Nitatumia siku ngapi Uhamiaji kama sitotoa Rushwa?

Mr Chromium

JF-Expert Member
Aug 20, 2020
2,090
2,705
Nauhitaji na passport lakini kama ujuavyo hizi idara bila chochote kitu utasoteshwa! Nataka nipate passport, na kama ilivo ni haki yangu bila kutoa hata senti. Kitachonigharimu ni muda tu, nitahesabu hapa siku nitazotumia. Pia unaweza share maswahibu yako.

Siku ya Kwanza
Nimefanya application online na kujaza kila taarifa humo na kuambatanisha vyeti na vitambulisho.

Siku ya Pili
Nimekuja hapa lakini tumesimamishwa nje tumeambiwa tumechelewa na mlinzi. Sasa hivi ni saa 9 na nusu( 3:30pm). Tumeambiwa mwisho saa 8 walioko ndani au waliokwisha anza ndio wataendelea hadi muda wa kufunga.

Nimegeuza narudi home…. Nimetumia elf 4000 narudi bila bila.

Siku ya Tatu
Nimefika saa 6 mchana. Zimekusanywa form zetu wote tumeambiwa tukasubiri kwenye mabenchi kuitwa. Wenye maelekezo wanawaita maofisa wanaongea vitu, ofisa anabeba form yake separately kwa ajili ya kushughulikia. Wengine tunasubiri foleni.

Kunabkaukakasi ka hapa na pale hasa baadhi unakuta anaenda moja kwa moja dirishani mwingine ananyooshewa kidole aende tu, ila si mbaya.


Nimeitwa dirishani NO: x nimeambiwa pamoja na kua nimejaza mtandaoni vyeti vyote bado natakiwa niwe na Hard copy na isainiwe na mwanasheria.
NB: sasa hii ya online sijui ya nn? unajaza unaweka viambatanisho lakin ukija huku wanataka hard copy.HAINA MAANA AISEE HII MIFUMO YA DIGITAL KWETU TUNAFANYA KAMA UTARATIBU LAKIN SI KURAHISISHA MAMBO.

Kifupi form haijapewa namba yaan tumesubiri muda wote just kuja kuambiwa hivo toka saa 6 saizi saa8:48 (2:48 am).Kifupi nimekasirishwa n hili kwan tulipoenda mapokezi kuna mlinzi mmoja alikua kuna baadhi ya watu anawachambulia na kuwatudisha au kuwaambia vitu vingine vya kuambatanisha kabla hawajaenda kupanga folen. Chaa ajabu akatokea afisa akakusanya mafom ya wengine wote na kusema kukasubiri HUU UTARATIBU SIYO.
Wakat aliyeko mapokezi angeweza kutoa maelekezo pale kwa watu waliojaza form mtandaon wafanye nn kabla hawaleta form au kwa wanaoanza. Kifupi kuna upotezaji wa muda hapa sana.
Ok kwaiyo sasa kazi ni kumuona mwanasheria na kuprint hard copy na mwisho wa kaz ushakaribia. Kesho n sikukuu hawafungui….. hii imeenda had jumatatu.

SIKU YA NNE:
Leo ni sikukuu hawafungui ofice aisee….Lakin na ihesabu si makosa yangu
 
Unaweza kusubiri siku laki nne nikiwa na maana unaweza usiipate kabisaaaa!!

Bila rushwa kujaza form na kuwa na uwezo wa kusubiri kwa siku nyingi sio vigezo pekee vya kukuhakikishia kipata pasipoti Tz
 
Huhitajiki kutoa chochote kitu!!...kwa hatua uliyoifikia unahitaji wiki moja au mbili kupata pasi yako, kama nyaraka zote ulizowasilisha hazina utata....Futa kabisa mawazo la kutoa rushwa wakati hakuna aliyekuomba rushwa!. 😳
 
Nauhitaji na passport lakini kama ujuavyo hizi idara bila chochote kitu utasoteshwa!!
Nataka nipate passport kama ilivo ni haki yangu bila kutoa hata senti.Kitachonigharimu ni muda tu,……
Nitahesabu hapa siku nitazotumia,,, Pia unaweza share maswahibu yako….

SIKU YA KWANZA
Nimefanya application online na kujaza kila taarifa humo na kuambatanisha vyeti na vitambulisho.


SIKU YA PILI
Nimekuja hapa lakini tumesimamishwa nje tumeambiwa tumechelewa na mlinzi .
Saizi ni saa9 na nusu ( 3:30pm).Tumeambiwa mwisho saa 8 walioko ndan au waliokwisha anza ndo wataendelea had muda wa kufunga.

Nimegeuza narudi home…. Nimetumia elf4000 narudi bila bila


SIKU YA TATU
Nimefika saa 6 mchana. Zimekusanywa form zetu wote tumeambiwa tukasubiri kwene mabenchi kuitwa .Wenye maelekezo wanawaiya maofisa wanaongea vitu ofisa anabeba form yake separately kwa ajili ya kushughulikia.Wengine tunasubiri folen.Kunabkaukakasi ka hapa na pale hasa baadhi unakuta anaenda moja kwa moja dirishan mwingine ananyooshewa kidole aende tu…. Ila si mbaya
kupanga ni kuchagua.

we umeona ipi rahisi , ya muda mfupi na sio gharama?

kutoa Rushwa au kufuata utaratibu?
 
Fuata utaratibu na usitoe rushwa kwa yeyote.

Kupitia wewe, utatoa elimu kwa wahitaji wengine kuendelea na utaratibu wa kawaida.
 
Walinifata kutoa nikawadindia baadae wakanipiga picha eti naulizwa wewe ni mtu wa nani? Black fucking Afghanistan war head. Ngombe wale. Nikawajibu wa boss wenu.
 
Back
Top Bottom