Nampongeza sana Mtumishi huyu wa Uhamiaji

Planett

JF-Expert Member
Mar 20, 2014
10,424
15,977
Bila shaka kila mmoja ni mzima wa afya, kwa wanaosumbuliwa na matatizo ya kiafya na wenye changamoto nyingine Mwenyezi Mungu awasimamie.

Ni kawaida pale ambapo Watumishi wa Serikali kwenye taasisi na mashirika wanapovurunda basi huwa malalamiko yanaletwa hapa kwa lengo kwamba wahusika wataona na kujirekebisha.

Leo naomba nimpe maua yake binti mmoja mtumishi wa Uhamiaji mkoa wa Lindi ambae kwa mujibu wa nametag yake anaitwa Moza.

Ni muda sasa umepita nililazimika kubadili pasport yangu kutoka ile ya zamani na kupata ya sasa (ya kidigitali). Kama kawaida nikajaza form mtandaoni, nikaprint na kupeleka uhamiaji Lindi. Reception nikamkuta huyu binti ambae kwanza ana customer care ya kipekee sana. Nikamkabidhi form zangu kwa pamoja tukapitia kipengele kimoja baada ya kingine ili kujiridhisha na usahihi wa taarifa zangu kabla hajazipokea kwa hatua zaidi.

Pale ambapo hapajakaa sawa alinielekeza kwa ustaarabu na upole sana (sio ile kiafande afande), attachments pia ambazo nilisahau au ambazo zilikuwa na kasoro nilielekezwa nini cha kufanya ilifika hadi nikasahau kuwa nipo Ofisi ya Jeshi na anaenihudumia ni CPL.

Finally in less than two weeks passport ikawasili Lindi na nikaenda kuichukua (hapa nisisahau kuwapongeza Uhamiaji in general).

Wewe dada Mungu akujaalie afya njema na akulinde siku zote. Japo ni muda umepita ila sio mbaya leo nimeona nikupe maua yako uyanuse kabisa.

Wassalaam.
 
Me kupata passport imekua changamoto kidogo coz cheti changu cha kuzaliwa kilikosewa tarehe ya kuzaliwa
Nkaenda Rita kubadili cheti cha kuzaliwa nkafanikiwa nkapeleka Kule uhamiaji lakini cha ajabu Passport ikatoka ikiwa imeandikwa Ile tarehe ya mwanzo ya kuzaliwa yenye makosa (cheti cha mwanzo)
Nimeirudisha ile passport uhamiaji ili waanze upya mchakato

Wameniambia kuwa passport kukosewa tarehe ya kuzaliwa sio big issue lakini mimi sijaridhika kabisa nimekubali kuingia hasara ya kujaza form upya
 
Uhamiaji ni JESHI?
 
Bwege wewe!
 
ninamfahamu vizuri sana dada huyo, amejaaliwa utu/ubinaadam lakini pia ni mrembo kweli kweli na sauti yake mash allah.
 
Back
Top Bottom