Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Inawezekana umeweka oil nyingi sana. Vile vile kumbuka ile dip stick ndicho kifuniko imojawapo cha oil; kwa hiyo ukikitoa ina maana umefunua sufuria wakati oil inatokota, na iwapo sump imejaa kuliko kiasi ni lazima oil hiyo itaruka nje. Katika kucheck engine oil, inabidi injini iwe imezimwa. Dip stick ile ina alama mbili, ya asubuhi kabla hujawasha gari ni cold level, na ya wakati wowote mara baada ya kuzima gari ni hot level,
Shukran sana mkuu maana uswahilini mafundi waliniambia nibadilishe piston ring eti haitakiwi oil iruke gari ikiwashwa.
Hata hivyo chombo ipo safi haina hitilafu yeyote.
 
@kuchuguu, kuna gari ni Ford Focus ya 2003, CC 1,600. Gari inasumbua sana, sasa kuna advise ya kuchange engene na gear box ili system yote ibadilike.

Kuna fundi kanishauri kuweka injini ya Toyota:

Swali: Je ni injini ya gari gani Toyota inaweza kuwa compatible na iwe na CC between 1,300 - 1,600?
Nisikudanganye mzee wangu; swali lako liko nje ya ufundi wangu. Kuswap injini ni ujanja wa mitaani tu lakini kifundi siyo jambo zuri kwa sababu wakati wa kudesign gari, kuna factors nyingi hutiwa maanani ikiwa ni pamoja na aina ya injini itakayotumiwa, vibration level zake, engine mounts za kutumia, na kadhalika. Kuhamisha injini za Toyota na kuziweka kwenye Ford siyo mambo ambayo license yangu inaruhusu kufanyika.
 
Asante bosi, very profession response.

Be blessed.
 
Kichuguu, magari used karibia yote madogo yanayokuja kutoka Japan yanakuja na stika kuonyesha recommended engine oil ni ~ W 30 na Japan ni baridi sana kuliko Tz, inakuaje tena unatushauri tuweke ~ W 20 ? Wakati hiyo ni kwa ajili ya nchi baridi sana ? Inasemekana oil recommended kwa Tropical countries like Tz ni ~ W 40 .. Tupe ufafanuzi wa hilo. Ukizingatia hata viwanda vya hapa nchini wanaozalisha oil utakuta wanazalisha zaidi no 40, sina hakika kama wanazalisha no 30 au hata no. 20 ..
 
Sijasoma taarifa ulizoletwa kutoka Japan kwenye gari lako, kwa hiyo inawezekana sitakupa jibu kamili la swali lako. Kila gari lina grade ya oil yake kulingana na tolerance ya parts zinazotumika katika injini ya gari lile. Ndiyo maana mara kadhaa nimewaambia watu wasome vitabu vya magari yao, hakuna oil ya kutumika katika magari yote, kila gari lina optimal oil yake.

Iwapo una gari ambalo hujui oil yake, ndipo experience ya mafundi kama mimi inapokuja. Elewa kuwa oil zote za injini zina namba mbili, moja inayoishia na herufi W na nyingine haina herufi yoyote; kwa mfano 5W-20. Namba zile maana yake kwa watu wa Engineering na Physics zinaonyesha viscosity, au kwa lugha rahisi ya kiswahili ni utelezi wa oil hiyo. namba ya kwanza yenye W, ina maana ya utelezi wakati wa Winter au joto la chini sana, na namba ya pili ni utelezi wakati injini inafanya kazi zake sawsawa.

Kwa Tanzania ambako hakuna Winter, watu tunatakiwa kuwa tunatazama zaid ile namba ya pili ambayo nimesema ni kati ya 20 na 30 tu kwa gari la kawaida. Ile namba inayoishia W inakusaidia wakati wa baridi, na kwa Tanzania hatuna baridi kali kwa hiyo tunahitaji namba ya chini tu. ndiyo maana nashauri kati ya 5W na 10W tu.

Sijui sticker unazopata wewe kutoka kwa exporter wako wa Japan kwani iwapo anajuwa kuwa anauza magari hayo kwenye maeneo ya tropical, ninaamini kuwa oil recommendation yake haitakuwa ile namba inayoisha na W. Kwa gari amabayo ni reconditioned, inawezekana mafundi wakapandisha viscoscity kidogo ili kujaza mapengo ya ukuukuu wa injini. Iwapo namba ya pili ya oil ni 40 au 50 ina maana kuwa injini hiyo ni chakavu sana,
 
Jina langu siyo Kitunguu aisee, hebu badilisha; mimi ni Kichuguu, ".....huwezi kulinganisha Kichuguu na mlima Kilimanjaro"

Bila shaka gari yako huwa inatoa moshi mwingi sana, yaani kuna oil inavuja na kuingia kwenye combustion chamber na kuunguzwa pamoja na mafuta. Iwapo injini yako ina nguvu kama kawaida, basi kuna vipete fulani ambamo valve stem hupita (vinaitwa valve guides) huenda vimepanuka sana na kuacha mwanya wa oil kupenya ndani ya injini. Fundi wako akifungua cylinder head cover anaweza kuvikagua na kuona kama vimepanuka. Ni rahisi kuvibadilisha kwani viko kwenye cylinder head, ila utahitaji cylinder head gasket mpya.

