Nitakabidhi nchi kwa CCM: JK

Nitakabidhi nchi kwa CCM: JK

Honey K

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2008
Posts
629
Reaction score
72
Kauli hii imetolewa na JK mjini Kigoma wakati wa sherehe za miaka 36 ya CCM....

"Nitahakikisha nina kabidhi nchi kwa mgombea wa CCM na si vinginevyo"!

KAMA RAIS WA NCHI, SALAAM HIZI MAANA YAKE NINI?!!
 
Kauli hii imetolewa na JK mjini Kigoma wakati wa sherehe za miaka 36 ya CCM...." nitahakikisha nina kabidhi nchi kwa mgombea wa CCM na si vinginevyo"!
KAMA RAIS WA NCHI, SALAAM HIZI MAANA YAKE NINI?!!

Hapo zamani za kale mnamo mwaka 1995 niliamini kua huyu mtanzania ana uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko nchini.

Nililaani sana kitendo cha mwalimu kuliengua jina lake katika kinyang'anyiro cha kuelekea kushika hatamu.

Ni takribani miaka 18 imepita ndipo nimeanza kujua maana ya mwalimu kwa ule mwaka 1995.

Sasa nimeamini hapa duniani tuna chui waliojivika ngozi ya kondoo, pia, majuto ni mjukuu.
 
Hivi bwana swai una ndoto za chadema kushinda urais?? Kuwa mkweli huwezi kutegemea ukoo mmoja usambae nchi nzima na kupewa nchi. Kighoma wameshasema hawachezi tena midundiko ya wapinzani wanataka uongozi si kupewa viroba orijino kurushia watu mawe
 
Duh, lakini kwa kuwa alikuwa kwenye sherehe za CCM, anastahili kuongea hayo. Angeongea kama Rais wa nchi ingekuwa taabu kidogo kumuelewa

Sawa ni mkutano wa ccm ina maana na hii nchi ni ccm mpaka aikabizi kwa ccm akasema anakabizi kwa wananchi wao ndio waamue
 
Hivi bwana swai una ndoto za chadema kushinda urais?? Kuwa mkweli huwezi kutegemea ukoo mmoja usambae nchi nzima na kupewa nchi. Kighoma wameshasema hawachezi tena midundiko ya wapinzani wanataka uongozi si kupewa viroba orijino kurushia watu mawe

Lazima utakuwa umelewa ugoro na kuberi
 
Ubabe wa CCM, hawajakubali system ya vyama vingi.
 
kuna mambo mengi yanafanyika Tz, hayawezekani kwingine ila hapa tuu
 
Hapo amesema kweli kabisa, upinzani bado sana Tanzania. CCM itatawala milele.
 
Kasema ukweli kutoka moyoni mwake kazi kwenu kujipanga. Yeye na wenzake wanajipanga kuhakikisha CCM inakabidhiwa nchi 2015... na keshawaambia sasa sijui tufanye nini isiwe hivyo...
 
Kama kauli JK ameishatoa nyingi sana, hizi ni baadhi tu,,,,

''Wanafunzi wanapata mimba kwa ajili ya kiherehere chao''

''Nitaleta maisha bora kwa kila mtanzania''

''Tatizo la maji Daresalaam litakuwa historia''

''Ukitaka KULA lazime ULIWE kidogo''

Na nyingine nyingi, but all in all ukifuata kauli za FASTJET unaweza kuumiza kichwa chako maana huwa anaongea huku hajui anamaanisha nini.
 
itakuwa vigumu sana Serikali ya CCM kukabidhi dola kwa chama Pinzani -- hilo tunalijua na ndiyo maana Rais kasema atahakikisha anakabidhi kijiti kwa CCM 2015.

Hii kauli si ya kubeza, kwa hivyo vyama vya upinzani, sisi wananchi tulijue hili kwamba whatever we do, 2015 bado CCM itakuwa madarakani njoo mvua njoo jua.

Anaweza kuikabidhi nchi CCM, lakini je kama sisi wananchi hatutakuwa tumeichagua itakuwaje? nahisi kuna mambo makubwa yatatokea 2015, na dalili za mambo hayo zimeanza tayari kwenye bunge letu tukufu. Badala ya wabunge kupingana kwa hoja sasa wanapingana kwa matusi na kejeli.

Mungu ibariki - Tanzania tuvuke salama 2015.
 
Na wawe tayari kuaanda mahali a kutuzikia maana watatuua wengi hatutakubali na wawe tayri kwenda the heague
 
Anayajua matokeo huyo wanajipanga kuchakachua hao tunaanza kula miziz kisha tuuangushe mbuyu. tutainguiza wabunge nusu ya wabunge bungeni tutakua na raisi kivuli ambae hatakua na maamuzi hili kasheshe la siku hizi litazidi
 
Hapo zamani za kale mnamo mwaka 1995 niliamini kua huyu mtanzania ana uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko nchini.

Nililaani sana kitendo cha mwalimu kuliengua jina lake katika kinyang'anyiro cha kuelekea kushika hatamu.

Ni takribani miaka 18 imepita ndipo nimeanza kujua maana ya mwalimu kwa ule mwaka 1995.

Sasa nimeamini hapa duniani tuna chui waliojivika ngozi ya kondoo, pia, majuto ni mjukuu.


Pole Mkuu. Mie nilikuwa tofauti kidogo na ww. Nilimwona kabisa JK ni chui ktk ngozi ya kondoo tangu mwanzo. swali la msingi nililojiuliza ni kuwa huyu jamaa anaonekana opportunity sana na mtafuta sympathy ya watu. mtu wa aina hii ni hatari sana. nikajiuliza pia huyu jamaa amewahi ku-achieve nini ambacho anaweza kuionesha nchi hii? kwa uelewa wangu mdogo sana sikuona chochote. sikuwa namfahamu personally kwa hiyo sikuwa na nafasi ya kupata majibu mengi. Namshukuru sana Mungu wangu sikuwahi kumpa kura yangu asilani....nimebaki namachungu tu kuwa kama wengi wetu tungeweza kumwona kama nilivyomwona mie siku zile, hili janga kwa taifa hili tungeliepuka.

Ingawa hivyo haikuchukua zaidi ya miaka 5 watanzania wakawa wameshajua walichemka kumchagua JK. Uchaguzi uliopita wakaonesha nia zao za kutomtaka. lakn kwa vile sasa JK alishashikilia vyombo vya dola na udhaifu wa Katiba yetu, akafanikiwa kubaki madarakani kwa ubavu na ubabe. Basi tujitahidi sasa tuhakikishe Katiba ijayo inaondoa mianya inayotumiwa na watu kama yeye ili matakwa ya wananchi kwa aina ya viongozi wawatakao yatawale na sio uchakachuzi wa aina yoyote. Asalam aleykum!
 
Back
Top Bottom