Nitagombea ubunge jimbo la Serengeti 2015

Nitagombea ubunge jimbo la Serengeti 2015

Nakukaribisha serengeti kama K/mwenezi(W) na mbunge ambaye hakutangazwa na diwani wa kata ya STENDI KUU.Karibuni wote tunaotangaza nia nikiwemo mimi binafsi tuijenge CHADEMA kwanza kwa kuwaunganisha wanachadema wote KATA 28 NA SIO 29 kama ulivyodai.
 
Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno....................je nafasi yako hivi sasa na utendaji wako kisiasa ukoje???????????????
 
Nakukaribisha serengeti kama K/mwenezi(W) na mbunge ambaye hakutangazwa na diwani wa kata ya STENDI KUU.Karibuni wote tunaotangaza nia nikiwemo mimi binafsi tuijenge CHADEMA kwanza kwa kuwaunganisha wanachadema wote KATA 28 NA SIO 29 kama ulivyodai.

Mwalimu, jitahidi kuandika kwa kutumia alama kama nukta, mkato nk. Nimepata shida kukuelewa hapo mwanzoni. Hata hivyo nakupa hongera za dhati kwani pamoja na kutotembelea kata zote ulishindwa kwa kura chache, pamoja na hujuma zote ulizozipata.
 
Safi sana kamanda naona umemuwahi Mwita Maranya, nitaakikisha natoa mchango wangu ili ushinde ubunge Serengeti.
 
Last edited by a moderator:
Nilihitimu Serengeti Sekondari miaka 19 iliyopita, nikaendelea na masomo IDM MZUMBE na kwingineko, Nina msimamo usio badilika ktk mambo ya msingi, ni mfuatiliaji na mshiriki kwenye mijadala mbalimbali lakini zaidi, mimi ni miongoni mwa watanzania tunao amini katu, pasipo kuiondoa CCM madarakani.....
Na kwingineko ndo wapi huko? Unamaanisha elimu yako haijulikani iliposhia? Au umesoma sehemu nyingi sana kiasi kwamba kuzoorodhesha haiwezekani? Halafu kukashifu viongozi au wapinzani wako ni umasikini wa sera. Wewe hubiri sera na siyo kusema mala yule tumbo liko nyuma na bla bla kibao. Unahitaji miaka tena mitano ya kujifunza. Kuhusu misismamo nafikiri, kwa sasa tunahitaji wetu wenye busara zaidi.
 
Safi sana kamanda naona umemuwahi Mwita Maranya, nitaakikisha natoa mchango wangu ili ushinde ubunge Serengeti.

Acha unafiki chaguzi za CHADEMA hazitawaliwi na rushwa kama chaguzi za CCM, Mchango wa nini? au ndo mikakati ya kuandaa mazingira ili kamanda aweze kulinda interest zako kwenye ile hotel ya Muishiwa dhaifu ijulikanayo kama kijiji cha Birila - Kempsik ?
 
Mkuu Omokora Nyangi,

Nakutakia kila la kheri kkt nia yako hiyo. Naamini una nia njema ktk kulitumikia taifa. Wewe na wengine watakao jitokeza kupitia cdm onesheni kuwa mnaweza na nitofauti kabisa na magamba. Ninachojua cdm haitaji wabunge tu ktk kilikomboa taifa hili kutoka tulipo kwenda mbele zaidi. Pamoja inawezekana. I wish u all the best.
 
Watu mko Dar mnaota Ndoto za Mchana, CC tunakomaa na M4C na michango yetu ya Ujenzi wa Chama huko Serengeti inajulikana na Record ziko Makao makuu, Kwa systeam ya sasa ya CHADEMA ili upate nafasi ya Kugombea ni lazima uwe na Record ya aina yake katika Kujenga Chama kupiga M4C na kujitolea kwa hali na mali, na si kukaa Mjini na kuota Ubunge, utausikia endapo hutakomaa kujenga Chama

Kwa sasa mambo mengine yatawekwa pembeni, Kama hushiriki kujenga Chama acha kujisumbua mkuu make utafyekwa wilayani, wanao Tangaza Nia kwa sasa wako Vijijini wanapiga M4C watu wanalaa kwenye mahema, wana tembea kwa Baiskeli, Pikipiki na hata Punda Ilimuradi kutoa elimu, sasa wengine wako Mjini wanakula AC and then wanaota Ubunge, Mkuu bila kupambana watu wakuone na Chama kikuone utakuwa unajidanganya Bure, kwa CHADEMA kwa sasa hakuna hilo bali ni juhudi pekee, wewe unazania wakina MAWAZO huko Kanda ya Ziwa wanacheza?
 
Mkuu Omokora Nyangi,

Nakutakia kila la kheri kkt nia yako hiyo. Naamini una nia njema ktk kulitumikia taifa. Wewe na wengine watakao jitokeza kupitia cdm onesheni kuwa mnaweza na nitofauti kabisa na magamba. Ninachojua cdm haitaji wabunge tu ktk kilikomboa taifa hili kutoka tulipo kwenda mbele zaidi. Pamoja inawezekana. I wish u all the best.

