Nitahamia Zambia na Sio Burundi

Kiongozi wa watu vs Mapaka👇
Si mapaka, haya ni manyang'au wa kutupwa yanayokula bila kunawa.

Masikini wadanganyika tumetulia tuli kama kondoo wanaopelekwa machinjoni huku Taasisi zetu nyingi zikiongozwa na vijana waliozaliwa na kukulia ndani ya CCM!

Vijana hawa, wengi wamefuzu katika wizi na udokozi toka utotoni...ama waliiba majina, waliiba mitihani, waliiba vyeti au yawezekana wengine walitumika katika wizi wa kura!

Halafu wanapewa ulinzi wa ghala zetu na hazina zetu, hatuponi hata kwa dawa!
 
Kama state haioni umuhimu wa hii kitu basi inatusaliti sana watanzania
The state imeamua KUTUMIA njia ndefu zaidi ku tu provoke raia ili tumkatae kiongozi na WAO wamweke wanaemtaka !!

Tutaumia KWA muda Hadi December matokeo ya Tozo tutaanza kuyaona meno ya state!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa iwe Katiba Mpya"
 
Angekua na "uelewa" japo Mdogo angeshauri tuhamie Zambia na sio Burundi. Zambia Raisi ni Mtumishi wa Wananchi, ni mnyenyekevu, amezuia matumizi ya magari ya kifahari kwa Mawaziri (Wakati yeye ana latest Toyota v8), Rais wa Zambia amegoma Katu kupongezwa na kuwakumbusha Watu wake kuwa anayoyafanya ni Wajibu wake na sio fadhila kama Mwigulu na Wenzie akina Nape wanavyotuaminisha.

Leo hii nchi nzima imejaa mabango ya kumsifia na kumpongeza Mtu mmoja, as if halipwi, as if ni msamaria mwema tu, tumejengwa kuaminishwa hivyo na wapuuzi Wachache wanaamini hivyo.

Mimi nitaenda Zambia ambako Pesa ya nchi Yao inazidi kuwa stable dhidi ya US Dollar, nchi ambayo Kuna kuaminiana na Rais hahitaji ulinzi wa mabilioni kujilinda......
Mungu ibariki Zambia
 
The state imeamua KUTUMIA njia ndefu zaidi ku tu provoke raia ili tumkatae kiongozi na WAO wamweke wanaemtaka !!

Tutaumia KWA muda Hadi December matokeo ya Tozo tutaanza kuyaona meno ya state!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa iwe Katiba Mpya"
Bora tukamuliwe kodi hadi akili zikae sawa.
 
Watanzania wengi hawana exposure wala hawana utaratibu wa kujisomea taarifa mbalimbali kuweza kujua uhalisia wa mambo. Kutishia kuhama Tanzania ni kelele tu zisizo na kichwa wala miguu. Zambia ni nchi iliyolemewa na madeni kila upande kiasi kwamba Hichilema alikimbilia IMF & WB ili kuwakwepa wachina ambao walikuwa wanaenda kuifanya nchi koloni lao. Kwa mfanyabiashara makini hawezi kuiacha Tanzania yenye watu 60m akaenda Zambia kwenye watu 20m. Bongo ukiwa smart kidogo tu unapiga hela kwasababu ya uwingi wa watu. Si mnaona Kalynda ghafla tu wamesomba mpunga wa maana.
 
Zambia walipo zingua mpaka barabara ya border ya Tunduma inayo ingiza mapato vumbi tu.

Ukienda zambia wanapenda sana kuja Tanzania yani.
 
Wana hali ngumu sana kimiundo mbinu. Ile barabara kutoka Nakonde hadi Kapiri Mposhi ni mbovu hakuna mfano.
 
Hakuna mkoani Bei inapofika elfu 4 kwenye kituo Cha mafuta..

Bei hizo ni huko Kijijini kusiko na vituo vya mafuta na ndio maana Serikali imetenga pesa za kukopesha watu wa Vijijini Ili waanzishe vituo vya mafuta potable.
Aisee daah upo busy ila unachokiongea unakijua mwenyewe...
 
Zambia maisha sio ghari kama Tanzania wao ukiwa na Tsh 5000 ukaibadili ukapata Kwatcha unanunua umeme unapata unit zisizopungua 98 na kipindi cha corona walikua wanatoa Bonus,Magari kodi zake ni favourable zinalipika hata mizigo pia kasoro Pombe tuu zipo juu ndio maana Mzambia anaweza kuendesha gari yeyote akiwa mfanyakazi ambayo Mtanzania hawezi labda aibe...Wazambia wana utaratibu wa kupenda kununua vitu vipya iwe Electronics mpaka nguo hiyo ni mpaka huko vijijini wakati Watz tupo sana kwenye mafriji ya mitumba na Tv...Bus za Zambia zinazoenda vijijini ni zile body za Iriza i Q 10 wakati Tanzania Wafanyabishara wa bus wapo kwenye chasis za maroli yawe bus...Trafik wa Zambia asumbui raia tofauti na Tanzania trafiki wana vita na watu wao kama paka na panya...Zambia unaweza kuendesha gari muda mrefu swala la trafik utakutana nao kwenye vizuizi hawa wa mjini sio wasumbufu kama wa Tanzania...
 
Umeeleza vizuri. Sema faini zao ukikutwa na kosa sio poa.
 
Wana faini kubwa. Kwacha 450 ukichenji Tsh ni nyingi kwa sasa.
Ok sema kwa magari madogo wanatuvizia tochi tena zipo sehemu mbili au tatu mpaka unafika Nakonde kutokea Lusaka sasa hivi napitia Chipata huko hakuna usumbufu kabisa nakuja kutokea kasumulu bara bara nzuri na magari sio mengi kama Nakonde mpaka kapirimposhi na ajali nyingi..huku Malawi ni Mlima Chiweta tuu
 
Unaingia Chipata then Malawi?
 
Back
Top Bottom