Naongezea kidogo tu juu ya tabia ambazo unaweza kujirekebisha pia
1. Usipende sana kula viini vya mayai, kula ile sehemu nyeupe ya nje ya yai. Ikiwa kuna ulazima wa kula na kiini cha yai basi usile zaidi ya vitatu kwa wiki
2. Jenga tabia ya kunywa maji ya dafu mara kwa mara, yana benefits nyingi unaweza kugoogle
3. Wanasayansi wanasisitiza sana suala la kunywa maji mengi kila siku lakini sio rahisi kufuata sheria hii. Kwa hiyo kuna njia rahisi sana ya kukufanya unywe maji mengi kwa siku, hakikisha unakuwa na chupa ya maji pembeni. Kwa mfano chukua chupa ya maji ya Afya 600ml ijaze maji kisha uwe unajipa zoezi la kunywa maji kidogokidogo hadi yaishe. Rudia kujaza chupa mara mbili tena yaani kwa siku walau jumla iwe chupa tatu za 600ml, utajikuta unakunywa lita 1.8 kila siku. Afya ya ngozi pia itaimarika, maana ubora wa ngozi huanzia ndani na sio nje kama wengi wanavyofikiri na kuishia kujipaka bidhaa za viwandani ili ngozi ing'ae
4. Kula mboga za majani kila siku. Lakini kuwa mwangalifu usile mchicha kila siku maana mchicha unaongeza sana damu, usije ukawa na damu nyingi sana, hivyo changanya-changanya mboga
5. Tunza matunda kwenye friji ili ule muda wowote utakaojisikia lakini kula matunda mengi mchana
6. Kwenye suala la kunywa maji hakikisha unakunywa mengi mchana na usiku kunywa kidogo sana au usinywe kabisa
7. Kula chakula kidogo asubuhi na usiku ila mchana jimwage, shindilia msosi wa maana
8. Tumia mafuta ya zaituni (Olive oil) kupikia na kama ni ghali sana bora utumie ya alizeti
9. Fanya mazoezi kila siku. Tena ungejua, mazoezi ambayo wanasayansi huwa wanashauri ufanye ni rahisi sana na karibia kila mtu huweza kufanya kwa mfano kukimbia, kutembea, kuogelea, kurukaruka na yale ya kujinyoosha. Hata sio magumu kama yale ya kunyanyua vyuma

10. Ogopa sana matumizi makubwa ya nyama nyekundu, badala yake kula nyama nyeupe. Miaka ya 1800s wanasayansi wa Ulaya walisisitiza sana kula nyama nyekundu lakini baada ya kuona madhara yake leo hii wanasisitiza ule mboga za majani na nyama nyeupe. Wamasai hula sana nyama nyekundu na damu, matokeo yake wanakua kwa haraka sana, ni warefu lakini hufa mapema. Majirani zao Wakikuyu, wa Kenya ni vegeterians, wanakula sana mboga za majani kuliko nyama, ni wafupi na huishi maisha marefu sana. Nyama nyekundu kula mara mojamoja mfano nyama ya nguruwe ni hatari sana kiafya kuliko nyama nyingine nyekundu kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, n.k. Kula nyama nyeupe kwa wingi mfano samaki na kuku. Watu wa Mwanza, Bukoba, Musoma, ukanda wa ziwa Nyasa, Mtwara, Lindi, Pwani Tanga, Zanzibar na Kigoma wanaenjoy samaki aisee


11. Kula katika timetable, yaani kama breakfast ni saa moja basi kila siku iwe hivyo. Unapaswa kula katika timetable nzuri uliyojiwekea kila siku. Kama lunch unakula saa saba mchana, basi kila siku saa saba mchana ikifika kula lunch hata kama huna njaa.
Kuna mambo mengi sana, nikipata muda nitakuja kuendeleza maana hii haijaishia hapa.