Naona unampa moyo, Mkuu mura bila jamaa kupiga M4C HUKO JIMBONI itakuwa ni vigumu sana, ni lazima apige kazi Chama na watu wamuone, apige kazi huko Rung'babure, Kibeyo, Kisangura, Nyamburi, Machochwe, na kwiingineko
 
Umesema ukweli kabisa kama ulikuwa kwenye mkutano wa kamati kuu vile.

sio nilikuwa huko haya mambo nayajua muda mrefu sana, CHADEMA haitakuwa na wale watu wano ibuka kipindi cha uchaguzi na kusema nagombea hayo yaliisha mwaka 2010 kwa sasa ni lazima upambane kwa vitendo CHAMA kikuone na wananchi wakuone na sio mabo ya kuibuka na wanachi wanaanza kusme huyu hatumujui mara sio mkazi wa huku,

Mambo vipi huko? Unanikumbuka? Ni ta Ku PM
 
Na kwingineko ndo wapi huko? Unamaanisha elimu yako haijulikani iliposhia? Au umesoma sehemu nyingi sana kiasi kwamba kuzoorodhesha haiwezekani? Halafu kukashifu viongozi au wapinzani wako ni umasikini wa sera. Wewe hubiri sera na siyo kusema mala yule tumbo liko nyuma na bla bla kibao. Unahitaji miaka tena mitano ya kujifunza. Kuhusu misismamo nafikiri, kwa sasa tunahitaji wetu wenye busara zaidi.

kama ameweza kutaja IDM-MZUMBE ameshindwa kutaja huko kwingineko?.
 
Hujakatazwa kaka,cha kufanya ni kuanza kufanya kz za chama,jitoe,uonekane hata usipoonekana,hatutaki mwana chadema mvivu,hatutaki m2 wa kuzuka,fuata katiba ya cdm,..
 
Umesema ukweli kabisa kama ulikuwa kwenye mkutano wa kamati kuu vile.

Mkuu, hakuna mwenye hati miliki na Serengeti. Tuepuke kumshambulia mtu, na kujiona sisi ndio wenye mamlaka ya kutangaza nia wilaya ya Serengeti.
 
Naona unampa moyo, Mkuu mura bila jamaa kupiga M4C HUKO JIMBONI itakuwa ni vigumu sana, ni lazima apige kazi Chama na watu wamuone, apige kazi huko Rung'babure, Kibeyo, Kisangura, Nyamburi, Machochwe, na kwiingineko

Chasha usiwe kama mtoto wa mama wa kambo, kama umo miongoni mwa watakao tangaza nia, nitakutia moyo. Chamsingi nikupata wagombea wenye ubora wa kulipeleka taifa mbele. Wenye mwono wa kulinda haki ya kila mtanzania na kumkoboa ktk hali hii ya ufukura na ujinga wa kukosa elimu bora.
 
Ndg Wanajamii-Forum,

Mimi ni mdau wa masuala mbalimbali ya kimaendeleo na kwa sasa naishi Serengeti. Kwa miaka 6 sasa nimekuwa nafanya utafiti kubaini fursa anuai ambazo zinapatikana ktk jimbo letu la Serengeti lakini ambazo CCM na serikali yake wameshindwa kuzitumia kwa makusudi.

Hali hii imeendelea kusababisha maisha ya watanzania wa Serengeti kuwa duni katika maeneo yote, yaani; Barabara, Maji, Afya na kubwa zaidi ELIMU.

Mwaka 2010 nilitaka kuingia kwenye kinyang'anyiro hiki lakini nilirudi nyuma kwa sababu sikuwa nimefanya utafiti wa kina ili kujiridhisha kwamba CHADEMA inaibwaga CCM vibaya ktk uchaguzi huo.

Lakini tangu hapo, nimezunguka kwenye kata 29 za Wilaya ya Serengeti na kubaini mambo mengi ya msingi. Nailaumu CCM na serikali yake kwa mambo manne makubwa ya msingi ambayo nitayaleta humu jamvin baadaye na hatimaye nitayaweka kwenye makala yangu kupitia Raia Mwema siku chache zijazo.

Kwa ufupi, mimi ni mwana Serengeti na tayari nishaanza kutengeneza mtego na mtandao makini ambao utaitafuna CCM na serikali yake pamoja na vibaraka wake ambao wametanguliza matumbo yao mbele na kuuweka mustakabali wa jimbo letu tajiri na mustakabali wa taifa letu, "REHANI! NATANGAZA NIA"!!,

Nilihitimu Serengeti Sekondari miaka 19 iliyopita, nikaendelea na masomo IDM MZUMBE na kwingineko.

Nina msimamo usio badilika ktk mambo ya msingi, ni mfuatiliaji na mshiriki kwenye mijadala mbalimbali lakini zaidi, mimi ni miongoni mwa watanzania tunao amini katu, pasipo kuiondoa CCM madarakani..... maisha ya watanzania hususani wana serengeti, yataendelea kuwa hivi hivi, na wao CCM watabaki kuwa na uwezo na ulafi huo huo ilhali raslmali zetu zikiendelea kutafunwa na watu hawa hawa wa CCM na kuwanufaisha wao marafiki zao na watoto wao!

Mkuu binafsi nakufahamu wewe ni Masalia,Bw Nyakarungu,
Swali langu ni moja tu,je haya ndio uliyotumwa na Mwigulu nchemba kutoka kile kikao chenu pale New Africa hotel baada ya kikao chako na hatimae kuachana kwa kukimbia baada ya kumuona Dk wa ukweli?

Pili napenda kuuliza mbona staili yako ya kutangaza kugombea imefanana na mh zitto,mnatoa tamko kabla ya mchakato rasmi kutokea kichama?

Au ndo unapima upepo hivyo?
 
Huyu ni Nyakarungu anapima upepo baada ya kukutwa na Mwigulu New Africa Hotel!!
Kwa hiyo anapima kama Katibu mkuu aliwaona? Ngoja amvutia pumzi kama kweli alionekana watambana kama shonza mpaka akimbilie magamba!
 
Back
Top Bottom