Nitapata wapi darasa la kujifunza kichina? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nitapata wapi darasa la kujifunza kichina?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Drake, Mar 25, 2011.

 1. D

  Drake Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Habari wanajamii,
  Natafuta mahali nipate kujifunza kichina, mtu anaye fahamu sehemu hiyo hapa dar anijuze
  drake
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  una bei gani?
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Dah! Hata mimi napenda nijifunze hii lugha. Ukipata utaniambia.
   
 4. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  hahahahahaha unanikumbusha mbali na siasa za kizushi za Tz hii lugha ilikuwa ikitumiwa na Mh Kitike alikuwa mgombea wa ubunge jimbo la Ubongo kwa tiketi ya Cuf 2000 ,baada ya fix kibaooo za kuomba kupewa KULA na kusema alisomea China utamckia akiongea kichina Nihomaa wafuac nao huitikia Nihoo
   
 5. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Tafuta marafiki wa kichina kwenye net watakusaidia japo kdogo mf: (kwadia=haraka) (sheshee=asante) (meyolaa=imeisha) (zai jian=kwaheri) baadhi ya maneno ya kichina
   
 6. D

  Drake Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  niliperuzi kwa haraka gazeti la mtanzania nikaona kitu kama hiki ila sikutilia maanani, sas naitafuta siipati,
  washawasha: hayo maneno uliyotoa yana unganishwaje?

  wana jamii,acheni utani dunia inaenda china, lazima ujianda kama wanauza maua kariakoo!kesho wako reception na marketing dept's kalia sit vizuri
   
 7. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Wasiliana na TANROADs watakuunganisha na makandarasi wa Kichina wanaojenga barabara zetu!
   
 8. B

  Bonge JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 868
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 80
  mikocheni karibia na shule ya east africa kuna shule utaona tangazo kuubwa linalosema "tunafundisha kichina". Ile barabara inayopita kiwanda cha cocacola na kutokea karibu na ofisi za clouds radio.
   
 9. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  kuai yi dian=haraka, xie xie=asante, mei you=hakuna

  Maneno hayo yameandikwa kwa Pinyin na sio chinese characters, pia kumbuka katika kutamka kuna tones mbalimbali na kila tone ina maana yake, kuna tone ya kwanza, ya pili , ya tatu na ya nne. So kwa maoni yangu kama unataka kujifunza ni vyema utafute shule kabisa inayofundisha kichina, kama ukitaka kufanya practice watu humu wapo kibao wanapiga kichina kile cha kufundishwa darasani, nakutakia mafanikio mema.
   
 10. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hii imeniacha hoi. Wabongo kucopy na kupaste wamo
   
 11. culboy

  culboy JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2014
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Jamani natafuta mwalim wa kunifundisha lugha ya kichina au sehem wanayofundisha kichina jijini Arusha. Natanguliza shukurani

  Cogito ergo sum
   
 12. N

  Nyang'omango Senior Member

  #12
  Jul 29, 2014
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF naombeni mwenye kufahamu mahali ambapo kuna chuo au mwalimu ambae ataniwezesha kuongea vizuri,au kuongea fasaha Lugha ya Wachina,naomba hivyo nikiwa na maana mbili,MOJA....uchumi wao unakuwa kwa kasi sana kias kwamba miaka kumi ijayo yawezekana wakateka soko la kila kitu Dunian,na wao hawapo tayari kujifunza kingereza kwani wanasema siyo Lugha ya kibiashara,MBILI....kila nikutanapo na mchina kwenye Dili mala nyingi nakosa kaz au Dili kwa kutojua au kufahamu Lugha yap,pls mwenye msaada aliepo ndani ya JF naomba msaada juu ya hilo....!!
   
 13. Young Warlock

  Young Warlock JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2014
  Joined: Dec 29, 2013
  Messages: 330
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Udom wanafundish kichina.....yu just apply there,tena ujachelewa ndo wakati huu
   
 14. N

  Nyang'omango Senior Member

  #14
  Jul 29, 2014
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nashukuru mkuu Young warlock,mi ni mtumishi wa Shirika moja hapa Dar,uwepo wa Darasa UDOM ni mbali kwangu,natafuta kwa Dar es salaam....
   
 15. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2014
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Udsm ipo. Pia unaweza kujifunza mwenyewe kutumia DVDs za kufundishia lugha mbalimbali za dunia ambazo hubadilika tafsiri kadiri utakavyo. So ya Kichina unaweza kui- sett ikufunze kwa kizungu ama kiswahili.
  Sijajua kama Tz zimefika but unaweza kuagiza toka Dubai.
   
 16. N

  Nyang'omango Senior Member

  #16
  Jul 29, 2014
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Oooh Pouwa asante sana,nitafuatiria hapo UDSM.....ASANTE SANA.. !!
   
 17. okaoni

  okaoni JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2014
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 1,197
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  Tunaulizia sehemu ya kusoma part time bila kuathiri majukumu ya kazi mfano hao wamachinga wa kichina waliojaa mitaani hakuna baadhi yao wenye tuition mitaani ili tukajifunze ? sasa mnatuambia UDOM na UDSM si unaanza ten a utaratibu wa kuaply mara maTCU NA MAMBO KADHA WA KADHA? Tuna hitaji zile za mitaani ili tunifunze kidogo kidogo NYI HAU MA?
   
 18. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2014
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Nenda UDSM ulizia taasisi ya Confucious, wanafundisha Kichina wale...
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2014
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  Umepata demu mchina nini?
  +255 719 011 980
  Piga hio namba utapewa maelekezo ya evening studies hapa hapa dsm posta
   
 20. J

  Jasmine_ Member

  #20
  Jul 31, 2014
  Joined: Jul 23, 2014
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hodi, bwana Nyang
  mimi ni msichana nchi ya uchina. ninajifunza kiswahili. nimejifunza kwa muda wa miezi sita hivi. labda tutaweza kusaidiana kwa kusoma lugha.
   
Loading...