Nitapiga kura ya hasira Oktoba 28, 2020 kwa maslahi ya Taifa na sio chama

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Wanabodi,

Kwa niliyoyaona kwenye kampeni za siasa mwaka huu hakika kuna mambo lazima kufanya maamuzi magumu na ya hasira ili Taifa lisonge mbele na watawala watuheshimu wananchi ikiwezekana kwa tutakachowafanyia mwaka huu watasimulia na kuandika kitabu cha kukiri udhaifu.

Kura ya Rais, Mbunge na Diwani nitaangalia uwezo wa mtu na uelewa wake wa katiba ya nchi na sheria za nchi na tayari hao watu ninao na nitawapigia kura bila kuangalia vyama vyao vya siasa.

Hata kama mimi nina faidika lakini kuna watu wanaumia hivyo kwa maslahi mapana na imani yangu sitamchagua mtu yeyote ambaye anajiona yupo juu ya wananchi na sheria za Tanzania.

Mimi ni mwana CCM na nipo CCM lakini kwa maslahi ya Taifa sitaangalia neno chama bali nitamtafuta mtu kwenye karatasi ambaye atasimamia katiba ya nchi na kuheshimu raia.

Huu uchaguzi sio rahisi ,Malalamiko ni mengi hivyo imenipasa kufanya maamuzi magumu oktoba 28 mwaka huu.

Mgombea mwenye Kiburi,Dharau ,Asiefuata sheria za nchi na mwenye tuhuma zozote zile sitamchagua.

Jumapili ya leo ndio imepelekea nipige kura ya hasira na ghazabu ili moyo wangu uridhike.

Kura ya hasira itanifanya kuwa huru moyoni na kukidhi furaha ya wale ambao wanalalamika kwenye ngazi za Urais,udiwani na ubunge.

CCM tutashinda kwa kishindo mwaka huu na tutaacha alama ya maendeleo ya watu,amani ,utii wa sheria ,miundombinu kila kona.
 

Habari wanajukwaa wote wapenda mabadiliko.

Kuna mambo ambayo ningependa kuwajulisha viongozi wa CHADEMA na A.C.T ya kwamba Kuna uhujumu wa UCHAGUZI unaopangwa wa kupitisha kura za wizi.

1: Wanapanga kuweka kura fake katika vituo ambavyo vipo nje ya miji na ambapo hakuna ushindani mkubwa wa upinzani na hasa vijijini sana.

2:Kutotoa fomu ya matokeo kwa mawakala wa vyama vya siasa hapa walengwa hasa Ni UPINZANI. Pia fomu za matokeo zitakazo bandikwa zitatklewa haraka Sana kwamba watu wasipate hata nafasi ya kupiga picha matokeo hayo na hapo Ni vituo ambavyo vipo vijijini sana na Ni kwa vituo vichache vitakavyokuwa vimeteuliwa kufanya uhujumu huo wa haki zawananchi.

3: Katika vituo vilivyopangwa kufanyika wizi Kuna uwezekano mawakala wakasumbiliwa kuingia ndani kwakutokuwa na barua ya utambulisho na SIO FOMU YA KIAPO na hapo ndipo watafanya yao.


Ushauri

A:Kuhakikisha Hadi vituo vya vijijini kunakuwa na watu wanaiufatilia uchaguzi huo kwa UMAKINI

B:Wawepo watu watakafuatilia kila tukio usiku wa kuamkia uchaguzi kwa vituo vyote nchi nzima

C: Watu walinde matokeo yote yatakayobandikwa muda wowote ule au Wana CHADEMA wapinzani waondoke na matokeo yatakayobandikwa haraka sana ikiwa wakala hatapewa fomu ya matokeo.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
1603645623902.png

Hata babu anatambua umuhimu wa Uhuru Haki na Maendeleo.
 
Kwa hiyo ulitaka tukusaidiaje, labda? Kwani machotara wamekwambia upigeje?
 
Kwa hiyo ulitaka tukusaidiaje, labda? Kwani machotara wamekwambia upigeje?
Huo ni ubaguzi kuita watu machotara
Sidhani kama Baba yako angekuwa smart na ana akili angekubali kukuzaa wewe mtu ambaye huna akili

Wenye akili walioa wanawake wenye akili zamani na wasomi na familia zao zilipiga hatua

Wapumbavu walioa yeyote aliye mbele yao

Kuna watu humu wanakuita wewe ustadhati sijui ustadhi nilikuwa sielewi kama wanakufahamu au kuna kitu wanakiona kwako

Hakika haupo sawa ustadhi kabisa kama kweli wewe ni ustadhi naomba unisamehe kosa sio lako kabisa

Nitakuambia siku nyingine
 
Back
Top Bottom