau mamilioni ya miaka biandamu kujitofautisha na wanyama wengine na kuanza kustaarabika.Katika kipindi hiki huyu binadamu alianzisha mambo mbalimbali ikiwemo Dini,mungu,sheria,taifa n.k.

There are no gods,no god in the universe,no nation,no money,no justice,no law,no human rights out side the common imagination of human beings.Mara baada ya kuapata ustaarabu binadamu aliweza kuanzisha mambo mengi ikiwe religion institutions,mungu n.k.

View attachment 1941529
Sawa, upande mmoja uaweza kuwa uko sawa! Lakini tunazungumzia suala la Mungu hili i jambo la imani, Hata hayo maandishi na yale ya kwenye iblia yote yaliandikwa a mwanadamu!
Kumbe hata wewe unayeandika hayo ukiulizwa kuwa je Mugu alikuthibitishia lini kuwa "nje ya mawazo ya mwanadamu hajawahi kuwepo na hatokuwepo??" Ofcoz hutakuwa a jibu, hivyo tusitowe Coclusion kwa mambo ambayo ya kufikirika tu!
 
Sema tatizo kuwa atheist sio jibu yani ukiwasikiliza atheists wengi humu kwanini wamekuwa atheists utasikia wanaanza kuelezea mapungufu ya dini waliyokuwa wanaamini mara sijui walikuwa walikuwa wanajiuliza maswali ambayo hayana majibu na ndio wakaamua kuwa atheist, kwahiyo ni kama watu ambao wamekata tamaa hivi.
Kama kuna mapungufu je ni faida gani wanapata kupinga?
 
kwangu nilishaclose discussion.......
unaweza kucheki mdau mwingine akufafanulie
Hakuna alichomzidi

Hao ni wapumbavu tu wasikupotoshe kwa vimaneno vyao vingi visivyo na maana

Kuandika andika kiingereza usifikiri ndiyo ishara una akili
 
Back
Top Bottom