CCM tulifanya kosa kubwa sana 2015, tusirudie tena. Chuki iliyopo ni kubwa sana

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Kuna mambo ambayo wana CCM wenzangu hawataki kabisa kuyasoma wakiogopa pengine kwa kudhani kuwa yatakigawa chama ima yatachochea chuki baina yetu.

Waswahili wanasema, unafuga chatu mwisho wa siku anakugeukia na kukumeza wewe. Huu ni usemi ambao ni kielelezo tosha cha ukweli na uhalisia kwetu wana CCM na taifa kwa ujumla.

Tulifanya kosa kubwa sana kumpa mwendazake nafasi ya kugombea Urais, JK lawama hizi hatazikwepa maana yeye kwa mdomo wake ndiye alikiri kumpatia nafasi hiyo na hatimaye baadaye kupitishwa na mkutano mkuu wa halmashauri kuu ya chama taifa. Hakika tutakubaliana kua pamoja na mazuri ambayo aliyafanya lakini kwa sasa tunaona taifa ni kama linazaliwa upya, taifa ndio kama limepata uhuru.

Kiwango cha chuki kilichopandikizwa kwa takribani miaka 5 iliyopita ni cha hali ya juu sana. Kwa tunayokutana nayo hivi sasa ni majuto na kweli majuto ni mjukuu, tunalia na mjukuu wa majuto.

Umepita katika kipindi ambacho hatujawahi kuona watu watu wakitekwa na kupotezwa kabisa, kipindi ambacho hatujawahi kuona mtu anatandikwa risasi hadharani mchana kweupe, yaani kipindi ambacho kwa mfumo wa vyama vingi chama tawala tunachukua ushindi kwa nguvu hata mahali tusikokubalika, kipindi ambacho chama tawala tunapitisha watu kupita bila kupingwa nchi nzima kwa mara ya kwanza, kipindi ambacho viongozi wa chama wanataka hadharani watu flani wanapaswa kuuawa kwa tofauti tu za kisiasa, kipindi ambacho mkuu wa wilaya au mkoa anaingia kwenye ofisi za watu usiku na kupora mali za watu kibabe. Haya yote nyuma hayakuwepo.

Kwakweli mzee aliiweka nchi mahali pabaya sana. Ni sawa alikua mkali kwenye rasilimali za nchi lakini siyo angetupeleka tulikofika hivi sasa, ninagundua utu wa binadamu ni muhimu kuliko hata barabara au daraja tunalojengewa. Mzee alipaswa kuwa waziri mkuu lakini pawepo na mtu wa kumpa maelekezo na siyo yeye kujiamulia mambo.

Tumelipuuza janga la ugonjwa wa Corona lakini Mola ndio anajua liliondoka na nani hata kama nami nimepoteza ndugu kadhaa kwa uthibitisho wa madaktari. Pamoja na umri wangu pia kujitupa mkono lakini kweli siwezi kuiweka kando na hata vijana wangu na wajukuu nimewasimulia ili kesho wajue wataishije kwa kuushinda unafki,fitina pamoja na tamaa.

Nimalize kwa kusema kwamba CCM tujifunze kwa yaliyopita, kama ni Urais tutazame tutazame matendo ya vijana wetu waliopo katika nafasi mbalubali za serikali na chama. Wapo viongozi wa chama, mawaziri, Wakuu wa wilaya na mikoa, wakurugenzi, mbalizi nk.

Kwenye makundi haya hatutakosa wagombea makini. Tusiangalie utendaji tu bali tutazame na utu na kiongozi wa kuliungamisha badala ya kuligawa taifa.

Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko!

Binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja!
 
Kuna mambo ambayo wanaccm wenzangu hawataki kabisa kuyasoma wakiogopa pengine kwa kudhani kua yatakigawa chama ima yatachochea chuki baina yetu...

Nimalize kwa kusema kwamba CCM tujifunze kwa yaliyopita, kama ni Urais tutazame tutazame matendo ya vijana wetu waliopo katika nafasi mbalubali za serikali na chama. Wapo viongozi wa chama, mawaziri, Wakuu wa wilaya na mikoa, wakurugenzi, mbalizi nk. Kwenye makundi haya hatutakosa wagombea makini. Tusiangalie utendaji tu bali tutazame na utu na kiongozi wa kuliungamisha badala ya kuligawa taifa.
Kwa kumbukumbu tu ndugu yangu. Hebu pitia huu uzi:

Huko ndiko CCM ilikotufikisha...
 
Mkuu mara nyingi tumezoea kuona baadhi ya nchi na hata Tanzania wagombea urais ama huwa wana Diplomasia au wanasiasa wabobezi.

CCM mwaka 2015 wameteua mgombea asiyejua siasa wala diplomasia, hilo limeumiza nchi.

Mh rais wa awamu ya 5 hakuwa na ujuzi wa kufanya siasa za ushindani wala hakuwa akijua Diplomasia ya kuishi kwa maelewano na maadui wa ndani na nje ya nchi bila kuwaonyesha chuki.

Ameendesha nchi hii kama jenerali wa jeshi ambaye uongozi wake haukutokana na Katiba ya nchi.

