Nitasema ukweli fitina kwangu mwiko "bado neno hili lina nguvu?"

mutabilwa

JF-Expert Member
Jul 11, 2011
305
80
Habari wana JF ningependa tujadili maneno haya machache ya chama chetu tawala CCM kama kweli yanaitaji kuendelea kutumika kwa nyakati hizi ambazo chama hiki tawala kinapitia.Nimelazimika kupost hii topic si kwamba siipendi CCM wala wanachama wake bali naitaka ijaribu kuutafakali msemo huu inaoutumia mara kwa mara inapokuwa katika vikao vyake utaona bango kubwa nyuma ya Meza kuu lina ujumbe huu.Kwa upande wangu naona msemo huu unakiua chama kwani wapo wengi wanaosema ukweli ndani ya CCM lakini wanapingwa, naongea kwa mfano: Mtakumbuka Mh Edward Lowasa aliposema kukosekana kwa ajira kwa vijana no BOMU linalosubiri Kulipuka lakini alipingwa sana na wana ccm akiwemo mmoja wa mawaziri wa Jk.
JF naomba tujadili kuanzia hapo ili nasi tusiondani ya CCM tutimize msemo huu wa nitasema ukweli fitina kwangu Mwiko?
Karibuni.
 
Back
Top Bottom