Niulize chochote jinsi ya kuclear mzigo mpakani

Niulize chochote jinsi ya kuclear mzigo mpakani

Nataka kujua sector ya vipodozi utaratibu upoje pale tunduma kwa mizigo inayotoka congo. Na kwann vipodoz wanavitolea macho sana. Na transporter yupi mzur from tunduma to dar
 
Utaratibu unakuwa vioi unapokuwa umenunua Trector kutoka zambia au msumbiji, ni gharama zipi ambazo zitapaswa kulipia... Maana trector huwa halilipiwi kodi, na process inaweza kuchukuq siku ngapi
Kama Ina exemption... Basi document zitapelekwa Kwa agent kwajili ya assessment Baadaye apo tunafuata idara kama tbs hapa ndo panakuaga na malipo na idara zingine ku prove tu process siku Moja tu.. Mzigo unatoka
 
Nataka kujua sector ya vipodozi utaratibu upoje pale tunduma kwa mizigo inayotoka congo. Na kwann vipodoz wanavitolea macho sana. Na transporter yupi mzur from tunduma to dar
Vipodozi autoboi kupitia custom aiwezekani ni illegal..... Labda kama utatumia njia zingine
 
Nikiagiza gari baada ya kulipa ushuru wa tra je natakiwa kuwa na kiasi gani ili kuitoa
Kupitia boda yoyote lazima uwe na agent fee kwajili ya clearance dollar 100 na malipo kama tbs 180k... Hela ya vihcle officer 50k apo inasajiliwa kabisa
 
Mkuu kama nivoeleza hapo sijawahi fanya clearance bandarini…kazi zangu ni clearance ya boda za mipakani ..kwasasa Niko boda ya TUNDUMA
Kwa upande wa bandarini
Kwanza tuanzie hapa:
Ukinunua mzigo nje mf:china utapewa invoice then ukilipa utapewa receipt (lisiti)
utafanya booking ya space ktk meli inayokuja Dar mara baada ya kupata nafasi utapeleka mzigo wako , ukipakiwa tu ndani ya meli baada ya kulipia shipping charges/freight charges (Kuna mambo mengi hapo ktkt bima, Hali ya mzigo n.k)
unapewa document inaitwa bill of lading (b/l) kidhibitisho kuwa mzigo umepokelewa ndani ya meli,

Mara baada ya meli kumaliza kupakia chief officer huandaa document inaitwa cargo manifest ya mzigo wote utakaoshuka Tanzania na kumtumia Agent wa meli hiyo aliopo Tanzania, Agent huyu atai upload document hiyo katika mfumo wa TRA (TANCIS) na mara Moja mzigo hufanyiwa makadilio ya Kodi.

Mzigo unapowasili ktk bandari ya Tz wote walio na mzigo ktk meli husika hupata notification wakijulishwa mzigo kuwasili

Wewe mwenye mzigo hurusiwi kuingia bandarini hivyo basi utazitumia kampuni za clearing ambazo ndio zilizoruhusiwa Kwa niaba ya mteja ambapo kampuni zote zimesajiliwa na TPA

Wewe mwenye mzigo utabisha hodi kampuni mojawapo ukiwa na documents zifuatazo Barua inayodhibitisha kuwapa ruhusa kampuni hiyo ya ku clear mzigo wako kitambulisho chako, bill of lading, invoice na receipts ya mzigo n. k

CFA rasimi watachukua majukumu Yako Kwa maelewano yenu nao wataanzia shipping line ya hiyo meli Ili kupata document inaitwa Delivery order pia ataanda document inaitwa assessment document, ata submit ktk mfumo wa TRA then Tra wakijiridhisha wanamrudishia majibu CFA kama assessment document yake imekubaliwa au imefanyiwa marekebisho bas CFA akikubaliana TU

atadhuru office za foroza za Tra kwa ajili ya physical verification ya mzigo wakijilizisha uta request control number utalipa ushuru na kupewa release Order hapo Sasa unakuja upande wa Bandari utaripa port charges kama storage kama ipo au cargo removal charges nk