Katiba ilipuuzwa, sheria zimewekwa kando eti mpaka nchi inyooke.

CCM lazima waje waombe radhi na hilo liwe funzo kwao siku zijazo.
 
Mkuu mara nyingi tumezoea kuona baadhi ya nchi na hata Tanzania wagombea urais ama huwa wana Diplomasia au wanasiasa wabobezi...
... uzalendo!
😅
1623018848721.png
 
Mkuu mara nyingi tumezoea kuona baadhi ya nchi na hata Tanzania wagombea urais ama huwa wana Diplomasia au wanasiasa wabobezi.
CCM mwaka 2015 wameteua mgombea asiyejua siasa wala diplomasia, hilo limeumiza nchi.
Mh rais wa awamu ya 5 hakuwa na ujuzi wa kufanya siasa za ushindani wala hakuwa akijua Diplomasia ya kuishi kwa maelewano na maadui wa ndani na nje ya nchi bila kuwaonyesha chuki.
Ameendesha nchi hii kama jenerali wa jeshi ambaye uongozi wake haukutokana na Katiba ya nchi.
Katiba ilipuuzwa, sheria zimewekwa kando eti mpaka nchi inyooke.
CCM lazima waje waombe radhi na hilo liwe funzo kwao siku zijazo.
Hata generali wa jeshi hufuata taratibu za kijeshi. Mwendazake aliendesha nchi kama familia yake.
 
Kuna mambo ambayo wanaccm wenzangu hawataki kabisa kuyasoma wakiogopa pengine kwa kudhani kua yatakigawa chama ima yatachochea chuki baina yetu.

Waswahili wanasema...unafuga chatu mwisho wa siku anskugeukia na kukumeza wewe. Huu ni usemi ambao ni kielelezo tosha cha ukweli na uhalisia kwetu wanaccm na taifa kwa ujumla.

Tulifanya kosa kubwa sana kumpa mwendazake nafasi ya kugombea Urais, JK lawama hizi hatazikwepa maana yeye kwa mdomo wake ndiye alikiri kumpatia nafasi hiyo na hatimaye baadaye kupitishwa na mkutano mkuu wa halmashauri kuu ya chama taifa. Hakika tutakubaliana kua pamoja na mazuri ambayo aliyafanya lakini kwa sasa tunaona taifa ni kama linazaliwa upya, taifa ndio kama limepata uhuru.

Kiwango cha chuki kilichopandikizwa kwa takribani miaka 5 iliyopita ni cha hali ya juu sana. Kwa tunayokutana nayo hivi sasa ni majuto na kweli majuto ni mjukuu, tunalia na mjukuu wa majuto.
Umepita katika kipindi ambacho hatujawahi kuona watu watu wakitekwa na kupotezwa kabisa, kipindi ambacho hatujawahi kuona mtu anatandikwa risasi hadharani mchana kweupe, yaani kipindi ambacho kwa mfumo wa vyama vingi chama tawala tunachukua ushindi kwa nguvu hata mahali tusikokubalika, kipindi ambacho chama tawala tunapitisha watu kupita bila kupingwa nchi nzima kwa mara ya kwanza, kipindi ambacho viongozi wa chama wanataka hadharani watu flani wanapaswa kuuawa kwa tofauti tu za kisiasa,kipindi ambacho mkuu wa wilaya au mkoa anaingia kwenye ofisi za watu usiku na kupora mali za watu kibabe. Haya yote nyuma hayakuwepo.

Kwakweli mzee aliiweka nchi mahali pabaya sana. Ni sawa alikua mkali kwenye rasilimali za nchi lakini siyo angetupeleka tulikofika hivi sasa, ninagundua utu wa binadamu ni muhimu kuliko hata barabara au daraja tunalojengewa. Mzee alipaswa kuwa waziri mkuu lakini pawepo na mtu wa kumpa maelekezo na siyo yeye kujiamulia mambo.

Tumelipuuza janga la ugonjwa wa Corona lakini Mola ndio anajua liliondoka na nani hata kama nami nimepoteza ndugu kadhaa kwa uthibitisho wa madaktari. Pamoja na umri wangu pia kujitupa mkono lakini kweli siwezi kuiweka kando na hata vijana wangu na wajukuu nimewasimulia ili kesho wajue wataishije kwa kuushinda unafki,fitina pamoja na tamaa.

Nimalize kwa kusema kwamba CCM tujifunze kwa yaliyopita, kama ni Urais tutazame tutazame matendo ya vijana wetu waliopo katika nafasi mbalubali za serikali na chama. Wapo viongozi wa chama, mawaziri, Wakuu wa wilaya na mikoa, wakurugenzi, mbalizi nk. Kwenye makundi haya hatutakosa wagombea makini. Tusiangalie utendaji tu bali tutazame na utu na kiongozi wa kuliungamisha badala ya kuligawa taifa.

Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko!
Binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja!
Umejiskia tu kupata likes ukaamua uandike huu utumbo ukijua humu ni kwa anti-magu. Kwanza ulichoandika ni marudio yaleyale ya mengi ambayo wenzako weeengi wameshandika usiku na mchana toka si tu Magu akiwa madarakani bali zaidi alipofariki. Go on get your likes.
 
Back
Top Bottom