Nitajuaje gari inachemsha?

Nimekuelewa mkuu. Ukikuta maji yameshuka na huyaoni jaribu kuingiza kidole chako kirefu kuliko vyote na ukiyagusa usiongeze, tembea hivyo hivyo siku nzima kesho yake pima tena kwa kidole usipoyagusa jua iko shida kwenye gasket au pipe ikiwa hamna leakage yeyote uloipata.
 
Basi kuna Shida Mkuu.
Maana siyafikii Maji yalipo. Na shida inaweza kutatulika vipi Mtaalam?
 
Nakazia hapo kwenye point namba 2..
Akiona bubbles wakati amefungua mfuniko wa radiator, kuna mawili.
1...head gasket imeungua au
2...Wakati wa kujaza maji/coolant kwenye radiator, mjazaji hakujaza kitaalamu hivyo akaruhusu hewa kuwepo ndani ha mfumo wa upoozaji...hii hutokea kama radiator inajazwa upya..

hali hii ya kuwepo kwa hewa kwenye mfumo wa upoozaji, pia hisababisha bubbles ambazo mafundi ambao si wataalamu, huwaambia wateja head gasket imekufa na kuwataka wanunue mpya...

Kuna watu watu wengi wameshawahi kukumbwa na hii kadhia ya kubadilisha head gasket,kumbe mafundi wao ndiyo hawajui..

Pia kuna njia ya kienyeji ya kupima na kundua kama kuna cylinder ambayo inapoteza comprehension kuelekea kwenye cooling system
 
Nakubaliana na wewe japo bubbles za hewa upandaji wake huwa tofauti ni zile zinazoashiria gasket head kuungua.. Very similar but not the same.
 
Linachemsha hilo wahi kwa fundi!
 
mkuu hii haina madhara kwenye feni? kuna mtu niliwahi msikia akisema kuna vibrush kwenye mota ya feni huwa vinawahi kusagika mapema kama itakuwa inafanya kazi mara tu uwakapo switch on sasa sijui hii kama ni kweli au uongo
 
Unachotakiwa kujua ni je head gasket ina leakage au la..kitu cha kwanza ni kuweka hayo maji au coolant halafu haufungi mfuniko wa radiator halafu unawasha gari wakati mfuniko upo wazi unachezea throttle ile kwa ku rev ukiona maji yanatoa mapovu na yanapanda juu kwenye radiator jua chuma kinachemsha
 
Ahsante kwa Elimu.
Ila tafadhali ufafanuzi zaidi, inatakiwa yasionekane Maji kabisa, maana huwa maji siyoni kwa macho ya kawaida?

Concern yangu nyingine ni kuwa je Maji napaswa kuyaona pale juu au hata nisipoyaona kwa Macho ni sawa? Naomba msaada Maelezo ya Kina maana napata Knowledge hapa Mkuu!
 
Una watu wanakutegemea?

Maana ni kama umejichoka hivi.

Hivi unaendeshaje gari na kwenda kufungua mfuniko wa Radiator?

Kuchemsha kwa gari unaangalia kwenye dashboard na siyo huko kwenye engine.
Anataka apake karolite
 
Maji yanatakiwa yaonekane kimtindo maana unapokua una rev maji yanakua yanazunguka kwenye vile vinjia vyake kwaionwalau unatakiwa uyaone yakiwa yanapita kama ukiweka maji ila haujayoni kuna possibility kubwa ya leakage kwenye cooling system mimi niliwahi kutumia gari nikiweka coolant asubuhi nikienda mizunguko maji yanapungua nikajakufanya uchunguzi nikakuta kwenye oil cooler kuna kutu na hio kutu inasababisha hewa kupita na maji yanatoka kwaio kukiwa na joto yanapotea unatumia gari yenye engine gani mkuu?
 
Ni IST CC1500 Mkuu.
 
gari yako aina gani mzee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…