Niulize maswali kuhusu software ya Adobe After Affect & Adobe Premiere Pro

Niulize maswali kuhusu software ya Adobe After Affect & Adobe Premiere Pro

Katika taaluma ya Film and Video Production, siku hizi wengi wetu tunajua ku-oparate camera, ku-shoot na kufanya editing. Lakini changamoto kubwa ipo katika Motion Graphics and Compositing.
Mkuu hongera kwa Nondoz huko juu,mimi napenda sana VFX Designing ila bado sijafika level nzuri nayotaka. Nina maswali mengi ya kukuuuliza.

Je unaweza ukanipa personal course /internship?
 
Mkuu hongera kwa Nondoz huko juu,mimi napenda sana VFX Designing ila bado sijafika level nzuri nayotaka. Nina maswali mengi ya kukuuuliza.

Je unaweza ukanipa personal course /internship?

hongera sana kwa kupenda VFX designing.yote yana wezekana kama utakuwa na dhamira ya kweli ya kutaka kujifunza na hatimaye upate msingi mzuri ktk motion design.

unaweza pia ukaanza kwa kuuliza maswali hapa hapa kwenye mada,ili na wengine wapate nafasi ya kuchangia/kujifunza.

karibu sana.
 
Lukansola

Lukansola, Deejaywilzz katoa pointer tu kuwa pamoja na uzuri wote wa after effect pia involvement ya camera-man lazima izingatiwe la sivyo hiyo application can be rendered useless kwa kuwa input ni mbovu.

Kuhusu suali la pili its obvious kuwa kuna kitu anataka amwambie mjuzi mwenzake ila anataka kujiridhisha kama anaifahamu hiyo application ili kupata mwega mzuri wa majadiliano kati ya wajuzi hawa!

Binafsi nimemwelewa Deejaywilzz nasubiri majibu ya mlengwa nipate faida katika majadiliano usitegemee straight forward Q&A kama mahakamani!

Asante 124 Ali,
Sorry deejaywilzz.
 
Last edited by a moderator:
Mimi umenitamanisha kuipata hii application!! Naweza kuipata vipi boss?? Ili niendelee na lectures zako huku nafuatilia kwa vitendo! Natanguliza shukrani nyingi kwako

Ni rahisi sana kuipata,njia moja wapo ni kuiomba toka kwa rafiki zako wa karibu ambao wanajihusisha na maswala ya video production (siku hizi watu hawanyimani softwares).njia ya pili ni kuidownload toka kwenye mitandao.
 
Kwa kutumia element 3d ambayo ni plugin ktk ae, naeza design model ya kitu chochote nachotaka

Nijuze zaid mkuu
 
upo sahihi sana kaka,ila mambo ya camera operator au director ku visualize ideas kama zilivyo andikwa ndani ya script na kuziunda katika hali halisi ya kifilamu,hufanyika zaidi kwa zile big budget project.

kwa hizi low budget project zetu huku kwetu tz,idea nyingi huja mkiwa location na mda mwingine mnajikuta mnatoka kabisa nje ya script kuanzaia dialogue,actions,costume etc.

mfano kwa kwa low budget project,huwezi kwenda mamlaka ya ndege uwaombe au uwalipe ili wazuie ndege zisiruke kwa saa kadhaa ili wewe u shoot movie yako,lakini kwa apps kama EA unaweza uka shoot ilihali ndege zina ruka na kusababisha kelele na hata kuingilia ktk engle ya shot yako,halafu baadaye ukakaa kwenye comp yako na kufanya "sky replacement''.mwisho wa siku mambo yakaendela.as simple as that.

cheki hapa.
before the sky replacement.
View attachment 226347

after the sky replacement.
View attachment 226348

Mkuu natamani sana ungekua unatoa mifano ya clip ulizocheza nazo ww mwenyewe tukaona.maujuzi yako, itatupa mzuka sana mkuu
 
Storyteller ondoa shaka,hapo juu niliambatanisha mifano ambayo nimefanya mimi mwenyewe kwa mkono wangu.nilifanya hivyo ili kumsaidia member ambaye aliniuliza swali kuhusu masking.
 
Kwa kutumia element 3d ambayo ni plugin ktk ae, naeza design model ya kitu chochote nachotaka

Nijuze zaid mkuu

Asante kwa swali,ninacho fahamu,element 3D ni plugin inayoundwa na video copilot na hutumika zaidi katika kuboresha vivuri na texturing(sina neno mbadala la kiswahili la texturing) kwa 3D objects ambazo zimekuwa extruded ndani ya AE au imported toka ktk 3D app nje ya AE.

Siwezi kukili kwamba app hiyo inaweza ikaunda chochote kama ulivyo niuliza,sababu sina uzoefu mkubwa na element 3D japo niliwahi kuitumia kwa kipindi kifupi.labda tuache member wingine mwenye uzoefu zaidi aje ajazie nyama.au kama vipi ingia HAPA.
 
Sawa sawa mkuu nimekupata,

Najua huu uzi hauzungumzii 3d lkn natamani kama ningependa nikuulize kama una ujuzi na 3d design kwa kutumia software yoyote ile km autodesk au maya... Na kama ni mtaalam wa 3d utupe uwanja wa tukuswalike mkuu...
 
kaka mbona niki download ni instal znagoma mkubwa? kama kuna maelekeza jins ya kuidowload na ku instal sorry ni nielekeze mkubwa


Zinaandika zimegoma au kuna maneno zinaleta ?
 
Yaan nikidowload faster to inamaliza bt niki instal..inafika kwenye next inapotea haionekan tena muendelezo wake kama wanavyoonyesha kwenye zle step kk
 
Sawa sawa mkuu nimekupata,

Najua huu uzi hauzungumzii 3d lkn natamani kama ningependa nikuulize kama una ujuzi na 3d design kwa kutumia software yoyote ile km autodesk au maya... Na kama ni mtaalam wa 3d utupe uwanja wa tukuswalike mkuu...

kwa kweli mimi sio mtaalamu wa 3D wa kiwango cha juu kiasi cha kuweza kufanya figure modelling ,na hata hizo maya,cinema4D and the likes sina uwezo mkubwa wa kuzielezea kitaalamu.

uwezo wangu mkubwa upo katika motion graphics,animation and compositing kwa kupitia adobe after effect.
nina uzoefu wa kutosha wa AE.tangu nimeanza kuitumia,huu sasa ni mwaka wangu wa nane.

zipo motion graphics apps zingine ambazo zinaleta ushindani mkubwa kwa AE,kama NUKE studio and Autodesk Smoke.
 
Back
Top Bottom