Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli


Ahsante kwa kunielewesha.
 
mkuu nipo arusha pia napata wapi castrol og au total nataka kwa ajili ya engine ya vtec sport car nadhan 5w30 ndo itafaa kama wadau walivosema apo juu
Total tembelea vituo vya total vilipo karibu na wewe...
Castrol sijawahi kutumia ila nasikia watu wakilalamika kuna feki...kwa uhakika wa Castrol OG nenda pale Manjis mitaa ya Metro Politan...wale wahindi hawana magumashi....Total pia inapatikana kirahisi maduka mengi ya spea za magari hapa town..
 
Nitajuaje hii injini imefanyiwa overhaul kuna jamaa yangu anataka kuniuzia TOYOTA CARINA YAKE.
 
Samahani mkuu kama nitakuwa nimekosea kukujibu. Ni hivi kampuni zote zinazotengeneza oil wana kila aina ya oil lakini changamoto inayotukuta sisi watanzania Mara nyingi tunapenda vitu vya bei rahisi sana na ambacho hakina ubora unaotakiwa kuliko kununua kitu chenye ubora na imara na iwekwe wazi tu oil nyingi zenye 5w30 ziko juu sana sio total,oryx castrol nk na bei yake zinauzwa kuanzia 55000+ kulingana na kampuni husika na kitendo cha kusema sae40 ndio imejaa madukani Mimi nakataa kwann usijaribu kutembea sehemu na maduka mengine kujionea? Kiukweli tunapenda vitu rahisi kuliko vya gharama na bora, mfn umenunua gari m20 unashindwa kubadili oil ya 80000 kwa kila baada ya miez miwil?
Mkuu hizi SAE ndo zimejaa dukani
 
Nitajuaje hii injini imefanyiwa overhaul kuna jamaa yangu anataka kuniuzia TOYOTA CARINA YAKE.
Boeing 747 Kakupa jibu kamili. Kununua gari mkononi mwa mtu bila kujua historia ya gari lile ni kucheza patapotea, hasa kwa vile sisi hatuna system ya kutunza record za matengezo ya magari yetu. La kufanya ni kumbana muuzaji akuuzie kwa bei nafuu zaidi ya market value kusudi kulipiza hayo usiyojua.
 

Shukrani mkuu
 
Mkuu Kichuguu
Gari yangu 4E engine nikikanyaga mafuta mshale unaishia nusu haimalizi yote na ni hivyo hivyo hata nikiendesha, itakuwa shida ni nini mkuu?
 
Mkuu Kichuguu
Gari yangu 4E engine nikikanyaga mafuta mshale unaishia nusu haimalizi yote na ni hivyo hivyo hata nikiendesha, itakuwa shida ni nini mkuu?
Fuel pump imeishiwa nguvu; haisukumi mafuta ya kutosha kwenye injector. Ama sivyo huenda fuel pressure regulator imelegea inarudisha mafuta mwengi kwenye tank
 
Fuel pump imeishiwa nguvu; haisukumi mafuta ya kutosha kwenye injector. Ama sivyo huenda fuel pressure regulator imelegea inarudisha mafuta mwengi kwenye tank
Shukran sana mkuu, je hii inaweza kuleta athari yeyote kwenye engine?
 
Shukran sana mkuu, je hii inaweza kuleta athari yeyote kwenye engine?
Kwa haraka haraka. Gari itahitaji wese jingi ili kusukuma maana presha ya msukumo wa pump ni mdogo, unaweza pia ona athari zake ukiwa unapandish mlima gari unaweza kukosa nguvu maana engine haipati mafuta kwa presa inayotosha, otherwise wese liwe jiingi.

Pia itahitaji ukanyage mafuta sana ili gari ichanganye

Katik mechanics ngoja Kichuguu atasema zaidi.
 
Shukran sana mkuu, je hii inaweza kuleta athari yeyote kwenye engine?
Haina madhara kwenye injini lakini ni hatari kwako hasa ukiwa unaedesha mlimani, kwani gari inaweza kushindwa kupanda ikaserereka kurudi nyuma. Vile vile katika hali hiyo gari linaweza kuzimika ghafla wakati wowote ukiwa njiani, ambayo inaweza kuharibu gearbox yako kama ni ya automatic
 
Shukran sana mkuu
 
Mkuu pole na kazi, Mimi natumia Toyota rav4, nilifanya overhaul apa majuzi lakin baada ya apo gari limekuwa na tabia ya kukata moto ninapokuwa kwenye mwendo mdogo, yaani inanilazimu nikanyage mafuta ya kutosha ili lisizime, hasa ninapoanza kuliwasha niondoke, sijajua tabia hii ya kukata moto imetokana na nini?
 
Ku-overhaul injini ya gari huwa ndiyo chanzo kikubwa cha uharibufu wa injini hiyo. Kwa sasa sitaweza kukupa jibu rahisi bila kulikagua gari lako. Hata hivyo baadhi ya sababu ndogondogo zinazoweza kusababisha gari kukata mafuta ni kama ifuatavyo.(a) Fuel pressure regulator ni mbovu inarudisha mafuta mengi kwenye tanki, kwa hiyo injini inakuwa na ukame. (b) Throttle position sensor haifanyi kazi vizuri, kwa hiyo computer haijui accelerator imebonyeswa kiasi gani, (c) Manifold Air pressure na Air flow sensor sensor ni mbovu, kwa hiyo computer haijui ndani kuwa hewa kiasi gani, na vile vile huenda Air cleaner yako siyo nzuri, haipeleki hewa ya kutosha kwenye injini.

Hayo ni matatizo madogo madogo ynayoweza kukupa kadhia hiyo, hata hivyo gari linatakiwa likaguliwe vizuri kuangalia iwapo ile overhaul iliyofanyika haikuleta matatizo zaidi.
 
Mkuu naomba kujuzwa kama kunauwezekano wa kubadili injini ya subaru legacy bl 4, 2004 na kuweka injini ya toyota na kama inawezekana ni injini upi inafaa zaidi.
 
Mkuu naomba kujuzwa kama kunauwezekano wa kubadili injini ya subaru legacy bl 4, 2004 na kuweka injini ya toyota na kama inawezekana ni injini upi inafaa zaidi.
Swali kama hilo nilishawahi kulijibu hapa

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…