Nitagombea Urais - Kisandu Deogratius

Nitagombea Urais - Kisandu Deogratius

FOR A TIME BEING I DO NOT WANT TO BE APPOINTED AS 2nd Vice President, I HAVE Said I WANT TO BE A President of Tanzania 2020.

My desire to Create New Government which have never seen before, to make Tanzania to be the Leading Nation on Potential Ideas to build strong government.

I got gossip somewhere that there is a plan to be appointed as second Vice President of Tanzania, Since October 2012 I declared my desire to be A President of Tanzania through Mass media and Social Network media. I can not change my God plan by pleasing me to highest position. No No No, my Dream must Occur.

But I say thanks for consideration and God have a bless over those who think so. I, Deogratius Kisandu am a Tanzanian and a Political Analysis apart of being a Teacher at Mkolani secondary school in Mwanza region.

I Feel Shame if Not shy to try to please me after they have blocked my Economic and Detented me Psychologically.

God give me long live and bless Tanzania.

Deogratius N Kisandu
From Tanzania, East Africa.View attachment 490766
Hivi Magufuli ameonyesha uwezo mdogo kiasi hiki mpaka huyu dogo anataka urais?kwa hali hii basi nchi yetu ina tatizo kubwa sana.
 
Hivi humu ndani hakuna wanafunzi wake tuwahoji japo kidogo nina mashaka na ubongo wa huyu teacher
 
Rais mtarajiwa, hebu endelea kutupa sera zako. Tumia tu kiswahili, najua wewe ni mwalimu lakini naona hiyo lugha ya mkoloni unaenda chaka tu.
 
Huyo awe teacher kweli au naye atakuwa alipofoa cheti, na mwenyewe alishakichukua, vinginevyo viroba vilivyitupwa majararani kavibugia
 
Moderator ningeomba mum block huyu mtu asiwe anapost humu JF. Ni mgonjwa anahitaji msaada wa kisaikolojoa. (I bet that)
Mkuu mi sikubaliani na wazo lako leo nilikuwa na stress kichizi uzi wa mshkaji DK umepoza stress maana ni full comedy asipigwe ban aisee,mod pls msimpige ban jamaa anatuburudisha mjue
 
naamini asilimia kubwa tuliofungua huu uzi tumeishia kucheka,huyu bwana avumiliwe tu hakuna namna.haya bwana kisandu tumekusikia
 
Ni kweli wewe ni mwalimu? Kama ni mwalimu je unafundisha masomo gani na ni ya primary school au secondary school?
 
Moderator ningeomba mum block huyu mtu asiwe anapost humu JF. Ni mgonjwa anahitaji msaada wa kisaikolojoa. (I bet that)
I am supporting this request. This guy is a classic psychiatrist patient.
 
Jan 14, 2014
Habarik blog

Huyu ndiye DEO KISANDU aliyefunguka kuhusu CHADEMA.

Naandika makala hii(Mimi Deogratius Kisandu)kwa Uchungu na furaha kubwa.Kuanzia miaka ya 2009-2012 vijana wengi waliokuwa Vyuoni waliijenga sana Chadema ikiwemo kuanzishwa kwa asasi ya CHASO waanzilishi wakiwa ni Deogratius Kisandu na Juliana Shonza na wengineo lakini pia kuliibuka vijana waliokuwa vyuoni na waliomaliza kipindi cha mwaka 2010 na kujitokeza kugombea nafasi za ubunge na udiwani wengine walipata na wengine hawakupata ambao ni Mtela Mwampamba, Deogratius Kisandu, David Silinde, Habib Mchange,Felix Mkosamali,Moses Machali, Chagulani Adam na wengine wengi. Kipindi hiki vijana walijitoa sana kujenga chama tena kwa kutumia nguvu zao mfukoni na ndipo vijana mihemko walipojitokeza wanaoamini kila kitu ni sawa. Lakini tija yao haikuonekana wengine walifukuzwa na wengine waliondoka wenyewe na wengine walibaki. Kiukweli wakati mwingine hutakiwi kulaumu kwa yaliyotokea ila ni kumshukru Mungu kwa kukuonesha njia nyingine ya kufikia malengo yako na kutimiza hata yale ambayo hukufikiria kuyatimiza ili kutimiza wajibu wa kumtumikia Mungu kama kiongozi.

Ikumbukwe kuwa nilikuwa mwenyekiti wa CHASO-Sekomu, Katibu wa Chadema(w)Lushoto, katibu wa BAVICHA(m) Tanga, mjumbe wa kamati tendaji wa BAVICHA. Nimezitumikia nafasi hizo kwa uaminifu na kwa nguvu zangu mwenyewe(akili, fedha na rasilimali nyinginezo zilizokuwa ndani ya uwezo wangu).