Kama Injini haina nguvu kama zamani na vile vile inakula mafuta mengi sana basi huenda piston rings zako zimekwisha; hapo utahitaji kazi kubwa kidogo ya karibu na overhaul kwani itabidi ufungue injini yote kuweka piston rings mpya. Usifanye makosa ukabadilisha piston kwani unaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi. Kazi ya namna hiyo fundi anaweza kuifanya kikamilifu bila kuangusha injini kabisa; utahitaji cylinder head gasket mpya pia.

Piston rings hufa iwapo hubadilishi air filter yako mapema kwani huruhusu vumbi (ambalo ni silica na ni ngumu kama msasa) kuingia ndani ya cylinder na kusaga hizo piston rings na vile vile iwapo hubadilishi engine oil katika muda unaotakiwa.
Asante mkuu kichuguu na sorry kukosea jina lako
 
Tunapozungumza baridi kwenye injini ya gari, Tanzania hakuna baridi, siyo hata lile la Makambako. Kulingana na mileage iliko unaweza kutumia oil yoyote kati ya 5W-20, 10W-20,5W-30, na 10W-30. Kama una zaidi ya km 180,000 tumia ama 5W-30 au 10W-30, na kama ni chini ya km 180,000 tumia 5W-20, 10W-20. Nakushauri zaidi utumie hizo nilizowekea msisitizo

Shukrani sana mkuu... ni chini ya KM 180,000. Nitazingatia ushauri wako
 
hivi mkuu unaweza badilisha engine toka six syllinder ya brevis na kuweka four cylinder ya Toyota Grande

Haya maswali ya modificationa nimekuwa nayaepuka kwa sababu license yangu hairuhusu kufanya modification ya gari, bali majukumu yangu ni kujaribu kuirudisha injini katika ubora wake. Modification ni utundu wa mitaani tu ambao hausomewi; jaribu kutafuta mafundi wenye uzoefu wa modification wanaweza kukusaidia.

Kitaalamu ni kuwa modification yoyote ya kutumia injini tofauti na iliyokusudiwa huwa inakuja na matatizo kadhaa; makuu ikiwa ni mtikisiko wa injini kuzidi kiasi, ambapo baada ya cycles kadhaa inaweza kuvunja au kupindisha chasis ya mbele au front subframe ya gari lako.
 
mkuu kwema nina honda accord 2000 uk version nimefanya service nimebadil sensor zote nilizoambiwa nibadili baada ya kuchekiwa kwenye computer , gari bado inawasha check engine nikiwauliza tatizo wananiambia oil nilioweka nikiweka castrol oil inayokaa kwenye kidumu cheupe mtakutimia no za iyo oil mara wanambie coz coolant fan sensor imeungea direct ndo maana inawasha taa je jinu lipi ni sahihi mkuu Kichuguu
 
Kwa gari ya mwaka 2000, iwapo gari inatembea vizuri tu lakini inawasha taa hiyo basi inawezekana kuwa tatizo lako ni Catalytic converter kama nilivyomjibu mtu mwingine kwenye post namba #7 hapa

Catalytic converter huishiwa nguvu baada ya muda wa kuazia miaka minane hadi 15. Haina madhara kwenye gari bali tu ni kuwa gari linakuwa linachafua mazingira sana, na vile vile ile kero ya kuwa na taa ya Check Engine.

Kama umeshafikisha km zaid ya 180,000, oil ya kutumia itakuwa ni ama 5W-30 au 10W-30; usizidishe hapo; kuna mtu kasema hapa kuwa aliambiwa aweke 20W-50 ambayo ni oil nzito sana na inachangia kuchosha injini ya gari yako haraka sana.
 
Haya maswali ya modificationa nimekuwa nayaepuka kwa sababu license yangu hairuhusu kufanya modification ya gari, bali majukumu yangu ni kujaribu kuirudisha injini katika ubora wake. Modification ni utundu wa mitaani tu ambao hausomewi; jaribu kutafuta mafundi wenye uzoefu wa modification wanaweza kukusaidia.

Kitaalamu ni kuwa modification yoyote ya kutumia injini tofauti na iliyokusudiwa huwa inakuja na matatizo kadhaa; makuu ikiwa ni mtikisiko wa injini kuzidi kiasi, ambapo baada ya cycles kadhaa inaweza kuvunja au kupindisha chasis ya mbele au front subframe ya gari lako.
Asante mkuu
 
Hiyo nina uhakika wa karibu 90% kuwa huenda siyo kweli ingawaje inawezekana kuwa ni kweli kwa vile sijui aina ya mlio wenyewe unaopata. Ile bendix ya starter ikiharibika kufikia kiwango hicho cha kushindwa kurudi baada ya kustart, basi vile vile huwa inashindwa kusukuma wakati wa kustart, halafu hiyo haitokei kirahisi vile.
Nimejaribu leo kuingia chini ya gari ili kusikiliza ule mlio unaogonga unatokea wapi,nimegundua unatokea ndani ya oil sump.Niliwahi pia kumuuliza fundi mmoja akaniambia inawezekana chekeche la oil sump lina mauchafu kwahiyo oil inapita kwa shida wakati wa kuwasha gari kwahiyo ikipata moto inalainika na ule mlio ndio maana huwa unaacha,ushauri alionipa nikufungua na kuisafisha,hapo napo ni vipi mkuu?pia ulinishauri niangalie lile bati la juu ya exhause pipe kama limelegea,lile liko tight kabisa na nut zote ziko vizuri...
 
Back
Top Bottom