Nitagombea Urais - Kisandu Deogratius

Sifa zake kama anamaanisha kugombea urais wa taasisi ya kidini, manake hizo sifa alizojipamba nazo.!
 

Kaka.. Unaweza kupinda ulimi kumshauri Mtu ukadhani ana weledi lau kiduchu Wa kusikia, Kumbe ukaambulia 00. Embu ona, Kwa Jotoridi la mvumo wa kisiasa Na Ujenzi wa chama unaoendelea Haijuzu Mtu timam akaingiza kitu kipya Kwenye bongo Za watu ilihali pana Movement inayoendelea ya kujenga chama.. Mbona Muda upo tu ambapo secretariat ya chama itapanga kila mwenye dukuduku ataliwasilisha hapo.. Why now talking loudly.. Hii inaitwa Nini ..
 
Kikwete amafanya urais uwe rahisi kila mtu anatamani kwenda kutalii ulaya na kuvutwa na vitoroli kama jk,kweli hata mimi ninaweza kuwa amiri jeshi mkuu kha!

Jamani mbav zetu wengine.. Ha ha haaaa.. Imagine kila kona Kati ya Mtu Tisa mmoja lazima apwayuke kuutaka urais.. Aisee..
 
With all due respect this must be presidential silly season for seeking political credits which may be will help to polish the name up the ladder. Let us wait and see if the mission will hold water tightly after being accomplished. Samahani lakini.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
Mimi nitaendelea kulia na Kamati Kuu CDM mpaka pale watakapotoa mwongozo kuhusu hizi fujo za watu wasiojua kupima upepo.Kamati kuu mnaweza kuwapuuza hawa wanaoleta ujinga chamani lakini niwahakikishie sisi tunaokaa huku chini na wanachama wanakereka kupita maelezo.Kuna mwanachama mmoja aliniambia juzi kwa masikitiko makubwa kwamba.....'CDM sasa wanachukua njia ileile ya CCM ya kugawa chama chao vipandevipande'....Haya ni maneno mazito sana..Tafakarini enyi Kamati Kuu....
 
Nyie "gombeeni", wajanja tutauchukua hata bila "kugombea".

Basi mwenzenu nilikuwa nachangia sred nikidhani iko makini kumbe mweshimiwa kaamua kuweka Comedian JF.. Manake kila comment nayosoma unacheka hadi mbav zinananihii.. Nyie watu acheni kuweka post Za Vituko..
 
Watu wakini wanafikiria kukijenga chama hasa vijijini - usiku na mchana wapo kuhimiza watu kujiunga na CDM, wengine wamekaa tu wakifikiria urais - kweli duniani kuna watu.

Kabla ya kufikiria Urais kwa tiketi ya CDM (Chama ambacho kinakuwa kwa kasi na kinapendwa na wananachi) Jiulize umekisaida nini ili kiingie madarakani 2015?

Urais CDM si hoja ya msingi kwa sasa watu watawashangaa sana wakati watu wanapanda mbegu shambani wewe na mwenzako mnapiga mahesabu ya kulangua mazao. Hoja kwa sasa ni kwa namna gani chama kitawafikia watanzania walioko vijijini hasa ukizingatia Jiografia ya nchi yetu.

Sasa chama kikiwa tayari basi tunakaa na tunamchagua mwakilishi wetu atakaye peperusha bendera ya chama. hatuzuii wanachama kuchukua kutoa maoni yake ila huu si muda muafaka. kwa sasa tunataka mchango wako mwenye M4C.

Watu wanapigwa mabomu huko kwenye harakati za ukombozi wewe na mwenzako mko ofisini mnasubiria urais --shame.
 


You are talking absolutely NONSENSE!
What qualifications do you have? Kawaida kila chama kina utaratibu wa kupata mgombea wake wa urais. Sijui mwenzetu utakuwa umepitishwa na nani kugombea huo Urais mwaka 2015 kupitia CDM.
Yaawezekana kabisa umetumwa na maadui wa CDM ili kujaribu kuleta chokochoko na vurugu ndani ya chama.

Natilia shaka kwamba yamkini wewe inawezekana kabisa ukawa ni mamluki wa CCM. Ngoja tusubiri hatima ya madai yako.
 
Nimtume nani aende?Unitume mimi nitume BWANA.Nitakwena kutangaza neno lako wewe,mataifa yasikie yakufuate wewe.Unitume mimi nitume Bwana.
 
bado rafiki yangu SHIBUDA, yeye hautaki urais?
 
Mkuu Ritz;
Haya mgombea mwingine huyu tuone mwenyekiti Mtei atasemaje

Chama
Gongo la mboto DSM
 
JF nadhani sasa ipange utaratibu wa kutoza gharama za matangazo kama haya, familia ya Nyerere wao tayari wanatoza tozo kuangalia kaburi, natumaini uongozi wa JF hii ni fursa yenu sasa na si watu kutangaza majina yao bure.
 
Aisee umekwenda mbali sana, ni kwanini unampromote sisimizi kama huyo? ana uwezo upi wa kuleta chokochoko ndani ya chama? labda awaletee ***** ***** wasambaa huko Tanga wamtandike tu.
 
Kuna watu vibuyu kweli kweli.
Yani watu wanapanda mazao wewe unafikiria kuyavuna...hata palizi na kupiga dawa hufikirii...
Majanga haya!!
 
Mimi nachukuwa fomu ya kugombea uenyekiti wa CCM Taifa.

Karibu sana ugombee CCM ni chama cha kidemokrasia haiongozwi kwa maamuzi ya baba mkwe; kama una sifa za kutosha njoo kwenye chama huru

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mimi nachukuwa fomu ya kugombea uenyekiti wa CCM Taifa.

Hahahahaha thubutu yake..... Kile ni cheo cha mtu mmoja kwa 10yrs bila kupingwa wala kuleta vyoko vyoko......demokrasia ya CCM hiyo.
 
Bora hapa umejaribu kuongea mwenyewe bila kumuita ritz, nimependa haya maendeleo.

Karibu sana ugombee CCM ni chama cha kidemokrasia haiongozwi kwa maamuzi ya baba mkwe; kama una sifa za kutosha njoo kwenye chama huru

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…