Namkumbuka Mbunge wa arusha mjini kaka yangu Godbless Lema alivyokuwa ananipa ujasiri sana hasa kipindi nilipokuwa nimepewa barua ya kujibu mashitaka ya kwanini nimemleta Lema wilayani Lushoto hasa barua hiyo iliibua mambo mengi sana ikiwa na mitego ya kila namna ili nifukuzwe chuo, japo vijana waliokuwa wanasoma sheria chuoni kwetu walinisaidia sana huku lema akinitia ujasiri wakutokuogopa na mwisho wa siku nilishinda Dhuluma na kufanikiwa kuhitimu chuo na hata Mkuu wa Chuo siku ya kupata cheti alinipongeza sana kwa ujasiri wangu na kuniambia angekuwa mwingine angekuwa kishaacha na chuo ila Mungu anampango nawe, timiza wajibu wako.

Makamu mkuu wa chuo mpya aliyeletwa kipindi tunaelekea kuhitimu chuo ndugu Molleli alipopewa taarifa kuhusu mimi mambo yalikuwa hivi; niliandika waraka wa kuwashukukru walimu wangu wote kwa nifundisha na kuwaahidi nitakwenda kufanya siasa safi kama ambavyo walikuwa wakiniasa mara kwa mara, makamu mkuu wa chuo nilipofika ofisini kwake akasoma waraka huo na kuniambia" Umesoma mpaka umehitimu chuo japo kwa vizingiti vingi na kushauri usikubali kufanya siasa za mabavu na siasa za kulaumu bila suluhu utajikuta unapoteza muda wako bure, bali fanya siasa za kubadilisha fikra kwa mlengo wa kidiplomasia na ukifanya hivyo hutaumia bali utaheshimika zaidi......" ni furaha kwangu japo leo hii wapo ambao wanasema nimeishiwa kumbe nimebadilika kimfumo na kisiasa.

Namshukru Mungu kwasasa nipo katika chama cha NCCR-Mageuzi tukifanya yetu kwa pamoja, kipindi kingine nitazungumza wajibu wangu kama mwana NCCR-Mageuzi.
 
wanafunzi wanaofundishwa nahuyu ticha wataongeza idadi ya mabashite nchini...ni bange kwenye kichwa mapepe ama?!?
 
DEO KISANDU HIKI NDICHO KILICHONIPATA NCCR MAGEUZI,SITAKI SIASA TENA

TAMKO LA KUJIVUA UANACHAMA WA CHAMA CHA
NCCR – MAGEUZI 17 Juni 2014.

1 :0 UTANGULIZI
Ndugu wana habari na ndugu Watanzania, kwa kutambua mchango wangu mkubwa ambao nimkuwa nikiufanya katika ujenzi wa vyama vya siasa hasa Upinzani hapa nchini, ni dhahiri nimekuwa mjenzi wa vyama kuliko mafanikio ya wananchi. Nimegundua mengi sana na kujifunza mengi sana juu ya hivyo vyama vyetu vya Siasa, tunapotafuta demokrasia katika nchi yetu sio tu kuwa huru kwa kila jambo bali kuwa na UTU kwa watu tunaowatafutia Demokrasia ya kweli, hatuwezi kusema nchi haina demokrasia kama hatujatenda haki kwa wanachama au wananchi wetu.
SABABU ZA KUJIUDHURU UANACHAMA NA NYADIFA ZOTE ZA UONGOZI.
2 :0 AJALI YA GARI
Mwaka jana June 2013 kulikuwa na uchaguzi mdogo wa Udiwani Wilayani sengerema Kata ya Nyampulukano na mimi nikiwa msimamizi wa Uchaguzi huo mdogo wa
marudio, jumamosi ya kuamkia uchaguzi tulipata ajali ya gari tukitoka kukagua vituo vya kupigia kura na mimi nilikuwa kiti cha mbele cha gari na nikapata maumivu makali sana, japo nilipewa huduma ya kwanza lakini baada ya hapo sikupata matibabu stahiki kitu ambacho mpaka sasa, nisingeweza kulaumu kama hawajui lakini wanajua fika viongozi wenzangu, na ukizingatia wakati ule nilikuwa Katibu wa Mahusiano na Uenezi Taifa kitengo cha Vijana.
Kutokana na hali kuwa si nzuri na kufikia kuona nalalamika ujue kabisa hali si nzuri ki afya, jambo la msingi kwa wenzangu hata kama wanahisi na makosa lakini jambo la Busara ni UTU kwanza wakumponya aliye mgonjwa ndipo busara zingine zinafanyika, kiukweli nasikitika sana na ninaumia sana kwa tukio hili maana ile ilikuwa ni kazi ya chama na siya mtu, ina maana hata Elfu kumi tu nayo ni ngumu ? kweli hapa tujiulize sasa, na ndio maana naumia sana kwa hilo, kwa hili mimi naona kama wamenitelekeza na kuniachia familia yangu mzigo.
Nashauri tu kuwa vijana wenzangu wa Kitanzania tunapo jiunga na vyama vya Siasa tuchunguze UTU kwanza kabla hatujafikia maamuzi na tusiwe washabiki wasiasa bila kujua hatima yetu kimaisha, nashauri kama vijana tuwe tunasapotiana kwenye matatizo maana leo limemkuta Kisandu kesho linakuja kwako. Nimejaribu hatakuomba msaada kwa baadhi ya viongozi rafiki msaada wa aina yoyote bila mafanikio.
USHAURI WANGU kwa chama changu NCCR – Mageuzi naomba kama hili limetokea kwangu basi lisijirudie kwa mwingine kwani hata Mungu hapendi kuona hali kama hizo.
Kutokana na hili la matibabu ndugu na familia yangu wamenishauri niachane na Siasa za vyama ili waweze kuona wananisaidia vipi, kimsingi naungana na ndugu zangu na kukubali ombi lao kuliko kuumia namna hii. Naomba msamaha kwa viongozi wenzangu pale tulipo kwazana na mimi na wasamehe pale walipo nikosea japo nabaki na maumivu ya kiafya.
3 :0 KATIBA MPYA
Kwa upande wa swala la KATIBA MPYA, huu mchakato si wa mtu mmoja au watu kadhaa bali ni mchakato wa Watanzania wote. Swala la Muundo wa Muungano si swala la CCM wala UKAWA bali ni letu sote, hapa ningeshauri tu kuepuka mvutano baina ya serikali mbili au Serikali tatu, wakakaa pamoja na kufikia maridhiano yenye Busara ili tupate Katiba mpya inayoendana na mazingira ya Kitanzania. Pia lazima wawakilishi wetu Bunge la Katiba watambue kuwa maoni ya Serikai mbili ni ya Wananchi na Maoni ya Serikali tatu nayo pia ni ya Wananchi hivyo Busara ndio itumike kurejesha Umoja wetu wenye katiba ya pamoja.
4 :0 KUHUSU BAJETI YA SERIKALI MWAKA HUU
Viongozi wetu watambue kuwa Bajeti hii ni ya Watanzania wote hivyo badala ya kukosoa tunapaswa kuboresha na tusikosoe bila kuiboresha maana kama tutakosoa tu mwisho wa siku tutakuwa hatuja tibu chochote bali serikali ikosolewe kwa kupewa solution.
5:0 UKAWA
Hakuna dhambi mbaya kama dhambi ya ubaguzi, Baba au Mama akibagua baadhi ya watoto tena wadamu ni dhambi kali sana ya ubaguzi inayohitaji kukemewa. Ndugu zangu wanao jiita UKAWA hawa jamaa si wazalendo kabisa wametawaliwa na dhambi ya ubaguzi wa vyama. Vyama vya Siasa vipo 23, vyama 22 vikawa ni vyama vya Upinzani, iweje leo wote ni wapinzani eti UKAWA iwe ya vyama vitatu vya upinzani fikiria kama ni uchaguzi Mkuu, vyama vitatu kugombea uchaguzi haisaidii maana hata robo haijafika. Ubaguzi uliofanywa na hawa jamaa hauvumiliki kabisa na si vitendo bali ni Umoja ndani ya Mtengano. Wakiweza kuungana vyote vyama 22 vikawa UKAWA basi nitakuwa tayari kuendelea na siasa na hata Serikali 3 nitaunga mkono lakini dhambi ya kubaguana ya vyama itaendelea basi ni heri Serikali 2 au 1 maana UKAWA ni ya vyama vitatu na si ya wananchi maana ya UKAWA ya wananchi ni ya vyama vyote 22 vya Upinzani dhambi ya ubaguzi iacheni ni Pepo mchafu.
6:0 FIKRA MBADALA
Vijana wenzangu tuache mihemko na jaziba katika ushabiki wa mambo ya kisiasa na tuhamie katika uzalendo wa kujenga nchi yeye Amani na Uzalendo bila kujali itikadi za vyama vyetu na tusijikite kuchagua vyama bali tuchague viongozi wanaotufaa bila kujali Ushabiki wa vyama.
7:0 MAPUMZIKO
Kwa sasa nimeamua kupumzika siasa na kuangalia mstakabli wa maisha ya kifamilia kwanza, pamoja na kupumzika huko nitapumzika na kwamba nitakuwa naelekea chama gani hilo si swala la leo mpaka pale nitakapooona inafaa na sijui ni lini.
Ndugu wanahabari nifikishieni taarifa hii kwa umma wa Watanzania na Mungu atupe uzima wa maisha marefu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.
MWL. DEOGRATIUS KISANDU
ALIYEKUWA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU
 
Kisandu apewa cheo NCCR

12/1/2013

Na Benedict Kaguo

CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kimemteua Bw. Deogratius Kisandu kuwa Katibu wa Mahusino na Uenezi Kitengo cha Vijana baada ya kujiunga na chama hicho hivi karibuni.


Bw. Kisandu ametokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambako alikuwa Katibu wa Baraza la Vijana
(BAVICHA), mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa barua ya uteuzi iliyoandikwa na Ofisa Tawala
wa NCCR-Mageuzi, Bw. Florian Rutayuga ambayo gazeti hili
inayo nakala yake, alisema uteuzi huo umeanza Januari 8,2013.

“Napenda kukuarifu kwamba, kuanzia kuanzia tarehe ya barua hii,
nimekuteua kuwa Katibu wa Mahusino na Uenezi Kitengo cha Vijana wa NCCR-Mageuzi.

“Uteuzi huu ni kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 39(g), ya toleo la pili lililohaririwa mwaka 2003 la kanuni za kitengo cha vijana NCCR-Mageuzi mwaka 2000,”
ilisema barua hiyo.

Akizungumzia uteuzi huo, Bw. Kisandu alisema nafasi aliyopewa ameipokea kwa furaha kubwa kutokana na chama hicho kutambua uwezo wake kisiasa na Mwenyekiti wa chama hicho Taiga, Bw. James Mbatia, kumpa moyo wa kuitumikia.

“Jukumu nililopewa ni pamoja na kuandaa kauli mbiu inayosema 'Vijana ni Rasilimali ya Taifa', lengo ni kuhakikisha kuanzia sasa, milango iko wazi ili waweze kulitumika Taifa.

“Kazi ya ukombozi wa pili wa Taifa hili iko mikononi mwao na wasikubali kufanya maandamano yenye faida kwa viongozi
badala ya wananchi,” alisema Bw. Kisandu.

Aliyataja majukumu aliyopewa kuwa ni pamoja na kuandaa wagombea ubunge na udiwani 2015 kupitia idara ya vijana nchi nzima, kusimika viongozi katika majimbo yote nchini na kuandaa kikosi kazi cha ushindi kwa vijana kila Wilaya ili kuhakikisha
vijana wanashika hatamu ya uongozi nchi nzima.



January 14, 2013 at 10:18 AMReactions:
Vijana kuweni na msimamo kama mna nia ya dhati ya kuikomboa TZ. Suala la kuhama CDM na kuhamia NCCR halafu kupewa wadhifa on the spot kidogo inaleta wasiwasi. Huenda ndugu huyu alirubuniwa ili ahame chama chake cha awali kwa kupewa ahadi ya kupatiwa cheo. Hata huko NCCR huenda akahama akaenda chama kingine ambacho kitakuwa tayari kumtunuku cheo zaidi. Hizo ni tamaa za kidunia.

Reply
 
English ikigusana na wasukuma hata kwa sauti tu huwa haiandikiki wala kutamkika .

Kabla ya vi-wonder kuna kazi kubwa ya kutenganisha kwanza wasukuma na English then tutaendelea na Vi-wonder j

not to that extend kha?
 
Huyu ndio harmorapa Wa Jf safi sana nawe uwe unatoa pole kwa wahanga
 
Mie siku za awali nilidhani mnamwonea kumwambia kuwa ni chizi lahaulaaa kumbe sasa mpaka mwenyewe kishajijua kuwa hamnazo.
 
Sept 28, 2014

Huyu ni wewe?

19.jpg


Deogratius Kisandu akiwasalimia wananchi wa Lwandai kata ya Mlola wilani Lushoto baada ya kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .Deogratius alishawahi kuwa na nyanzifa zifuatazo kwenye chama cha NCCR Mageuzi,Katibu Mwenezi Taifa kitengo cha Vijana (2013) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya NCCR-Mageuzi (2014

Michuzblog
 
Eti anataka kuwa Rais wa Tanzania, Kwa kiingereza kibovu hicho halafu eti ni Mwalimu wa sec,hii nchi kweli ni matope kabisa, English mbovu hiyo ndo anafundisha nini na halafu ni chizi kabisa huyu.
 
Back
Top Bottom