farajakwangu
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 1,942
- 701
Kiwanja hakijapimwa lakini nimeshajenga, nataka kuanza kushughulikia hati kwa kutumia kampuni binafsi. Nataka kujua inachukua muda gani kupata hiyo hati na ni hatua gani inapitia mpaka kukamilika zoezi zima.
Ukijaribu kuwauliza wenyewe (kampuni binafsi) mara nyingi wamekuwa waongo hawasemi ukweli kuhusu muda utakaochukua kupata hiyo hati, wao wanasema lipa kwanza tuanze mchakato baada ya hapo ndipo tutajua itachukua muda gani, kitu ambacho naona hawataki kusema ukweli ila wanataka ukishalipia wanaanza kusema ooh ramani imeenda Dar haijarudi.
Wakuu nawasilisha, kiwanja kipo BUKOBA mjini.