Nitagombea ubunge Jimbo la Segerea – Dar es Salaam

Joined
Jun 20, 2009
Posts
45
Reaction score
225
NITAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SEGEREA – DAR ES SALAAM.

Ndugu zangu, kesho Jumatatu 09 Machi 2015 saa 4.00 asubuhi, nitachukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Segerea kama ambavyo taratibu za ndani ya chama changu zinaruhusu. Hakutakuwa na mbwembwe vifijo wala nderemo kwa sababu bado hatutajajua kwa hapa Dar Es Salaam jimbo gani litaachwa kwa chama gani au ikiwa wagombea wa vyama vyote vya UKAWA watakutanishwa na kupigiwa kura ya maoni, vyovyote vile iwavyo niko tayari kukabiliana na demokrasia ya ndani ya chama changu na hata ndani ya UKAWA.

Hivi sasa nina umri wa miaka 32 tu lakini nikiwa nimepitia kila aina ya uzoefu wa kiuongozi, kisiasa n.k. Naamini kuwa nina uzoefu wa kutosha kuwavusha wana Segerea mahali ambako nimeishi kwa takribani miaka 12 huku shughuli zangu zote za ujasiriamali zikiwa jimboni humu. Ninalifahamu jimbo hili vizuri, watu wake, matatizo yao na changamoto zinazowakabili. Zaidi ya yote nina uwezo wa kushirikiana na wananchi tukioneshana njia ya kuzitatua changamoto hizi na wakati ukifika nitazieleza huku nikiweka wazi njia za kupita.

Pamoja na kwamba nina elimu ya darasani ya kutosha, uzoefu wa uongozi usio na shaka na tabia na mienendo ya maadili huku nikiwapenda watu wa kila namna, natambua kuwa kazi ya kuwa mbunge ni zaidi ya hayo, inahitaji weledi, wepesi, staha na heshima, kujali, kuwa karibu na watu na kujitolea kwa hali na mali kuwapigania wale ambao haki zao na mahitaji yao yanacheleweshwa – kaliba ya namna hii imejengeka na sina shaka kuwa ninakidhi sifa na vigezo hivi vya nyongeza.

Mimi ni muumini wa demokrasia, nitasaidia wagombea wote waliojitokeza kunipinga na kushindana nami ikiwa kutakuwa na haja hiyo, sitamtukana wala kumsema vibaya yeyote yule, kazi yangu kuelekea Oktoba ni kujinadi na kueleza sifa zangu na uwezo wangu huku nikivihusianisha na utatuzi wa matatizo ya wananchi wa Segerea kwa kushirikiana na wananchi.

Nawaomba wanachama wengine wa vyama vya UKAWA wenye sifa, vigezo na uwezo wajitokeze kwa wingi. Sote tutapimwa kwa uwezo na vigezo vyetu na mwisho wa siku atapatikana mmoja wetu na ataungwa mkono na sisi sote. Baada ya Oktoba 2015, Segerea itakuwa na mpambanaji mpya, mbunge wa wananchi na atakayepigana hadi tone la mwisho la damu kwa ajili ya wananchi wake. Na labda mtu huyo atakuwa ni mimi.

Nawatakia kila la heri na kwa ambao wangependa kunifahamu zaidi wanaweza kusoma katika kiunganishi hiki https://www.facebook.com/JuliusSundayMtatiro/posts/578218822317742:0

Julius Mtatiro,
+255 787 536 759, 0755 855 144, Juliusmtatiro@yahoo.com
 
Attachments

  • 10955760_859749797405185_6266134415988192498_n.jpg
    10955760_859749797405185_6266134415988192498_n.jpg
    28.1 KB · Views: 2,239
safari njema mkuu nina imani ukawa tunabeba majimbo mengi kwa upande wa dsm mpaka sasa majmbo 5 uhakika ilala bado
 
Ebu taja hizi haina za uzoefu ulizopitia ili tukujue vyema wanasegerea manake bunge hili kuna wananchi wamedhalilika kwa kupeleka masela bungeni na vijana wakakulie huko wakati bunge ilitakiwa tupeleke watu waliokomaa katika kila njanja. Hatutaki kupeleka mbunge kutoka segerea atakayeenda kutukana, kupigana wala kuzomea. Kwanini usianzie Udiwani?

Kwakuwa segerea ni mjini tunataka chama chenu kilete cream, Matatizo ya watu wa segerea yako katika advance level manake misongamano ya foleni, kuhamia kwa Pub na Bar kutoka Sinza, kuongezeka kwa mateja segerea mwisho. Kuna soko la kisasa kinyelezi na kufungwa kwa mitambo ya gas kuwanufaishe wadau. Ajira zenye maana kwa vijana zaidi ya kuendesha bodaboda sasa na tunataka uwanja wa segerea shule itandikwe capeti bandia ili vijana wacheze soka la kisasa na michezo mengine.
 
mkuu this time ukivuka mchujo wa UKAWA,umechukua ubunge!mambo yamebadilika ni kama zamani ilikua mtu akishinda kura za maoni CCM anajihesabu mbunge!
kila la heri kamanda.
 
kwani Mpendazowe yuko wapi maana alifanya vizuri sana kwenye hilo jimbo kama asingefanyiwa hujuma na CCM
 
