Hakusema alitutawala vizuri. Alitaja baadhi ya mambo mazuri yaliyofanywa na mkoloni yule ikiwemo ujenzi wa reli. Halafu, Mjerumani yule, Carl Peters, sio huyu Gauck aliyetutembelea juzi.Kumpigia makofi mkoloni kwamba alitutawala vizuri ni sifa kwa taifa sio? Vioo vina sehemu ya kuwekwa!
Tena licha ya Ikulu, Mjerumani kafanya kweli, reli ya kati mpaka leo.
Barabara karibu zote unazotumia leo ni zile zile za Mjerumani, sanasana tumezipanuwa na kuweka lami.
Nenda Tanga, moja katika miji ambayo imepangika vizuri na hiyo ni toka Mjerumani, si leo.
Ukweli ubaki kuwa ukweli. Natamani tungebaki kutawaliwa na Wajerumani hadi leo hii. Hatuwezi lolote.
Wewe ni mwalimu kihiyo. Ukifundisha jambo mara zote inakupasa ueleze hasara na faida zake, kwa lugha ya kukopa prons na cons zake. Mazuri na mabaya yake. Rais hajakosea kueleza mazuri ya utawala wa kijerumani, kwanza uongo?Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Profesa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa kututawala na kutuletea maendeleo wakati wa ukoloni.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ikulu jana, Rais Kikwete alimuambia Rais wa Ujerumani kwamba wakati wanatutawala walitufanyia mambo mengi sana mazuri ikiwemo kutujengea jengo la ikulu ambalo tunalitumia hadi sasa.
Rais ameniumbua. Sijui nitaficha wapi uso wangu.
Tangu mwaka 2008 nimekuwa nikiwafundisha wanafunzi wangu Historia nikiwaaminisha kwamba wakoloni hawakuwa na nia njema. Nimekua nikiwaambia wanafunzi wangu kuwa wakoloni walikuwa wakitunyonya, kutukandamiza na kutudhalilisha sana.
Niliwaambia hata elimu waliyoitoa na miundombinu waliyojenga ilikuwa ya kuendeleza unyonyaji.
Niliwaambia wanafunzi wangu kuwa watu waliowapinga ukoloni na kuwapiga vita kama kina Mkwawa, Mangi Meli, Mtemi Isike na Chifu Kimweri ndio mashujaa wetu. Niliwasema vibaya sana wakoloni huku nikitumia vitabu vya kina Walter Rodney kama HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA katika kujenga hoja. Pia nilitumia sehemu ya nukuu za The Dar es salaam School of thought kuaminisha wanafunzi wangu kwamba wakoloni walikuwa watu makatili na wasiotufaa.
Leo rais kaniumbua. Kawaambia Watanzania kuwa Wakoloni walikuwa watu wema sana na waliotuletea maendeleo. Rais akafika mbali zaidi na kukiri bila Ujerumani kututawala tusingekuwa na Ikulu ya Dar es Salaam.
Sasa najiuliza kama wanafunzi wangu wamemsikiliza Rais Kikwete nitakoma maana nitaumbuka. Na kama wamemsikiliza Lazima watamuamini kwa sababu Rais wetu ni Profesa.!!
Kwa heshima ya Malisa Godlisten naomba kushirikisha hii simanzi!
Wakati Mjerumani anakuja hatukuwa NCHI. Ni Mjerumani ndie aliunda Deutch Ostafrica( sijui kama nimechapia!). Kwa kweli aliunda nchi hii kwa nguvu.Hatuwezi kuwashukuru wajerumani kwa kututawala kwa sababu
- walitutawala kwa nguvu
- walitupokonya ardhi
- walitufanya manamba - forced labour
- walituweka katika daraja la chini
kwa hivo hata kama waliacha ikulu, barabara hata reli hii haitufanyi tuwasifu maana hawakutujengea bali walijijengea wao. Tunaweza kuwashukuru kwa misaada wanayotupa sasa au baada ya uhuru na si wakati wa utawala wao.
Wewe ni mwalimu kihiyo. Ukifundisha jambo mara zote inakupasa ueleze hasara na faida zake, kwa lugha ya kukopa prons na cons zake. Mazuri na mabaya yake. Rais hajakosea kueleza mazuri ya utawala wa kijerumani, kwanza uongo?
Wewe ni mwalimu kihiyo au almaarufu kama mwalimu wa Voda faster. Nguchiro we!
4
Hii kitu siyo ngeni masikioni mwangu! Kipindi cha mwalimu Nyerere wanafunzi wa Chuo kikuu Mlimani waliwahi kusema "AFADHALI WAKATI WA MKOLONI" baada ya kugomea jambo fulani!
Naam hata kwenye biblia ipo.
Unasema "ilikuwa" kama vile sasa hakuna biashara ya utumwa. Unashangaza!
Hilo mkuu ni suala la historia. Ikiwa kwa mfano baba yako alichukuliwa manamba na huko ugenini akakutana na mama yako ikawa bahati wewe ukazaliwa huwezi kuwashukuru wale waliomfanya baba yako manamba. that is is co incidenceWakati Mjerumani anakuja hatukuwa NCHI. Ni Mjerumani ndie aliunda Deutch Ostafrica( sijui kama nimechapia!). Kwa kweli aliunda nchi hii kwa nguvu.
Alipoondoka ardhi yetu ilibaki tena na mashamba ya mkonge makubwa tu;
Hilo mkuu ni suala la historia. Ikiwa kwa mfano baba yako alichukuliwa manamba na huko ugenini akakutana na mama yako ikawa bahati wewe ukazaliwa huwezi kuwashukuru wale waliomfanya baba yako manamba. that is is co incidence
Rais wa nchi anausifia ukoloni.
Ni kwanini tusimdai fidia ya watu wetu waliouzwa kama karanga,
wamama waliozalishwa watoto na hao wakoloni bila ridhaa yao?
Hivi inakuwaje hadi mwanaume tena rais wa nchi unakuwa mnyonge kwa mgeni wako kiasi hicho;

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Profesa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa kututawala na kutuletea maendeleo wakati wa ukoloni.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ikulu jana, Rais Kikwete alimuambia Rais wa Ujerumani kwamba wakati wanatutawala walitufanyia mambo mengi sana mazuri ikiwemo kutujengea jengo la ikulu ambalo tunalitumia hadi sasa.
Rais ameniumbua. Sijui nitaficha wapi uso wangu.
Tangu mwaka 2008 nimekuwa nikiwafundisha wanafunzi wangu Historia nikiwaaminisha kwamba wakoloni hawakuwa na nia njema. Nimekua nikiwaambia wanafunzi wangu kuwa wakoloni walikuwa wakitunyonya, kutukandamiza na kutudhalilisha sana.
Niliwaambia hata elimu waliyoitoa na miundombinu waliyojenga ilikuwa ya kuendeleza unyonyaji.
Niliwaambia wanafunzi wangu kuwa watu waliowapinga ukoloni na kuwapiga vita kama kina Mkwawa, Mangi Meli, Mtemi Isike na Chifu Kimweri ndio mashujaa wetu. Niliwasema vibaya sana wakoloni huku nikitumia vitabu vya kina Walter Rodney kama HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA katika kujenga hoja. Pia nilitumia sehemu ya nukuu za The Dar es salaam School of thought kuaminisha wanafunzi wangu kwamba wakoloni walikuwa watu makatili na wasiotufaa.
Leo rais kaniumbua. Kawaambia Watanzania kuwa Wakoloni walikuwa watu wema sana na waliotuletea maendeleo. Rais akafika mbali zaidi na kukiri bila Ujerumani kututawala tusingekuwa na Ikulu ya Dar es Salaam.
Sasa najiuliza kama wanafunzi wangu wamemsikiliza Rais Kikwete nitakoma maana nitaumbuka. Na kama wamemsikiliza Lazima watamuamini kwa sababu Rais wetu ni Profesa.!!
Kwa heshima ya Malisa Godlisten naomba kushirikisha hii simanzi!
Siwezi amin Dr Kikwete anaweza kusema haya maneno! Mpaka nisikie mwenyewe!
Hilo la dini nyingine sijakuelewa, mimi najuwa dini ya haki ni moja tu Uislam.