Hapo ndipo utafanya kitu kinaitwa Truck announcement hii ni kuomba mamlaka ya bandari uingize gari bandarini utakubaliwa Kwa kupewa gate pass A ikiwa na taarifa za gari dereva mmiliki, na mzigo

utaingiza gari kupitia document hiyo utapakia mzigo wakati was kutoka utaiacha hiyo gate pass A geti la mwisho la askali mf gate no3 happy ndipo mteja atakuwa tayali kuupokea mzigo wake.

kumbuka 95%ya process hizo ni online
unaweza kuzifanya huku ukiwa kitandani unakula popcorn

kazi iendeee.
 
Habari…tupeane Muongozo kidogo wa mizigo inayotoka nchi hizo kuingia Tanzania kupitia boda ..Document zote za mzigo husika kutoka kampuni ya nchi tajwa hapo juu hutumwa kwenye kampuni ambayo iko Tanzania kwajili ya kufanyiwa assessment kwenye mfumo wetu wa TANSIS.Hapo ndipo mzigo huanza safari ya kuja Tz kwa kupitia boda zote kufuatana na nchi mzigo umetoka hadi unafika boda ya Tz.Process inafuata ni wakala wa forodha aliepo boda husika ya Tz kuanza kazi.

1.Kwenda kwa supervisor alisome file lenye document zote then akupangie afisa ambaye atenda kuangalia mzigo phyiscally then apige picha na kuandika alichokiona nakutuma makao makuu Dar kwajili ya wao kukadilia mapato

2.Wakiwa wanaendelea kusubili majibu kutoka makao makuu process za ukaguzi na idara zingine zinazohusika na mzigo mfano TBS,TISS,AGRIC,TFS,TPDF,POLICE ..nk na wao watasain form ya phyical examination kwa kuandika na kusign walichokiona.

3.Kodi ikishalipwa then kampuni husika ita compare manifest yao na kodi ikireflect kwa supervisor wa boda husika then wakala wa forodha atarudi kwa afisa wa kwanza alopangiwa kwajili ya kuandika final remarks.
4.Then wakala wa forodha atarudi na file kwa supervisor kwajili ya kuprit release order mchezo unakuwa umeisha.

5.Then mzigo unaanzakutolewa gate la mwisho kwa afisa aliepo siku io getin kwa kupewa realease kwajili ya ku gate out gari inatoka na mzigo

Nb..Kama gari ni ya kigeni lazima ikate roadtoll ya Kutembelea Tz bei inafuata na umbali wa safari…

[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Naomba kujua ukaguzi wa tiss na tpdf unafanyikaje?
 
Nasikia harufu ya mtu kupigwa na kitu kizito kichwani
Acha Uswahili na kuharibu Mishe za Watu, wewe kama unakaa Mpwapwike, endelea na kilimo.

Mtu anatangaza Huduma zake, ambazo ni za kawaida na zinajulikana, wewe hapo Utaperi umeuona wapi!?
 
Naomba kujua ukaguzi wa tiss na tpdf unafanyikaje?
Wale wanaverify Kwa macho tu ile physically basi wana saini kwenye fomu unakuwa nayo Kwa kila afsa aliona mzigo tunaita physical examination form
 
Kwa upande wa bandarini
Kwanza tuanzie hapa:
Ukinunua mzigo nje mf:china utapewa invoice then ukilipa utapewa receipt (lisiti)
utafanya booking ya space ktk meli inayokuja Dar mara baada ya kupata nafasi utapeleka mzigo wako , ukipakiwa tu ndani ya meli baada ya kulipia shipping charges/freight charges (Kuna mambo mengi hapo ktkt bima, Hali ya mzigo n.k)
unapewa document inaitwa bill of lading (b/l) kidhibitisho kuwa mzigo umepokelewa ndani ya meli,

Mara baada ya meli kumaliza kupakia chief officer huandaa document inaitwa cargo manifest ya mzigo wote utakaoshuka Tanzania na kumtumia Agent wa meli hiyo aliopo Tanzania, Agent huyu atai upload document hiyo katika mfumo wa TRA (TANCIS) na mara Moja mzigo hufanyiwa makadilio ya Kodi.

