Nebuchadinezzer
JF-Expert Member
- Oct 1, 2018
- 1,403
- 2,545
Habari za humu wanaJF?
Bila kuwachosha naomba niende moja kwa moja kwenye lengo la uzi huu.
Kuna jamaa (tunafanya nae kazi) pia ni rafiki yangu tunaishi nae ghetto moja.
Juzi katika kufanya usafi kwenye room nilikuwa naamisha mabegi naweka sebuleni ili nifanye intensive cleanness kuna kadi ya kliniki ya matibabu ya ARV niliiona, baada ya kuisoma nimegundua kuwa jamaa ni muathirika wa VVU na mbaya zaidi jamaa anatumia ARV kama mwaka wa 6 sasa. Hii sio shida maana kuumwa ni sehemu ya maisha ya yyte aliyezaliwa na mwanamke.
Kinachonisukuma kuwaomba ushauri ni juu ya tabia ya huyu jamaa. Yaani jamaa ni mchakataji mzuri wa papuchi hapa mtaani. Habagui barmaids wala waimba kwaya. Mbaya zaidi ni kiongozi kwenye kwaya yao na huwa naona anavusha baadhi ya waimba kwaya na watoto wa shule.
Hili ni tatizo ila mbaya zaidi kuna binti flani wanamiadi ya kukutana kesho kutwa; maskini binti wa watu namhurumia sana maana jamaa kwa anavyojitapa kuwa hatumii kinga yeye ni nyama kwa nyama. Natamani nimwambie huyu binti ila nakosa lugha nzuri ya kumwambia na ukizingatia binti huyu anatarajiwa kuolewa soon maana ndoa yake imeshatangazwa kwa mara ya kwanza kanisani.
Utata mwingine unakuja kwa sababu nahisi kumwambia huyu dada ukweli ni sawa na kumsaliti jamaa maana ugonjwa ni siri. Na kama hakuwahi nambia kwa miaka yote hiyo hii inamaanisha hataki yyte ajue.
Namshukuru Mungu; ameniepusha na wadada anaotembea nao...mimi sina tabia ya uhuni japokuwa huwa naona rafiki zangu wengine wanagonga mashemeji(mademu wa marafiki zako) .
Naombeni ushauri katika hili, na nitumie mbinu gani kumuepusha huyu binti.
NB: Ukimwi bado upo; Mungu atusaidie; tuepuke ngono haramu.
ASANTENI.