Promethazine
JF-Expert Member
- Sep 6, 2017
- 262
- 260
Wakuu heshima kwenu.
Miaka ya juzijuzi nilizaa na binti Fulani akiwa bado yupo chuo, muda wa kujifungua ulipofika baada ya mwezi mmoja nilimchukua mtoto kwa kuwa alikua na mitihani (UE), mtoto akiwa na mwezi mmoja, yes mwezi mmoja! Kwa ushirikiano wa sister angu ambaye alijitolea kulea mtoto yule akiwa anafanya biashara zake.
Basi nimekuwa natoa fedha za matumizi bill ya maziwa na mahitaji mengine( akina mama wanayafahamu vizuri zaidi.
Sasa binti juzi nilimuambia kuwa nampa jina mtoto litakalokuwa official atatumia mpaka shule maana jina analotumia mpaka sasa alipewa na babu yake upande wa mama, alichonijibu ni kuwa kakaribia kumaliza chuo aje amchukue mwanae, kuwa kama nataka kumpa jina nitafute mtoto mwingine, yaani hapo hasira yangu iliwaka juu yake ina maana huyu binti ananichukuliaje? Maneno anayonitamkia ni ya dharau sana, kwamba mimi akili zangu ni mbili!!
Wakina mama wanajua kazi ya kulea ilivyo ngumu, Mimi pia nimeingia gharama za kulea mpaka sasa mtoto ana mwaka na nusu.
Sikubali kuchekwa ujinga nitakachomfanyia huyu binti hatoamini maana nilikwishasikia anashirikiana na mama yake watamtorosha mtoto binti atakapomaliza chuo and once he is gone is forever!!! (kwenye hili Nina ushahidi, alishanitamkia kuwa siku nikiruhusu mtoto akaenda kwa mama yake alipoolewa sitampata tena),
Nitakachofanya hataamini nitamhamisha mtoto aende mbali sana, najua atakosa malezi ya mama kuliko kuwa na mama mpuuzi wa hivyo.
Watu wanaachiwa watoto bila msaada wowote wewe unaleta dharau!!!
Sikubali kuchekwa ujinga.