Njaa kali yasababishe wale viwavi, tena wanauzwa sokoni

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Watu wanasema Tanzania kuna njaa? njaa ndio hii bana
kutokana na kuwa na njaa kali na kukosekana kwa nafaka nyama au samaki viwavi ndio chakula kikuu cha hawa wadau tena wanauzwa sokoni kwa mafungu..!! Hii ndio Afrika bana pamoja na rasilimali zote na zana za kisasa za kilimo tulizotengenezewa na wazungu bado tunakula wadudu kwa kukosa chakula
 
Wewe ubongo wako umeathirika kabisa.
Huyo kiwavi unapata direct protein ambayo haina madhara yeyote. Au ulitaka wawe kwenye makopo prepared from ulaya.?
Hawana tofauti na senene au nzige .
 
Wewe ubongo wako umeathirika kabisa.
Huyo kiwavi unapata direct protein ambayo haina madhara yeyote. Au ulitaka wawe kwenye makopo prepared from ulaya.?
Hawana tofauti na senene au nzige .
wewe umeelewa walichosema hapo? au unaishia kutukana tu
 
Kuna nchi nyingi za kiafrika kula wadudu ni sehemu ya utamaduni! DR Congo ni mfano hai!!
 
Kwa hiyo na sie wahaya wala senene tuna njaa? Nadhani kula wadudu ni suala la utamaduni. Leo hii huwezi kwenda Mtwara ukakuta wanakula panya ukasema Mtwara wamekumbwa na njaa, hapana ule ni utamaduni wao.
 
Kama wanakula Viwavijeshi na wana afya nzuri kama wanavyo onekana kwenye video, shida ipo wapi?
 
Tanzania je!?, pweza, prawns, nzige,senene, kumbikumbi mention.....
Nzige, Senene, Kumbikumbi..., wanapatikana kwa sana.

Pweza na Prawns ni aina ya samaki (hawapendeki sana huku kwetu bongo)
 
Hawa wadudu Zambia na Congo ni chakula cha hadhi ya juu sana hta tunduma wanauzwa sokoni mm bnasfi nmekula sana ni watamu ajabu ukionja huwez acha
 
Kwa mfano ndo unakumbana na hao jamaa wanao kula hao chavichavi, ktk kucheza mpira, dah inaonekana kikumbo chake kimoja tu we kule kudadadeki
 
Watu wanasema Tanzania kuna njaa? njaa ndio hii bana
kutokana na kuwa na njaa kali na kukosekana kwa nafaka nyama au samaki viwavi ndio chakula kikuu cha hawa wadau tena wanauzwa sokoni kwa mafungu..!! Hii ndio Afrika bana pamoja na rasilimali zote na zana za kisasa za kilimo tulizotengenezewa na wazungu bado tunakula wadudu kwa kukosa chakula

Acha kupotosha, hiki ni chakula chao cha kila siku! Wanakula kama kumbikumbi vile
 
Watu wanasema Tanzania kuna njaa? njaa ndio hii bana
kutokana na kuwa na njaa kali na kukosekana kwa nafaka nyama au samaki viwavi ndio chakula kikuu cha hawa wadau tena wanauzwa sokoni kwa mafungu..!! Hii ndio Afrika bana pamoja na rasilimali zote na zana za kisasa za kilimo tulizotengenezewa na wazungu bado tunakula wadudu kwa kukosa chakula

Siku nyingine jifunze kutafiti kiduchu tu kabla hujaandika. AFRIKA sisi sijui tukoje. Hapo mchina ama mvet akila chura, mende, minyoo na viwavi wala hutasema njaa. Utasema anaongeza protein.
Wewe ubongo wako umeathirika kabisa.
Huyo kiwavi unapata direct protein ambayo haina madhara yeyote. Au ulitaka wawe kwenye makopo prepared from ulaya.?
Hawana tofauti na senene au nzige .
 
Nchini Zambia viwavi hutumika kama chakula. Ukitaka kujionea vuka mpaka wetu na Zambia hapo Nakonde tu,utakuta wakati wa msimu wake soko limejaa viwavi wakiuza kwa mafungu kama dagaa. Viwavi hutokea kwa msimu kama vile tunavyoona kule Bukoba wanavyosherehekea msimu wa senene, Kigoma wanavyosherehekea msimu wa kumbikumbi na manyigu. Hii haina tofauti na Japan wanavyokula konokono,Slovakia wanavyokula mapanya buku n.k. Kwa kawaida hawali viwavi kwa ajili ya njaa ila ni moja kati ya mila na destuli ya maeneo husika.
 
wewe umeelewa walichosema hapo? au unaishia kutukana tu
Mkuu, kama huli viwavi ni wewe. Rukwa na especially swax, pamoja na kuwa na chakula cha kutosha, lkn viwavi ni moja ya mboga yao mhimu sana. So kula viwavi sio sababu ya njaa.

Ni kama mbozi wanavyukula panya, sio sababu ya njaa hata kidogo, ni vyakula vya asili vyenye heshima yake katika jamii
 
Sioni ubaya wa kula viwavi jeshi per se,afterall it's a good source of protein.Kusini mwa Africa in Zambia, Malawi etc. it's a delicacy.Inakuwa ni tatizo kama
sio kuwaida kwa wahusika kula,na pia kama vinaliwa kwa kuwa hakuna alternative.
Watu wanasema Tanzania kuna njaa? njaa ndio hii bana
kutokana na kuwa na njaa kali na kukosekana kwa nafaka nyama au samaki viwavi ndio chakula kikuu cha hawa wadau tena wanauzwa sokoni kwa mafungu..!! Hii ndio Afrika bana pamoja na rasilimali zote na zana za kisasa za kilimo tulizotengenezewa na wazungu bado tunakula wadudu kwa kukosa chakula
 
Kule Zambia wanaita VINKWALA na ni mboga ya heshima haina uhusiano na njaa. Usichanganye watu.
 
Back
Top Bottom