GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Wanabodi,
Kwa niliyoyaona kwenye kampeni za siasa mwaka huu hakika kuna mambo lazima kufanya maamuzi magumu na ya hasira ili Taifa lisonge mbele na watawala watuheshimu wananchi ikiwezekana kwa tutakachowafanyia mwaka huu watasimulia na kuandika kitabu cha kukiri udhaifu.
Kura ya Rais, Mbunge na Diwani nitaangalia uwezo wa mtu na uelewa wake wa katiba ya nchi na sheria za nchi na tayari hao watu ninao na nitawapigia kura bila kuangalia vyama vyao vya siasa.
Hata kama mimi nina faidika lakini kuna watu wanaumia hivyo kwa maslahi mapana na imani yangu sitamchagua mtu yeyote ambaye anajiona yupo juu ya wananchi na sheria za Tanzania.
Mimi ni mwana CCM na nipo CCM lakini kwa maslahi ya Taifa sitaangalia neno chama bali nitamtafuta mtu kwenye karatasi ambaye atasimamia katiba ya nchi na kuheshimu raia.
Huu uchaguzi sio rahisi ,Malalamiko ni mengi hivyo imenipasa kufanya maamuzi magumu oktoba 28 mwaka huu.
Mgombea mwenye Kiburi,Dharau ,Asiefuata sheria za nchi na mwenye tuhuma zozote zile sitamchagua.
Jumapili ya leo ndio imepelekea nipige kura ya hasira na ghazabu ili moyo wangu uridhike.
Kura ya hasira itanifanya kuwa huru moyoni na kukidhi furaha ya wale ambao wanalalamika kwenye ngazi za Urais,udiwani na ubunge.
CCM tutashinda kwa kishindo mwaka huu na tutaacha alama ya maendeleo ya watu,amani ,utii wa sheria ,miundombinu kila kona.