Nitaishitaki CCM Mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nitaishitaki CCM Mahakamani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Thanda, Apr 21, 2012.

 1. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nitaishitaki CCM Mahakamani, Bado najadiliana na wakili wangu kuhusu hilo.

  Nia ninayo, Uwezo ninao, na Sababu ninazo.

  Baadhi ya mashitaka yatakayoainishwa ni:

  Kupigwa kibao nikiwa mtoto mdogo (1985) na kada wa CCM, pale nilipouliza swali la msingi baada ya kuiona karatasi ya kupigia kura hasa ukizingatia wakati ule hakukuwa na haja ya kujiandikisha kupiga kura, unaenda tu kituoni unachukua karatasi na kuijaza. Msingi wa swali langu ni hoja, nilimuuliza msimamizi wa kituo " hivi hakuna mgombea mwingine hapa ili tumchague?"

  Ile karatasi ilikuwa nyembamba na ndefu kidogo, halafu ilikuwa na sehemu mbili za picha, upande wa kulia ilikuwa picha ya baba aliyejaa mashavu, mwenye tabasamu na mvi moja moja kwa mbali,na chini yake kuna alama ya V au ndio. Upande wa kushoto kulikuwa na sehemu ya picha yenye kivuli (giza) na chini yake alama ya X. Hapo ndipo nikauliza swali langu la msingi na kupigwa, sasa basi kwanini nipigwe badala ya kujibiwa na kama ilivyo kawaida kwa watoto kuuliza maswali hata 200 ikibidi.

  Pili niliona watoto wakipiga kura kwa maelekezo kwamba"njoo jaza hapa"ulikuwa ni utani wa kweli.

  Sababu nyingine ni kubakwa : Uhuru wangu ulibakwa mwaka 1987, pale nilipolazimishwa kuimba nyimbo zenye hamasa ya chama cha mapinduzi bila idhini yangu. Shuleni mimi nilikuwa mtafsiri wa lugha ya kiingereza kwa wenzangu, M/kiti wa kamati ya "maadili lugha " ila kila siku asubuhi niliamriwa kuimbisha wenzangu nyimbo za CCM" Chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi", Aaaah TANU na CCM vyajenga nchi, na nyinginezo nyingi, nilipokataa nilipewa adhabu mbaya sana, Kwanza mwalimu mkuu, (Mwl Daudi Minja soma hii)aliniingiza ofisini kwake, akanivua nguo zote, akanichapa viboko ambavyo havina idadi....

  Kulazimishwa kutoa Sh 5, kama mchango wa mafuta ya mwenge hata kama hakukuwa na mwenge, mwalimu wa uhamasishaji alikuwa kada wa CCM (Bibiana Tarimo)..jamani wote hawa wapo tena bado ni waalimu na wanaendelea kufundisha (Naomba nisizitaje shule wanazofundisha,na waliopandishwa vyeo kuwa waratibu wa elimu hadi nitakapo wasiliana na mwanasheria wangu).

  Jina langu kupewa mtu mwingine na akasoma kwa jina langu katika shule moja kule Arusha huku mimi nikisoma shule ya bei mbaya kwa kujishughulisha na kuombaomba mitaani hadi kufikia hatua ya kusaidiwa na kanisa (Naomba nisiitaje kwa sasa kutokana na taratibu za kesi kutokamilika) kwa kutumia majina yangu matatu..huyu niliwahi kutana naye nikamuuliza na kumdadisi akanieleza ukweli wote...huyu ni key person kwani atakuwa mmoja kati ya mashahidi. Baba yake ni kada wa CCM, hivyo naamini atatupa ushirikiano wa kutosha. Yote haya yalifanyika kwa kauli mbiu ya kuwaandaa vijana wa kakamavu wa CCM....tupewa mifano mingi ya jinsi Lord Powel, mwanzilishi wa Scout huko Uingereza!

  Hayo ni baadhi ya yale yatakayoainishwa na kujumuishwa katika hati ya mashitaka.

  Naomba mwongozo!!!
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kulikuwa na mpiga picha kwamba alichukua picha ya ushahidi unawajua tena CCM walivyowabishi na wazushi,lakini nakuasa endelea na uamuzi wako washitaki japo jamii ijue uzandiki wao ulivyo hata kunyanyasa watoto
   
 3. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,025
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Hii kali qeli. Baada ya mashauriano na wakili wako plz tujuze ili tuweze kukushauri ipasavyo
   
 4. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kweli nitaishitaki na ninaamini hii mtaiona live

  Kuna kesi moja ya kuvutia sana, na hii niliifuatilia kwa karibu sana...nitawakumbusha wanajamii.

  Mwaka 2009 mwishoni Kulikuwa na vichwa vingi vya habari katika magazeti duniani kwa style ya "Stop Press", vyombo mbalimbali vya habari, hata CNN wakaibuka na "Breaking News" kuhusu Mungu kuitwa mahakamani. Ngoja Niwakumbushe, kesi hii ilifunguliwa Mwaka 2007

  Senator wa Jimbo la Nebraska kwa tiketi ya Chama cha Republican, tena mtu mweusi, Dr. Ernie Chambers, alimshitaki Mungu Mahakamani na kumtaka Jaji Marlon Polk aliyekuwa anasikiliza kesi yake atumie mamlaka aliyonayo kama ilivyo katiba ya jimbo kumuita MUNGU mahakamani hapo mara moja ili aje ajibu tuhuma zinazomkabili.

  Katika hati ya mashitaka, moja ya madai ya Senetor huyu ni kwamba anamtaka MUNGU atoe tamko la kusitishwa mara moja SITISHO LA VIFO, UHARIBIFU NA UGAIDI ambavyo yeye (MUNGU) ndio chanzo cha matatizo hayo.

