Kuna mapito ambayo yaliipoteza nguvu Chadema na kuifarakanisha na Umma usio wa Kihayawani

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,321
11,410
Huwezi amini.lakini ndo ukweli kuwa kuna wakati Chadema walikuwa wanamwona Nape Nnauye ni Shujaa wao. Ni jasiri wao. Huwa naumia sana ninapokumbuka kipindi hicho. Nilikuwa nawaza yaani Chadema kweli walikengeuka kiasi kikubwa namna hiyo?

Nikawa nawakumbusha kuwa Nape hajawahi kuwa shujaa. Nape ni mchumia tumbo na mnafiq aliyekubuhu. Wakanitukana sana na kusema Nape ni Shujaa na ana msimamo. Huyu huyu wa Bao la Mkono.

Sasa wanapata kigugumizi Nape anaposema kwa sasa bundle inauzwa kwa bei ya chini kuliko wakati mwingine wote. Hapo ngoja Ncheke kwanza. 🤣 HUWEZI AMINI.

Kuna wakati Chadema walikuwa wanampigia Debe Makamba kuwa anafaa kuwa Rais. Na alionekana Shujaa. Nikawa nawauliza huyu Makamba kaanza lini kuwa Shujaa na Smart? Mbona sikuwahi kuna smartness yake? Nlitukanwa sana na kuitwa Sukuma Gang.

Nikashukuru tu sababu hayo majina hayakuwahi kuniathiri. Yalinifunza zaidi kufahamu CDM imevamiwa na watu wa namna gani. Leo hii Makamba anazunguka kugawa mitungi ya gesi vijijini huku gesi ikiwa imepanda. Hatumii akili kufikiria kuwa watu wataacha kutumia kuni na mkaa ikiwa bei ya gesi itakuwa rafiki.

Hafikirii kuwa watu hawashindwi kununua gesi sababu wanakosa mitungi. Ila ni sababu gharama za kununua gesi ni kubwa sana. So leo atawapa mitungi na gesi itakapoisha watarudi kuendelea kutumia mkaa na kuni sababu hawatakuwa na pesa tena ya kununulia Gesi.

Chadema hawa hawa hawajielewi wanataka nini na hawataki nini. Kweli yao ya jana si ya leo. Na kweli ya leo si ya kesho. Nliwaambia CCM wanapogombana nyie chukieni Jembe mkalime. Wao wakajikuta CCM wanapogombana wanakaa kitako kuchagua upande. Wanasahau CCM wengi ni watu wa Maslahi wanagombania Maslahi na si Uzalendo.

Leo hii chama hakina nguvu. Kimebaki na watukanaji wengi kuliko wajengaji hoja. Kimesinzia hakijui kinataka nini. Wengi wamekuwa watukanaji Nguli kwenye mitandao. Wamekuwa wapambe. Hawa wa Anaupiga Mwingi.... Hawa wa Sukuma Gang. Hawa wa Mwendazake.

Wameachana na hoja za Msingi. Kwa sasa hata Katiba Mpya huisikii ...Mbowe nadhani yupo Likizo/Mapumzikoni. Hana hoja tena. Ni kusubiria matukio ndo wayasimamie. Ila wao kama wao hawana Mada tena.

Karibuni kuja kutoa povu. NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO.
 
Acha wakae tu kimya na wenyewe ni binadamu wamepiga kelele sana, watanzania wakaishia kuwadharau na kuwaona kama wendawazimu au waliokosa cha kufanya!!

Kwa sababu walichokuwa wanapigania ni kwa ajili ya wote lakini wakaonekana wehu, sasa acha watawala wafanye watakacho mpaka akili ziwakae sawa!!

Siku mkiambiwa bungeni kunahitajika kuwa na wapinzani wengi sana ili sheria za hovyo za kumgandamiza mwananchi zisipitishwe kirahisi muelewe wanaamanisha nini!!

Wakipiga kelele tunahitaji katiba mpya kwa ajili kuweza kuweka dira mpya ya nchi yetu muelewe wanamaanisha nni!!

Watawala kamatieni hapo hapo,, ongezeni kodi zaidi, wakihoji waambieni waende Somalia kabisa,, hamna namna!!
 
CDM wamepitia kipindi ambacho kimeonyesha rangi yao halisi, CDM ni wajasiria-siasa ambao wapo tayari kutafuta madaraka kwa njia yoyote haramu. Nia ni madaraka na sio kuibadili Tz kwenda mbele, wapo tayari kushirikiana na shetani yoyote kujaribu kutimizi lengo lao, kwa sasa hawana dila, maono wala misimamo wanayoisimamia.
 
Acha wakae tu kimya na wenyewe ni binadamu wamepiga kelele sana, watanzania wakaishia kuwadharau na kuwaona kama wendawazimu au waliokosa cha kufanya!!

Kwa sababu walichokuwa wanapigania ni kwa ajili ya wote lakini wakaonekana wehu, sasa acha watawala wafanye watakacho mpaka akili ziwakae sawa!!

Siku mkiambiwa bungeni kunahitajika kuwa na wapinzani wengi sana ili sheria za hovyo za kumgandamiza mwananchi zisipitishwe kirahisi muelewe wanaamanisha nini!!

Wakipiga kelele tunahitaji katiba mpya kwa ajili kuweza kuweka dira mpya ya nchi yetu muelewe wanamaanisha nni!!

Watawala kamatieni hapo hapo,, ongezeni kodi zaidi, wakihoji waambieni waende Somalia kabisa,, hamna namna!!
Wewe Chadema wa miaka ipi? Hujatukana kwenye huu uzi. Hujaniita majina yale? Wewe una umri gani? Umenishangaza maana hapo nyuma watu wa aina yako walipotea sana. Wangetukana hapa mpaka basi....🤣
 
Nashauri wakae Kimya hata miezi 24 ili watanzania wajingawajinga hasa wa ccm akili ziwarudi!.
 
Back
Top Bottom