Nitapata wapi darasa la kujifunza kichina?

Ndugu wana JF naombeni mwenye kufahamu mahali ambapo kuna chuo au mwalimu ambae ataniwezesha kuongea vizuri,au kuongea fasaha Lugha ya Wachina,naomba hivyo nikiwa na maana mbili,MOJA....uchumi wao unakuwa kwa kasi sana kias kwamba miaka kumi ijayo yawezekana wakateka soko la kila kitu Dunian,na wao hawapo tayari kujifunza kingereza kwani wanasema siyo Lugha ya kibiashara,MBILI....kila nikutanapo na mchina kwenye Dili mala nyingi nakosa kaz au Dili kwa kutojua au kufahamu Lugha yap,pls mwenye msaada aliepo ndani ya JF naomba msaada juu ya hilo....!!

Hongera kwa kufikiria hilo, Nenda UDSM venue B-109 UDBS

kama wewe ni Udsm student utalipa 120,000, kama sio 300,000
Masomo ni kuanzia saa kumi na nusu hadi saa kumi na mbili na nusu jioni!
Itakuchukua miezi miwili, na baada ya hapo utapata scholarship ya kwenda kusoma china bure, kama tuu ukifaulu mitihani yao!
Starting time ni January, March, June, October, na kama uko interested, unaji rejester mwezi mmoja kabla!

Ahsante
 
Jasmine karibu ila mwenzangu tayari ushajua mpaka kuandika mimi mwenzio sijui lolote kuhusu lugha ya China,hapa ndio mwanzo,sasa tutatumia njia gan kufundishana....??
 
bwana Nyang,
labda tutatumia njia ya "skype" na "zoho". kwa hizo, tunaweza kusema na kuandika pamoja.
 
hodi, bwana Nyang
mimi ni msichana nchi ya uchina. ninajifunza kiswahili. nimejifunza kwa muda wa miezi sita hivi. labda tutaweza kusaidiana kwa kusoma lugha.


Bata sistimu.

Hiyo shawa! (Chinese pron...)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom