Nipende kuweka wazi kwa Uongozi wa CRDB ukiongozwa na Dr.Kimei kama gawio kwa hisa moja ni shillingi 10 kesho asubuhi nitaenda kwanza kuhamisha akaunti yangu CRDB na pia kuuza hisa zangu zote. Ni jambo la kusikitisha na lisilo la maana kuona Benki kubwa na yenye heshima na iliyopata faida ya 75bn kama CRDB kuwagawia wanahisa wake shillingi 10 kwa kila hisa moja. Tunawaheshimu sana uongozi wa CRDB lakini kwa hili mnataka kutukwaza. Tunafahamu mtandao wenu, kazi mnazofanya na idadi ya wateja walivyo wengi halafu mnakuja kutugawia shillingi 10 kwa hisa. Labda iwe shs.150 kwa hisa hapo nitakubali. Kwa kweli mnatakiwa mjitathmini kuanzia sasa.