Mzigo unapowasili ktk bandari ya Tz wote walio na mzigo ktk meli husika hupata notification wakijulishwa mzigo kuwasili

Wewe mwenye mzigo hurusiwi kuingia bandarini hivyo basi utazitumia kampuni za clearing ambazo ndio zilizoruhusiwa Kwa niaba ya mteja ambapo kampuni zote zimesajiliwa na TPA

Wewe mwenye mzigo utabisha hodi kampuni mojawapo ukiwa na documents zifuatazo Barua inayodhibitisha kuwapa ruhusa kampuni hiyo ya ku clear mzigo wako kitambulisho chako, bill of lading, invoice na receipts ya mzigo n. k

CFA rasimi watachukua majukumu Yako Kwa maelewano yenu nao wataanzia shipping line ya hiyo meli Ili kupata document inaitwa Delivery order pia ataanda document inaitwa assessment document, ata submit ktk mfumo wa TRA then Tra wakijiridhisha wanamrudishia majibu CFA kama assessment document yake imekubaliwa au imefanyiwa marekebisho bas CFA akikubaliana TU

atadhuru office za foroza za Tra kwa ajili ya physical verification ya mzigo wakijilizisha uta request control number utalipa ushuru na kupewa release Order hapo Sasa unakuja upande wa Bandari utaripa port charges kama storage kama ipo au cargo removal charges nk

Hapo ndipo utafanya kitu kinaitwa Truck announcement hii ni kuomba mamlaka ya bandari uingize gari bandarini utakubaliwa Kwa kupewa gate pass A ikiwa na taarifa za gari dereva mmiliki, na mzigo

utaingiza gari kupitia document hiyo utapakia mzigo wakati was kutoka utaiacha hiyo gate pass A geti la mwisho la askali mf gate no3 happy ndipo mteja atakuwa tayali kuupokea mzigo wake.

kumbuka 95%ya process hizo ni online
unaweza kuzifanya huku ukiwa kitandani unakula popcorn

kazi iendeee.
Shukrani Kwa Elimu apo sisi huku MA agent ndo tunasubiliaga Movement sheet, TI, invoice na b/l kwajili ya kutengenezea documents ya mzigo upande wa boda ya Zambia Au atakama mzigo ni transit Zambia tunachaji dollar 80,,, hapo mzigo ndo unaweza kwenda nchi yoyote Zambia, Congo, Zimbabwe South Africa umo .....HIO NI MIZIGO YA TRANSIT
 
Acha Uswahili na kuharibu Mishe za Watu, wewe kama unakaa Mpwapwike, endelea na kilimo.

Mtu anatangaza Huduma zake, ambazo ni za kawaida na zinajulikana, wewe hapo Utaperi umeuona wapi!?
Kama kazoea kuuza simu used akomae nazo haya mambo yatampasua kichwa... Sisi tunafanya kazi na MA Boss wa kibongo, wahindi waarabu ata amjawahi kuonana ata siku Moja ila anatuma hela na magari yake yanavuka na kurudi kila siku,,, UAMINIFU TU
 
Kipodozi kinaingiaje Tunduma na kupita mpaka mikoa mingine boss?

Kahawa inatokaje bongo kuingia Zambia?
 
Kipodozi kinaingiaje Tunduma na kupita mpaka mikoa mingine boss?

Kahawa inatokaje bongo kuingia Zambia?
Kipodozi ni njia za magendo tu akuna njia nyingine mkuu

Kahawa kama unapeleka Zambia inafuatana na mzigo upo kiasi gani?
Kama ni mwingi unafuta process za exportation tu
 
Back
Top Bottom