Njaa isiyokuwa ya Kawaida inaniandama

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,229
3,525
Jaman wakuu naomba kufahamu ni Tatzo gani ambalo linaandama mwili wangu, Mda mfupi uliopita nilikuwa sjui maana ya njaa yaani nilikuwa sihisi njaa kirahisi nilikuwa nina uwezo wa kushinda siku nzima bila kula na bila kupata mabadiliko ya aina yeyote mwilini mwangu.

Ila kwa sasa baada ya kuoa nimejikuta Mwili wangu umebadilika nimekuwa ni mtu anaetamani kula kula kila wakati na ikitokea mda kama nusu saa hivi bila kula kula naanza kuhisi njaa yaan naskia kama tumbo linauma kwa ndani na viungo kuishiwa nguvu mda mwingine naanza kutetemeka

Kuna mda nilifikria labda hali hii inanitokea kutokana na hali ya fongati ya ndoa ila kwa namna moja au nyingine ninaweza kupingana na wazo hilo

Kwani kuanzia awahi hata kabla sjaoa huyu mwanamke na kuanza kukaa nae rasmi kwangu kama mke wangu hata awali tulikuwa tunashinda mda wote tukiwa pamoja kwani tulikuw tunasoma chuo kimoja japo kila mtu alikuw na room yake ila tulikuwa tunakaa pamoja mda mwingi hata zaidi ya saizi

Sasa tatzo langu hii hali nashindwa kujua kwann initokee saiz?
Yaani napata njaa isyoya kawaida niliamua kustisha hata huduma ya unyumba kwa mke wangu nikidhan kuwa labda ndio chanzo ila bado ndio hali hii inazidi kuniandama

Naomba kujulishwa na wataalamu hali hii inatokana na nini?
Na nikitaka kuangalia saiz msos ninaokula ni msos mzuri na huwa ninabadilisha diet tofauti na maisha ya zaman ya kutegemea chakula cha cafeteria chuon??
 
Kuna alarm inalia kwenye masikio ya tumbo lako. Kiufupi una dalili za Kisukari au kama si hivyo "Msongo wa mawazo a.k.a Depression" unakusogelea. Fanya hima angalia hivi vitu.
 
Umesema mwanzo ulikuwa unauwezo wa kushinda njaa muda mrefu, napia ukasema unasikia njaa inayopelekea viungo vya ndani ya tumbo kuuma... Hizo ni ulcers suspected...

Yaani ni dalili za Vidonda vya tumbo... Kuwa makini... Sasaivi njaa inayokuum ni ya kukwangua tumbo sio ya kawaida mwisho wa siku litaanza kuuma tumbo lenyewe sasa hata ukila tumbo litauma...fanya ule kwa wakati badilisha mtindo wa maisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom