Niulize maswali kuhusu software ya Adobe After Affect & Adobe Premiere Pro

Niulize maswali kuhusu software ya Adobe After Affect & Adobe Premiere Pro

Adobe After Effect

Senior Member
Joined
Dec 31, 2012
Posts
144
Reaction score
75
Katika taaluma ya Film and Video Production, siku hizi wengi wetu tunajua ku-oparate camera, ku-shoot na kufanya editing. Lakini changamoto kubwa ipo katika Motion Graphics and Compositing.

Sio kila Cameraman au Video Editor anaweza pia kuwa Motion Grahics Designer au Compositor. kwa mataifa yaliyo endelea, hii ni field inayo jitegemea na inayo waingizia kipato kikubwa sana watendaji wake.

Kwa kulitambua hilo, leo natoa nafasi ya pekee kwa walio na interest na sanaa ya Motion Graphics, kuniuliza basic technical questions kuhusu Adobe After Effect ambayo ni moja kati ya Core Application in Motion Graphics.

Beginners wa ADOBE AE nafasi yenu ndio hii. Niulizeni yanayowatatiza kuhusu Application hii.

Karibuni.

NB : Mimi sio mjuzi sana wa Adobe After effect, ila naweza changia mawili mawili matatu kwa maswali nitakayo ulizwa,sambamba na hilo nakaribisha pia wajuzi wengine kusaidia kujibu pale nitakapo onekana kuchemka.

UPDATE:
wakati maswali yanayohusu Adobe After Effects yakiendelea,nimekuja na wazo jipya la kukaribisha maswali kuhusu Adobe Premiere Pro.bila shaka hii itawahusu wengi zaidi ukizingatia kwamba baadhi yetu angalau tunajua ABCs za kuedit video,tofauti na kufanya motion design au 3D creation.

video editing ni skills na art,kila editor ana editing art yake,lakini pia kila editor ana machaguzi yake ya software aliyo bobea,binafsi nimebobea katika Adobe Premiere Pro japo pia naweza kutumia final cut ingawa si kwa kiwango cha juu sana.

kwa hayo machache nawakaribisha pro editors,mje tusaidine kujibu maswali yatakayo ulizwa au kutoa msaada wa kimaarifa kwa wenye shida.

karibuni.
sh1.jpg
 
Asante sana, naomba kujua kama kuna namna ya kuondoa back ground kwenye video iliyopigwa bila green/ blue screen?
 
sasa nataka kuwapa mosheni vikaragosi wangu wawili na imekaaje upande wa 3d motion me napenda sana hiyo kitu thanks
 
Asante sana, naomba kujua kama kuna namna ya kuondoa back ground kwenye video iliyopigwa bila green/ blue screen?

kwa video ambayo haikupigwa ktk green/blue color as a background,si jambo rahisi kuondoa background(keying).ila kwa AE ni jambo rahisi kama utafata maelekezo kwa umakini.njia ya kwanza ni kupitia masking.unatumia pen tool ambayo ipo ktk EA,unachora shape ya object unayotaka ibaki ktk screen.baada ya hapo ile background itakuwa imeondoka.then una animate mask yako kama kulikuwa na movement ndani hiyo object iliyo baki.

njia ya pilli ni kupitia transfer modes,ila njia hii inaweza kuwa sio sahihi sana kwa sababu inachangua rangi ambayo ime dominate zaidi katika video yako.hii inafaa zaidi katika images.

nakuwekea screen shot hapa uone ni namna gani masking iliyo useful kuondoa background kwa video ambayo haikurekodiwa ktk green/blue screen studio.

before masking.
kabla.jpg

after masking
baada.jpg
 
sasa nataka kuwapa mosheni vikaragosi wangu wawili na imekaaje upande wa 3d motion me napenda sana hiyo kitu thanks

kwa upande wa vikaragosi,itategemea na program uliyo tumia kuwatengeneza.kuna apps ambazo zina ingiliana na AE,mfano ni cinema 4D na 3D studio max.hivyo basi kama uta import project yako ndani EA,uwezekano wa kuongeza life,emotions,feeling and movement kwa vikaragosi vyako ni mkubwa.
 
Adobe After Effects, asante sana, ache nifanya zoezi hili kwanza halafu nitarudi baadaye,
unaposema ku animate mask una maana gani? kwamba unaweka mask mpya kwa kila frame au?

thanks again mkuu
 
Adobe After Effects, asante sana, ache nifanya zoezi hili kwanza halafu nitarudi baadaye,
unaposema ku animate mask una maana gani? kwamba unaweka mask mpya kwa kila frame au?

thanks again mkuu

una animate mask path frame by frame kufatisha movement ya obejct ndani ya layer.si jambo rahisi lakini pia si jambo gumu.ni umakini wako tu wa kucheza na shape.

tazama screen shot hii.
mask path.jpg
 
Asante sana kwa majibu mazuri yaliyoambatana na vielelezo murua, nitafanya hii kltu, nina footage nataka kutumia kwa project tatizo ina back ground.

Endelea kushusha nondo sasa, naona hakuna maswali zaidi.
 
Nondo zipo ila nina shaka kama wapo members wengi wenye interest na AE ndani ya JF cos the topic is trending very slow.naogopa kupoteza mda wangu hapa kushusha vitu,halafu mwisho siku watu wakapuuza.
 
After Effects ni nzuri na inapunguza budget lakini mpango mzima ni Camera shooting, Kama camera man wako asipokuwa na vision ya kitu unachotaka kufanyia effects inakuwa ni useless so still camera man is the main man.

Umeshatuia Adobe After Effects CC ?
 
nondo zipo ila nina shaka kama wapo members wengi wenye interest na AE ndani ya JF cos the topic is trending very slow.naogopa kupoteza mda wangu hapa kushusha vitu,halafu mwisho siku watu wakapuuza.

Mimi niko tayari kupoteza muda wangu kukufuatilia mkuu.

Hivi unadhani mimi ni answering machine?
 
After Effects ni nzuri na inapunguza budget lakini mpango mzima ni Camera shooting, Kama camera man wako asipokuwa na vision ya kitu unachotaka kufanyia effects inakuwa ni useless so still camera man is the main man.

Umeshatuia Adobe After Effects CC ?

Samahani lakini mkuu, nilidhani mada inahusu kujifunza Adobe After Effects! unavyoongea ni kama; bila kuwa na camera man mzuri basi hakuna haja ya kujifunza after effetcs kwa sababu itakuwa ni useless, unatushauri tuanze kujifunza after effects baada ya kupata mpiga picha mwenye vision?

Kwanini unamuuliza kama alishawahi kutumia Adobe After Effects CC?
 
Lukansola

Lukansola, Deejaywilzz katoa pointer tu kuwa pamoja na uzuri wote wa after effect pia involvement ya camera-man lazima izingatiwe la sivyo hiyo application can be rendered useless kwa kuwa input ni mbovu.

Kuhusu suali la pili its obvious kuwa kuna kitu anataka amwambie mjuzi mwenzake ila anataka kujiridhisha kama anaifahamu hiyo application ili kupata mwega mzuri wa majadiliano kati ya wajuzi hawa!

Binafsi nimemwelewa Deejaywilzz nasubiri majibu ya mlengwa nipate faida katika majadiliano usitegemee straight forward Q&A kama mahakamani!
 
Last edited by a moderator:
deejaywillzz

ni kweli mkuu,camera movement and composition of shots is very important in production of film/videos,lakini pia VFX apps kama AE zinacheza nafasi kubwa ktk kuboresha project na kufanya vitu ambavyo kamwe camera peke yake haiwezi.

Mfano EA ina uwezo wa kustabilize shot, inauwezo wa kufanya motion tracking in 2D/3D space, ina uwezo wa kuboresha rangi kuendana na mood ya eneo, ina uwezo wa kufanya advanced titleling in 2D/3D space,

ina uwezo wa kufanya advanced compositing,ina uwezo wa kufanya epic VFX na zenye kuleta mshangao machoni pa mtazamaji.imejengewa uwezo wa kupokea third part plug ins nyingi toka kwa third part developers (video copilot,red giant,aescript,new blue fx,atomkraft nk).

Orodha ni ndefu hata siwezi kumaliza.lakini kubwa kuliko yote,imeshinda tuzo nyingi za filamu ktk category ya VFX.

Sijatumia AE CC,since ndio kwanza ilitoka 2013/2014,bado natumia CS5 japo nilijaribu kutumia CS6 lakini niliachana nayo kwa sababu sikuona tofauti yake na CS5,labda kidogo issue ya ray tracing. Siku zijazo nitajaribu hiyo CC, waswahili husema mchagua jembe si mkulima. kuna watu wanafanya mambo makubwa mpala leo kwa kutumia AE CS4.

NB: Nitafurahi ukinielimisha kuhusu AE CC.
 
Last edited by a moderator:
Samahani lakini mkuu, nilidhani mada inahusu kujifunza Adobe After Effects! unavyoongea ni kama; bila kuwa na camera man mzuri basi hakuna haja ya kujifunza after effetcs kwa sababu itakuwa ni useless, unatushauri tuanze kujifunza after effects baada ya kupata mpiga picha mwenye vision?

Kwanini unamuuliza kama alishawahi kutumia Adobe After Effects CC?

Kuanza kujifunza After Effects haiitaji uwe na camera man, good camera man anakuja pale unapofanya real production sababu director ndio anakuwa na vision ya iyo shot. My Point ilikuwa Camera man na Director wana big role kwenye After Effects sababu kabla hujafanya effects lazima uwe una picha iko kichwani (Picha ya effects unayotaka kufanya)

Kuhusu After Effects CC ni version iliyotoka baada ya CS6, nilikuwa namuuliza sababu nime install na kuna ishu imenipa ugumu sehemu flani nilitaka anisaidie
 
Kuhusu After Effects CC ni version iliyotoka baada ya CS6, nilikuwa namuuliza sababu nime install na kuna ishu imenipa ugumu sehemu flani nilitaka anisaidie

Uliza tuu kaka,sio lazima nijibu mimi, anaweza akatokea mtu mwingine anaye ielewa vizuri CC na akakupa jibu lenye msaada kwako.halafu uzuri wa previous versions za AE hazina tofauti kubwa na hizi versions za sasa,

vitu vingi hubaki constant na baadhi huachiwa plugins developers waviboreshe.hivi punde tu nimecheki tutorial ya AE CC na kugundua some of the new features are very common for an experienced AE user:

Effect Masks & composition options for individual effects, Two new keying effects: Key Cleaner and Advanced Spill Suppressor. HTML5 panels using CEP for more dynamic and interactive content.Kuler HTML5 panel. Text templates in AE can be edited in Premiere.

Typekit integration improvements.New and updated Curves effect.Scripting changes and many more
 
Kuanza kujifunza After Effects haiitaji uwe na camera man, good camera man anakuja pale unapofanya real production sababu director ndio anakuwa na vision ya iyo shot. My Point ilikuwa Camera man na Director wana big role kwenye After Effects sababu kabla hujafanya effects lazima uwe una picha iko kichwani (Picha ya effects unayotaka kufanya)
upo sahihi sana kaka,ila mambo ya camera operator au director ku visualize ideas kama zilivyo andikwa ndani ya script na kuziunda katika hali halisi ya kifilamu,hufanyika zaidi kwa zile big budget project.

kwa hizi low budget project zetu huku kwetu tz,idea nyingi huja mkiwa location na mda mwingine mnajikuta mnatoka kabisa nje ya script kuanzaia dialogue,actions,costume etc.

mfano kwa kwa low budget project,huwezi kwenda mamlaka ya ndege uwaombe au uwalipe ili wazuie ndege zisiruke kwa saa kadhaa ili wewe u shoot movie yako,lakini kwa apps kama EA unaweza uka shoot ilihali ndege zina ruka na kusababisha kelele na hata kuingilia ktk engle ya shot yako,halafu baadaye ukakaa kwenye comp yako na kufanya "sky replacement''.mwisho wa siku mambo yakaendela.as simple as that.

cheki hapa.
before the sky replacement.
b4.png

after the sky replacement.
after.png
 
Kuanza kujifunza After Effects haiitaji uwe na camera man, good camera man anakuja pale unapofanya real production sababu director ndio anakuwa na vision ya iyo shot. My Point ilikuwa Camera man na Director wana big role kwenye After Effects sababu kabla hujafanya effects lazima uwe una picha iko kichwani (Picha ya effects unayotaka kufanya)

Kuhusu After Effects CC ni version iliyotoka baada ya CS6, nilikuwa namuuliza sababu nime install na kuna ishu imenipa ugumu sehemu flani nilitaka anisaidie

Poa mkuu, mimi ndo najifunza ae, nitafatilia uzi huu kujifunza zaidi.

kadoda11 njoo tujumuike huku
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom