Nitagombea ubunge jimbo la Serengeti 2015

Nitagombea ubunge jimbo la Serengeti 2015

Joined
Apr 5, 2012
Posts
58
Reaction score
66
Ndg Wanajamii-Forum,

Mimi ni mdau wa masuala mbalimbali ya kimaendeleo na kwa sasa naishi Serengeti. Kwa miaka 6 sasa nimekuwa nafanya utafiti kubaini fursa anuai ambazo zinapatikana ktk jimbo letu la Serengeti lakini ambazo CCM na serikali yake wameshindwa kuzitumia kwa makusudi.

Hali hii imeendelea kusababisha maisha ya watanzania wa Serengeti kuwa duni katika maeneo yote, yaani; Barabara, Maji, Afya na kubwa zaidi ELIMU.

Mwaka 2010 nilitaka kuingia kwenye kinyang'anyiro hiki lakini nilirudi nyuma kwa sababu sikuwa nimefanya utafiti wa kina ili kujiridhisha kwamba CHADEMA inaibwaga CCM vibaya ktk uchaguzi huo.

Lakini tangu hapo, nimezunguka kwenye kata 29 za Wilaya ya Serengeti na kubaini mambo mengi ya msingi. Nailaumu CCM na serikali yake kwa mambo manne makubwa ya msingi ambayo nitayaleta humu jamvin baadaye na hatimaye nitayaweka kwenye makala yangu kupitia Raia Mwema siku chache zijazo.

Kwa ufupi, mimi ni mwana Serengeti na tayari nishaanza kutengeneza mtego na mtandao makini ambao utaitafuna CCM na serikali yake pamoja na vibaraka wake ambao wametanguliza matumbo yao mbele na kuuweka mustakabali wa jimbo letu tajiri na mustakabali wa taifa letu, "REHANI! NATANGAZA NIA"!!,

Nilihitimu Serengeti Sekondari miaka 19 iliyopita, nikaendelea na masomo IDM MZUMBE na kwingineko.

Nina msimamo usio badilika ktk mambo ya msingi, ni mfuatiliaji na mshiriki kwenye mijadala mbalimbali lakini zaidi, mimi ni miongoni mwa watanzania tunao amini katu, pasipo kuiondoa CCM madarakani..... maisha ya watanzania hususani wana serengeti, yataendelea kuwa hivi hivi, na wao CCM watabaki kuwa na uwezo na ulafi huo huo ilhali raslmali zetu zikiendelea kutafunwa na watu hawa hawa wa CCM na kuwanufaisha wao marafiki zao na watoto wao!
 
Hujapitishwa na chama chochote, unawezaje kusema utagombea? Uhakika huo umeupata wapi? SIHASA angalia !!!
 
Na usipopitishwa na chadema utaenda kupokelewa na mwenyekiti wa ccm na kuanza kuivurumishia matusi chadema.
Watu ambao wako so desperate huwa wanaishia huko.
 
"ukitaka kuwa kiongozi.... Sharti uutamani uongozi, uwe na sababu za msingi na hatmaye ugombee na kuupata".....f. Kenedy
 
Mkuu Omokora Nyangi nakutakia kila kheri katika mapambano yako ya kuikomboa Serengeti kutoka kwenye uongozi dhalimu na waki-imla ulio asisiwa na John Ng'weina na kundi lake.

Mie kama mdau wa Serengeti napenda kukupa ushauri wa bure; Yakupasa ujiandae kikamilifu ili uweze kupenya kwenye kura za maoni kwani huu ndo mtihani mgumu kuliko yote utakao kabiliana nao katika uchaguzi ujao 2015. Utakubaliana na mimi ya kuwa kila mwenye akili timamu anafahamu fika ya kuwa Serengeti ni jimbo la CHADEMA, hivyo basi wapambanaji wote wanakusudia kuwawakilisha wananchi wa Serengeti kupitia CHADEMA.

Kumbuka we siyo wa kwanza kutangaza nia, tumeshasikia majina ya watu maarufu kama Dr. Ayoub Ryoba, Mapinduzi n.k, je umejipanga vipi kuibuka kidedea? Ni vyema ukalitambua hili mapema na kuchukua tahadhari stahiki. Otherwise am wishing ALL ZE BEST.

PAMOJA TUIJENGE SERENGETI YETU.;
 
Mkuu Omokora Nyangi all the best; ni haki yako kikatiba ila mambo yakienda ndivyo sivyo sio tena unakuwa wa kwanza kuporomosha matusi kama walivyo wajinga wachache wasiojua maana ya demokrasia.

CC: Mwita Maranya
 
Last edited by a moderator:
Ni vyema ukajipambanua humu jukwaani kwa jina lako halisi (verified name), nia haitangazwi kwa majina bandia. Wengine sisi ni wakazi wa Serengeti tuwekee humu majina yako kwani itakuwa na faida kwako, twaweza kukusapoti humu jamvini pia kwa watu wanaokufahamu wanaweza kutoa taarifa juu ya uadilifu wako na jinsi wanavyokufahamu.😛eace:
 
omokora nyangi, aman'gana , nahisi u mzima, hongera kwa uamuzi wako, ila inatakiwa kupata ushauri toka kwa watu kama MOSENA JOHN NYAMBABE juu ya kushindwa kwake kuchukua jimbo licha ya kampeni alizokuwa anafanya, kujitahidi kupambana na sumu ya ukanda, yaani NGOREME, ISSENYE na ROGORO, pia unahitaji kuonana na mtu anaitwa MUHOCHI huyu anajua vema siasa za SERENGETI pia unahitaji kuunga mawazo na kamand amwita maranya kwani ana ufahamu mkubwa na serengeti, vilevile uwe na mtandao mzuri wa mawakala kwani watuj wa kule kuuza ushindi hata kwa kemoro inawezekana, mwisho unatakiwa kuwa na wagombea udiwani wanaokubalika kila kata
 
master peace

Najua wapo watu na majina makubwa yatakayo penda kushiriki ktk kinyang'anyiro hiki baadhi yao nawafahamu, lakini yapo pia majina makubwa ktk CCM. Nauhakika hata baada ya kupepetana bado CHADEMA itakuwa imempata mgombea bora dhidi ya CCM. Ikatokea sipati fursa hiyo, bado nitakuwa miongoni mwa makada tutakao iporomosha CCM tukisaidiana na mgombea wa CHADEMA.

Nawatahadharisha wote wenye kiu km yangu kwamba, tujipange sawasawa tayari kwa ajili ya "KUNG'ANG'ANIA" kuiwakilisha CHADEMA Serengeti si ktk Ubunge tu lakini hasa kwenye Udiwani, Uwenyekiti wa Serikali za Vijiji na Vitongoji, maandalizi haya ya kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa yalianza mda mrefu, km wenzangu hawajafanya maandalizi ktk hili, ni vyema waanze mara moja kwani wamechelewa mno!
 
Last edited by a moderator:
Ni vyema ukajipambanua humu jukwaani kwa jina lako halisi (verified name), nia haitangazwi kwa majina bandia. Wengine sisi ni wakazi wa Serengeti tuwekee humu majina yako kwani itakuwa na faida kwako, twaweza kukusapoti humu jamvini pia kwa watu wanaokufahamu wanaweza kutoa taarifa juu ya uadilifu wako na jinsi wanavyokufahamu.😛eace:
Ssi watu wa Mara, tuna hulka ya kuwa na majina ya "Ujana au uzee", Jina hili Omokora Nyangi ni jina langu halisi (verified) linalo nitambulisha mbele ya wana jamii forum na hasa mbele ya umma wa wapiga kura wa serengeti. Wakati ukitimu, utanisikia nikijitambulisha kwa jina hili adhimu. Kadhalika, kwa kuwa Jamvi hili lapaswa kuwa la watu makini, naamini kupitia umakini huo nitaanza kupimwa uadilifu ktk maandishi na matamshi yangu kabla ya kuiona sura yangu! Oba, naamini nimejitahidi kujibu suala lako.
 
Mkuu yaani uliona Chadema haina uwezekano wa kushinda ukaingia mitini na sasa wenzio wamejenga chama kiko Imara na kina uwezo wa kushinda na wewe umeamua kuingia humo. Hizi ndio siasa za kisanii za akina Mwampamba tunazokataa. Ilitakiwa utueleze umeshiriki kiasi gani kuhamasisha umma kuikataa CCM na kujenga chama utakachoomba fursa ya kugombea.

Ni bora agombee mkuu Issenye huko Serengeti kuliko wewe...
 
omokora nyangi, aman'gana , nahisi u mzima, hongera kwa uamuzi wako, ila inatakiwa kupata ushauri toka kwa watu kama MOSENA JOHN NYAMBABE juu ya kushindwa kwake kuchukua jimbo licha ya kampeni alizokuwa anafanya, kujitahidi kupambana na sumu ya ukanda, yaani NGOREME, ISSENYE na ROGORO, pia unahitaji kuonana na mtu anaitwa MUHOCHI huyu anajua vema siasa za SERENGETI pia unahitaji kuunga mawazo na kamand amwita maranya kwani ana ufahamu mkubwa na serengeti, vilevile uwe na mtandao mzuri wa mawakala kwani watuj wa kule kuuza ushindi hata kwa kemoro inawezekana, mwisho unatakiwa kuwa na wagombea udiwani wanaokubalika kila kata

Aknowledged! Najitahidi ktk hili lakin naawaalika nyote tushirikiane kwa pa1,naamini kwapa1 TUTASHINDA!
 
Kamanda, Hongera kwa kutangaza nia. Tupo wengi makamanda, njiani kutangaza nia. Kikubwa tupate mtu safi mwenye records and aliye na nia thabiti ya kuwaletea watu wa serengeti tumaini jipya na maendeleo endelevu. Magamba wanatuchelewesha. Mokoro Rugatiri
 
kwa muda mrefu halmashauri ya wilaya ya serengeti imeongozwa na madiwani wasio na elimu, na wababaishaji n a hivyo kushindwa kusimamia mapato ya wilaya yatokanayo na hifadhi, ili kuishinda CCM serengeti inahitajika mbinu za kisayansi hasa utafiti juu ya kujua namna ya kucheza na wapiga kura
 
Omokora wa Gi Nyangi wewe ni mwana Chadema ? Unaijenga Chadema huko? Naona kama hufai kwa kuwa wewe kuingia Chadema unataka madaraka ulipo ona kwamba Chadema haijakaa swa Serengeti hukutaka kuingia kuijenga kabla hujaja JF kutangaza nia .

Je unatangaza JF nia yako ukiwa na maana gani ? Isije ukawa uko CCM una pima upopo hapa ukatiwe chako ukatulie ? Nakushauri nenda Chadema ukapimwe kwa kazi na si elimu yako .Kama ni Elimu CCM wanazo kubwa na za kutisha za kweli na wanazo lukuki za kuunga unga na majina kama Mchumi namba moja au fest klasi .

Rudi Chadema uweleze ulicho fanya kujenga Chama Serengeti vinginevyo utabakia kufanya Nyangi tu .
 
Mkuu Omokora Nyangi all the best; ni haki yako kikatiba ila mambo yakienda ndivyo sivyo sio tena unakuwa wa kwanza kuporomosha matusi kama walivyo wajinga wachache wasiojua maana ya demokrasia.

CC: Mwita Maranya
Mmh!!isije ikawa huyu ni nyakarungu maana si ni mtu wa kule?kama umetangaza nia mapema hivi na chama kikikupitisha sawa ila msije fanya yale mambo ya masalia maana siku hizi njaa nyingi sana.....
 
Ssi watu wa Mara, tuna hulka ya kuwa na majina ya "Ujana au uzee", Jina hili Omokora Nyangi ni jina langu halisi (verified) linalo nitambulisha mbele ya wana jamii forum na hasa mbele ya umma wa wapiga kura wa serengeti. Wakati ukitimu, utanisikia nikijitambulisha kwa jina hili adhimu. Kadhalika, kwa kuwa Jamvi hili lapaswa kuwa la watu makini, naamini kupitia umakini huo nitaanza kupimwa uadilifu ktk maandishi na matamshi yangu kabla ya kuiona sura yangu! Oba, naamini nimejitahidi kujibu suala lako.

Omokora Nyangi nadhani hili litakuwa ni la uzee. Mzee Omokora Nyangi yaani unataka tukupime uadilifu wako kwa maandishi na matamshi yako humu jamvini?. Rudi ujipange, humu hatuangalii mbwembwe za uandishi au ufundi katika kuyaumba maneno. Haya wanayafanya MAGAMBA kwani ndio hodari wa kuwahadaa wananchi kwa maneno matamu matamu.

Wenzako waliotangaza nia humu wameweka majina yao halisi na tumeweza kuwafahamu na kuwauliza maswali kadha wa kadha tukiwa tayari tumeishawafahamu. Kama umeona wakati haujatimu ni kiherehere gani kilichokutuma uje kutangaza nia kwa majina fake?. Narudia kukushauri, weka majina yako halisi humu sisi watu wa SERENGETI tukujue. Mbona Mokoro Rutiginga kijana machachari kutoka kata ya NATTA ameweka jina lake humu kwanini wewe unaendelea kujificha nyuma ya pazia?.😛eace:

SAHIHISHO: Naitwa don-oba.
 
Omokora Nyangi :nni bora kuweka jina halisi ili wanaserengeti tuendeleze mapambano binafsi ni Mwana Serengeti na nimesoma Serengeti secondari miaka 18 iliyopita ila hilo jina sijui funguka :nono:
 
Omokora Nyangi,taarifa ya tafiti ulizofanya na kujiridisha nazo ni vizuri ukazitumia kukijenga chama kwanza
kupitia kwa wananchi,badala ya kutaka kujijenga wewe mwenyewe.
Chadema,watu wake na hasa wanachama safi hawajaanza kutangaza nia zao,ila wapo kwenye
mkakati wa ujenzi wa chama kwa kutumia mapungufu ya chama tawala yaliyopo.
Hivyo basi funguka zaidi na tafiti ulizozifanya ili chama tawala kizidi kuchimbiwa kaburi.
Haya ya nani atagombea wapi tuwaachie waliona fikra walio ndani ya ccm na sio Chadema.
 
Back
Top Bottom