Unajisumbua bure. Ccm kisiki cha mpingo itachukua jimbo hilo kama kawaida yake
 
Seconded Mh.Jimbo lako hilo.CV yako kwa ujumla haina chembe ya kutilia shaka.Asiyekufahamu aulizie sifa zako.All the best
 
nakuomea Ukawa ipitishe jina lako tutahakikisha unachukua ushindi,sasa maadam umekuwa wazi be careful yule jamaa wa Segerea ni hatari anaweza fanya lolote
 
kwani Mpendazowe yuko wapi maana alifanya vizuri sana kwenye hilo jimbo kama asingefanyiwa hujuma na CCM

Hata naye mpendazoe kashauri na Mtatiro hapo juu pamoja na wengine wajitokeze kugombea thenly watapimwa na kupatikana mmoja anayefaa hope atakuwa ni Kamanda Julius Mtatiro
 
Last edited by a moderator:
Ebu taja hizi haina za uzoefu ulizopitia ili tukujue vyema wanasegerea manake bunge hili kuna wananchi wamedhalilika kwa kupeleka masela bungeni na vijana wakakulie huko wakati bunge ilitakiwa tupeleke watu waliokomaa katika kila njanja. Hatutaki kupeleka mbunge kutoka segerea atakayeenda kutukana, kupigana wala kuzomea. Kwanini usianzie Udiwani?

Kwakuwa segerea ni mjini tunataka chama chenu kilete cream, Matatizo ya watu wa segerea yako katika advance level manake misongamano ya foleni, kuhamia kwa Pub na Bar kutoka Sinza, kuongezeka kwa mateja segerea mwisho. Kuna soko la kisasa kinyelezi na kufungwa kwa mitambo ya gas kuwanufaishe wadau. Ajira zenye maana kwa vijana zaidi ya kuendesha bodaboda sasa na tunataka uwanja wa segerea shule itandikwe capeti bandia ili vijana wacheze soka la kisasa na michezo mengine.

Haina=aina.
 
nakukubali sana kaka yangu mtatiro,pamoja na ukwel kwamba mi ni Chadema damu UKAWA 4 LIFE....
 
NITAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SEGEREA – DAR ES SALAAM.

Ndugu zangu, kesho Jumatatu 09 Machi 2015 saa 4.00 asubuhi, nitachukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Segerea kama ambavyo taratibu za ndani ya chama changu zinaruhusu. Hakutakuwa na mbwembwe vifijo wala nderemo kwa sababu bado hatutajajua kwa hapa Dar Es Salaam jimbo gani litaachwa kwa chama gani au ikiwa wagombea wa vyama vyote vya UKAWA watakutanishwa na kupigiwa kura ya maoni, vyovyote vile iwavyo niko tayari kukabiliana na demokrasia ya ndani ya chama changu na hata ndani ya UKAWA.

Hivi sasa nina umri wa miaka 32 tu lakini nikiwa nimepitia kila aina ya uzoefu wa kiuongozi, kisiasa n.k. Naamini kuwa nina uzoefu wa kutosha kuwavusha wana Segerea mahali ambako nimeishi kwa takribani miaka 12 huku shughuli zangu zote za ujasiriamali zikiwa jimboni humu. Ninalifahamu jimbo hili vizuri, watu wake, matatizo yao na changamoto zinazowakabili. Zaidi ya yote nina uwezo wa kushirikiana na wananchi tukioneshana njia ya kuzitatua changamoto hizi na wakati ukifika nitazieleza huku nikiweka wazi njia za kupita.

Pamoja na kwamba nina elimu ya darasani ya kutosha, uzoefu wa uongozi usio na shaka na tabia na mienendo ya maadili huku nikiwapenda watu wa kila namna, natambua kuwa kazi ya kuwa mbunge ni zaidi ya hayo, inahitaji weledi, wepesi, staha na heshima, kujali, kuwa karibu na watu na kujitolea kwa hali na mali kuwapigania wale ambao haki zao na mahitaji yao yanacheleweshwa – kaliba ya namna hii imejengeka na sina shaka kuwa ninakidhi sifa na vigezo hivi vya nyongeza.

Mimi ni muumini wa demokrasia, nitasaidia wagombea wote waliojitokeza kunipinga na kushindana nami ikiwa kutakuwa na haja hiyo, sitamtukana wala kumsema vibaya yeyote yule, kazi yangu kuelekea Oktoba ni kujinadi na kueleza sifa zangu na uwezo wangu huku nikivihusianisha na utatuzi wa matatizo ya wananchi wa Segerea kwa kushirikiana na wananchi.

Nawaomba wanachama wengine wa vyama vya UKAWA wenye sifa, vigezo na uwezo wajitokeze kwa wingi. Sote tutapimwa kwa uwezo na vigezo vyetu na mwisho wa siku atapatikana mmoja wetu na ataungwa mkono na sisi sote. Baada ya Oktoba 2015, Segerea itakuwa na mpambanaji mpya, mbunge wa wananchi na atakayepigana hadi tone la mwisho la damu kwa ajili ya wananchi wake. Na labda mtu huyo atakuwa ni mimi.

Nawatakia kila la heri na kwa ambao wangependa kunifahamu zaidi wanaweza kusoma katika kiunganishi hiki https://www.facebook.com/JuliusSundayMtatiro/posts/578218822317742:0

Julius Mtatiro,
+255 787 536 759, 0755 855 144, Juliusmtatiro@yahoo.com

Tunataka vijana sasa mtuonyeshe uwezo we nu. wazee wa ccm wameshachoka
 
Kwanini asiende kwao Tarime, manzese alishindwa au segerea ndio kwepesi nini?

Kwanini na wewe ni mnyiramba wa Ndago singida lakini bado upo segerea? Kwanini na wewe usiende kuishi kwenu singida mkuu?
 
Back
Top Bottom