Niwadhibitije mende na wadudu wengine watambaao chumbani kwangu?

Niwadhibitije mende na wadudu wengine watambaao chumbani kwangu?

Mwiyuzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2011
Posts
854
Reaction score
452
Naomba msaada juu ya namna ya kuwadhibiti mende na wadudu wengine watambaao.


Mimi ninaishi nyumba ya kupanga ambayo ina wapangaji wengi. Siku hizi kuna mende na wadudu wengine wengi sana wanaotoka nje na kuingia ndani ya chumba changu.

Nimefanya usafi na kupulizia expel but bado haijasaidia.


Usiku huu nimeshuhudia mende kibao wakubwa kwa wadogo wakizunguka humu chumbani pamoja na wadudu wengine.
Kwa kweli ninakereka saaaana!

Sijui hata nifanyeje ili kuepukana na adha hiiii!


Naombeni msaada wa namna ya kuwadhibiti hawa mende
 
pole sana. endelea kutafuta dawa kali zaidi.

asante, dawa sasa nitumie ipi manake nimetumia expel ambayo inasemekana kuwa kiboko ya wadudu wa aina hii lakini sioni mafanikio
 
Jaribu kufanya fumigation. Dawa za fumigation uzinunue mwenyewe au tafuta mtu mwenye uzoefu sio lazima utafute makampuni makubwa. Tafuta vijana wanafanya hizo kazi watakusaidia.
 
Dawa ni kuhama hiyo nyumba fasta

CHAKUFANYA NENDA MADUKA YA DAWA ZA PEMBEJEO ULIZIA DAWA INAITWA AKHERI POWDER HALAFU UNYUNYUZIE KWENYE PEMBE ZOTE ZA CHUMBA, HAKIKISHA HAUWEKI MABAKI YA VYAKULA NDANI MAANA YENYEWE YANASASABABISHA UWEPO WA MENDE. Halafu usisasahau dawa ya mende ile kama chaki uchore kwenye njia zao inasaidia sana. AKHERI POWDER INAUA MENDE, VIROBOTO,KUNGUNI,MCHWA,SIAFU,UTITIRI,BEI YAKE PIA NI NAFUU SANA, CHUPA NDOGO WAWEZA PATA KWA 2500/=
 
ukishindwa kwa plan a zote,tumia plan b..(hama hiyo nyumba)si umepanga tu!
 
sasa unataka msaada gani?kama hvo vumilia tu..

nilikuwa najaribu kukuonyesha ugumu ninaoupata kutoondoka fasta....si unajua tena kuacha kodi
 
CHAKUFANYA NENDA MADUKA YA DAWA ZA PEMBEJEO ULIZIA DAWA INAITWA AKHERI POWDER HALAFU UNYUNYUZIE KWENYE PEMBE ZOTE ZA CHUMBA, HAKIKISHA HAUWEKI MABAKI YA VYAKULA NDANI MAANA YENYEWE YANASASABABISHA UWEPO WA MENDE. Halafu usisasahau dawa ya mende ile kama chaki uchore kwenye njia zao inasaidia sana. AKHERI POWDER INAUA MENDE, VIROBOTO,KUNGUNI,MCHWA,SIAFU,UTITIRI,BEI YAKE PIA NI NAFUU SANA, CHUPA NDOGO WAWEZA PATA KWA 2500/=


Akheri naikubali sana. Nilinyunyiza kibarazani kwangu once ili kuua sisimizi na wamehama kweli. Weka kwenye entrace ya mlango, hakuna mdudu ataingia ndani lakini usafi na proper disposal ya wastes izingatiwe!!
 
Jaribu kutumia dawa inayoita DIAZONON / DIZON hii ni kiboko kwa wadudu wataambaao na warukao pia. Nebda duka la dawa za mifugo watakupa maelekezo jinsi ya kutumia.
 
Back
Top Bottom