Nilikuwa nikisikiliza wimbo huu na nikajikuta najiuliza, "hivi kuna wanaume wanaokubali kushare mapenzi huku wakitambua kuwa wanashare"
Eti wanaume hii imekaaje? Maana mie kila mwanaume niliyewahi kuwa nae walikuwa wakiniambia "nikigundua unanisaliti ndio tiketi yako na nakuacha"
Na ni sababu gani haswaa inayokupelekea ukubali kushare? Ni uhaba wa wanawake? Maana nijuavyo mimi wanawake ni wengi kuliko wanaume.
Karibuni.