Nitaficha wapi uso wangu? Rais Kikwete ameniumbua

Nikapata ushahidi wa haya kama ameyasema kweli Le Professeri JK, ndipo nitakapopata ari ya kuchangia hapa.
 
Ni kweli walifanya mema lakini yote ilikuwa kwa ajili ya kutunyonya. Motive haikuwa nzuri na hilo linanifanya niwaone kuwa ni wakoloni tu; na hawastahili shukurani yoyote. Hata mimi nimeumbuka sana kwa kauli za mkuu wa kaya. Nimeendelea kuthibitisha kuwa tuliingia choo kisicho. Tuwe makini zaidi ktk uchaguzi mkuu ujao.
 
Mwafrika mweusi bado ana matatizo, hajitambui, huo ndiyo ukweli.Kwa vile Prof JK ametokana na sisi basi hiyo ni aibu yetu sote kama watanzania weusi na waafrika wengine weusi!
 
bila ukoloni tungekuwa ma bush man kama wa hazabe vile au masai hatuna dira,kila kitu kinatokea kwa sababu,elimu ya zamani ilikuwa jando tu na unyago sasa hivi mnapata elimu dunia.

Kikwete yuko sawa ila hakutakiwa kulopoka hivyo maana aibu
 

watu gani hao mlikutwa hamna nguo au historia uliyoisoma haiongelei ushonaji wa nguo za pamba, magome, ngozi n.k. kabla ya karne ya 19?
 
bila ukoloni tungekuwa ma bush man kama wa hazabe vile au masai hatuna dira,kila kitu kinatokea kwa sababu,elimu ya zamani ilikuwa jando tu na unyago sasa hivi mnapata elimu dunia.

Kikwete yuko sawa ila hakutakiwa kulopoka hivyo maana aibu

Tanzania ina zaidi ya 'makabila' 120 na kila moja ilikuwa na dira na maendeleo ya kiwango fulani, hatuwezi kuweka kila kitu kwenye kundi moja
 
nchi hii imekwisha kata tamaa hakuna matumaini yoyote. asipo sema hivyo hawezi pata misaada kwssababu fikra zake zote zimeengemea kwenye misaada.
 
Hapo itakuwa aliahidiwa suti ya dhahabu
 
Heri utawala wa kikoloni kuliko huu wa CCM!
 

Kwani yeye kakataa. Yeye kasema kaumburiwa
 
Mwafrika mweusi bado ana matatizo, hajitambui, huo ndiyo ukweli.Kwa vile Prof JK ametokana na sisi basi hiyo ni aibu yetu sote kama watanzania weusi na waafrika wengine weusi!
I always ask myself kwanini kivuli Ni cheusi?!
 
Historia inajirudia;
1884 Carl Peters vs Chief Mangungu

2015 Germany President vs Tanzania President

Wakati ule Mangungu alipewa shanga akagawa nchi sijui mwaka huu tumepewa nini yarabi! Na hizo sifa zinazoanza kutolewa hivyo lazima kuna kitu. Tusije sikia Serengeti anayotembelea kesho inakuja kuitwa SERENGETI BUNDES PARK
 
Mr.Kikwete amelitia taifa aibu ya mwaka.
jamani huu ukilaza wa ccm kumbe unaanzia kwenye level ya mwenyekiti wao?
Nadhani unajua nini maana ya Profesa. Ni mtu ambaye baada ya kuwa mzamivu sasa amebobea na kuwa bingwa wa taaluma fulani. Huyu amefanya tafiti nyingi na kuzichapisha katika majarida mengi ya kitaaluma ya vyuo vikuu kadhaa. JK ni Profesa. Huo ni utafiti wake. Tuuheshimuni jamani!! Wajerumani walituletea maendeleo na labda wasingeshindwa vita na Waingereza, sasa nchi hii ingekuwa kama Ujerumani. Na CCM haijafanya mengi kwa muda wote waliotutawala kama wajerumani ambao walitutawala kwa muda mfupi na kufanya yote hayo. Hongera Prof. JK!!
 

Kuna wakati Rais Kikwete aliwahi kusema hii nchi ina viwanda vya kutengeneza uongo...

Vyovyote vile mimi naamini utawala wa Mjerumani ulikuwa na manufaa maradufu ya Mwingereza.
 

Jirani akiwa azini na mkeo/mumeo na anampa fedha hilo ni jambo la kushangilia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…