  Akaenda mbali zaidi kwa kutumia haki yake kikatiba kumtaka Jaji amwandikie MUNGU "summons" ili aje kusikiliza kesi yake yeye mwenyewe, kwani hata mahakama inajua kuwa MUNGU yupo. Chambers katika kuwasilisha akadai" Mahakama inajua kuwa Huyu Mungu yupo, na yote ayafanyayo kiasi cha kujua uwezo wake wa kujua yote, na kwa kuwa Mungu anajua kila kitu,basi ni wazi kuwa atakuwa anajua kwamba kuna shitaka hili mahakamani linalomkabili.

  Shauri la msingi katika kesi hii ni kwamba MUNGU alikuwa amesababisha vifo vingi na uharibifu mkubwa na ugaidi kwa mamilioni ya wakaazi wa dunia.

  Kesi hiyo iliyovuta umati duniani Jaji Polk aliitupilia mbali na kutoa ushauri wa kisheria kwa Hon Senator, kuwa kesi hiyo hawezi kuifungua upya bali anaweza kukata rufaa.

  Sababu za kesi hiyo kutupiliwa mbali hizi hapa, na kwa kweli CCM hawataweza kutoa sababu kama hizi katika kesi ya msingi nitakayoifungua.

  1. Ni kweli Mungu anajua yote,ana nguvu zote na ana ufahamu wa kila tukio hata ambalo halijwahi tokea, Kwa kuwa mahakama hii tukufu imegundua kuwa hakuna uwezekano wowote wa samansi "summons" au tamko la wito kumfikia mshitakiwa, na kwa kuwa moja ya sheria iliyo katika katiba ya jimbo inamtaka mlalamikaji awe na anuani ya mshitakiwa jambo ambalo mlalamikaji hana,kesi hii haiwezi kuendelea..hivyo (akataja vifungu vya sheria, next week nitaviambatanisha Mungu huyohuyo akinijalia)naitupilia mbali kesi hii...alisema Jaji M.Polk.

  Chamber's akitafakari kwa kina ,usikivu na upole kiasi, alinyanyuka na kumwambia jaji natafakari juu ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hii.

  Nachukua uamuzi huu mgumu kwa kuwa anwani ya mshitakiwa haipatikani na hivyo hawezi kupelekewa samansi ya kuitwa shaurini ,"aliongeza Mh.Jaji"

  Katika "Breaking News" katika vyombo mbalimbali vya habari zilisomeka hivi"HUKUMU YA MUNGU LEO, MUNGU KUFUNGWA, MUNGU ,GAIDI NAMBA 1, .....ETC

  BAADA YA KESI KWISHA VIKASOMEKA "MUNGU CHUPUCHUPU, MUNGU ATOWEKA,KUNA MWENYE ANWANI YA MUNGU,AJUAE MUNGU ALIPO ZAWADI NONO KUTOLEWA, MTAFUTENI MUNGU ....ETC

  MWISHO SENATOR HUYO WA NEBRASKA, KIJANA MACHACHARI ALINUKULIWA NA VYOMBO VYA HABARI AKISEMA ALIFUNGUA SHITAKA HILO ILI KUTOA UJUMBE KUWA MTU YEYOTE YULE ANAO UWEZO WA YEYOTE YULE BILA KUJALI CHEO CHAKE, UWEZO WAKE NIA YAKE HATA KAMA NI MUNGU.

  Angalizo: Kama Mungu alishitakiwa ili kufikisha ujumbe kwa WANAJAMII HUSIKA kwa nini isiwe mimi kuishitaki CCM?.(source: Mwanahalisi, Dec 2, 2009)

  Mungu hana anwani, sawa, Vipi kuhusu CCM, Wako kila mahali anwani ninayo hivyo sidhani kama mahakama itakuwa na uwezo wa kuitupilia mbali kesi yangu kwa NIA IPO, SABABU ZIPO, NA UWEZO UPO....NALIA NAO.

  Naomba kuwasilisha hoja.....mimi binafsi.

   
 5. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa tarehe Jumanne ya tarehe 1, mwezi wa 12, 2009
   
 6. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wana JF, mu hali gani?..Kama nilivyowaahidi kuwa "nitaishitaki ccm mahakamani", kuna mwanajamii mmoja alinipigia simu na kuniambia eti kati ya mawakili nitakaowaweka katika kesi hii, nisimuache KIMOMOGORO yule aliyemwakilisha Godbless Lema katika kesi yake kule Arusha mjini kwani yeye alifuatilia hiyo kesi hadi mwisho.

  Anashauri kuwa ni mzuri sana isipokuwa "ILE HUKUMU ILIPIKWA"

  Nina uwezo wa kuweka mawakili hata watatu ikibidi, ila kwa kuwa nawaheshimu wanajamii wote, hapa NO WAY OUT, lazima niwaombe ushauri.

  Asateni kwa ushauri wenu.
   
 7. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wana JF, mu hali gani?..Kama nilivyowaahidi kuwa "nitaishitaki ccm mahakamani", kuna mwanajamii mmoja alinipigia simu na kuniambia eti kati ya mawakili nitakaowaweka katika kesi hii, nisimuache KIMOMOGORO yule aliyemwakilisha Godbless Lema katika kesi yake kule Arusha mjini kwani yeye alifuatilia hiyo kesi hadi mwisho.

  Anashauri kuwa ni mzuri sana isipokuwa "ILE HUKUMU ILIPIKWA"

  Nina uwezo wa kuweka mawakili hata watatu ikibidi, ila kwa kuwa nawaheshimu wanajamii wote, hapa NO WAY OUT, lazima niwaombe ushauri.

  Asateni kwa ushauri wenu.
   
Loading...