Nitarudi tena Marangu

Samahanini sana akina Mangi sikujua kama inakuwaga siri.Ila ndo hivyo tena nimesha mwaga mchele kwenye kuku wengi.

Samahani bila sale na ndoo ya mbegee!!? Wewe namna gani aisee makosa yanatozwa eti.
 
Bora iseme wewe chasaka wakiongea wengine humu hawakawii kusema mwamba ngoma karibu sana marangu hakukupeleka kinuka mori mkuu.

nakuambia angeenda kinuka mori huyu angeandika kitabu cha historia..au angeenda kwenye mihoteli ya kitalii kama Kilimanjaro Mountain Resort au angempeleka maeneo ya kinapa ajionee mihoteli asingerud huyu...lol
 
Mshiki unaonaje ukinipeleka huko kote....:dance:

nakuambia angeenda kinuka mori huyu angeandika kitabu cha historia..au angeenda kwenye mihoteli ya kitalii kama Kilimanjaro Mountain Resort au angempeleka maeneo ya kinapa ajionee mihoteli asingerud huyu...lol
 
Wasinenepe kichwa kwa masifa. Mbaona wengi waliochangia ni wa hukohuko. Tena mmojawao ana jina la Rauya, wengine naanglia kamusi yakichagga? au kajiunga leo JF?
 
mara nyingine mpeleke kwanza usukumani kabla wewe hujarudi huko marangu, usisahau hilo
 
Kuna Rauya mbili: Rauya ya Marangu na Rauya ya Mamba. Wewe ulikuwa Rauya ipi na yenye maporomoko ya maji kama siyo muongo kama yule waziri wa TANESCO?
kama hujui kitu nyamaza mkuu maana ulichoandika kinakufunga mwenyewe .ina maaana kama alikuwa rauya ya marangu alikwenda marangu mtoni kuona maporomoko ya kinukamori wewe
 
sijuim kwann sion kitufe cha like
BTW karibu tena unywe kiburu, kitalolo, kisusio, kitawa, ng'ande., ngararimo, mtori, machalari, vibere, vikwa, viiye, nyany' et al
cc Arushaone, Asprin Smile, Lily Flower et al
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hiyo ni sembeti nyingine au? mimi ninafahamu sembeti ya kupitia mahali wanaita barabara ya kilema au kwa Anaseli. Marangu mtoni ukielekea kushoto unaenda kilema, si ndio?
wewe unatokea kijiji kipi??

manake nakufananisha na wa kimaroroni vile................
 

Karibu tena jamani,ndo asili yetu siye wachaga kutengeneza nyumbani kwanza,na ndo heshima yetu,hapana chezea mchaga weye.
 

Kweli unamauzauza kama jina lako lilivyo,kule ndo nyumbani,elewa ivyo,kwingine tunapita tu tukitafuta maisha,ila tunarudi paleee kijijini marangu kwenye chimbuko,kwa baba na mama zetu,babu na bibi zetu,kwetu,kwa ndugu zetu (kwenye shina letu) huku mjini ni watafutaji tu.na mwisho wa siku hata tukifa tunarudishwa paaaaaaleeee.put in your mind,tafuta pesa,peleka maendeleo nyumbani,hayo mengine ya ziada mjini.
 
Kisusio, Next time ukifika maeneo ya Marangu Hotel nitafute nikuonjeshe Kiburu, Kitawa, Machalari, Shiro, Ng'ande, Mtori, Ndafu na Ngararimo.

umenikumbusha mbali sana mi ni mpenzi wa hivyo vyakula nimevimiss kweli pasaka itabidi niende, umesahau ndizi za kuchoma kwa maziwa ya mtindi au parachichi
 
Kwa maelezo yako wewe ni Mmarangu, naona umetak upazungumzie kijijini kwenu.

Sishangai sana kwa kuwa Wamarangu na misifa hawajambo.
Siku ingine uwaulize wakuoneshe pia kwa yule mzee aliyekuwa akiwalawiti mabinti zake kule Marangu

Ha ha ha..nimeshakuwa tena Mmarangu.Thanks anyway.
 
Kwa wachaga wezangu wale tuliopo mijini zamani tulieshemika kwa elimu na ndiyo iliyotupa eshima mpaka sasa lakini tukumbuke wakati hule kaka zetu walisomesho na kahawa ambayo sasa akuna lakini kuna wadogo zetu wameshidwa kwnda shule kwasababu kahawa akuna tena kwanini tusifanye arambee ya kusaidiye watoto hawo najuwa kabisa wachaga tuko kila mahali na tu uwezo wakusaidia wadogo zetu ili mkoa wetu uendelea kuwa na heshima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…