Nitaficha wapi uso wangu? Rais Kikwete ameniumbua

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Posts
13,402
Reaction score
12,787
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Profesa Jakaya Mrisho Kikwete ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa kututawala na kutuletea maendeleo wakati wa ukoloni.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ikulu jana, Rais Kikwete alimuambia Rais wa Ujerumani kwamba wakati wanatutawala walitufanyia mambo mengi sana mazuri ikiwemo kutujengea jengo la ikulu ambalo tunalitumia hadi sasa.

Rais ameniumbua. Sijui nitaficha wapi uso wangu.

Tangu mwaka 2008 nimekuwa nikiwafundisha wanafunzi wangu Historia nikiwaaminisha kwamba wakoloni hawakuwa na nia njema. Nimekua nikiwaambia wanafunzi wangu kuwa wakoloni walikuwa wakitunyonya, kutukandamiza na kutudhalilisha sana.

Niliwaambia hata elimu waliyoitoa na miundombinu waliyojenga ilikuwa ya kuendeleza unyonyaji.

Niliwaambia wanafunzi wangu kuwa watu waliowapinga ukoloni na kuwapiga vita kama kina Mkwawa, Mangi Meli, Mtemi Isike na Chifu Kimweri ndio mashujaa wetu. Niliwasema vibaya sana wakoloni huku nikitumia vitabu vya kina Walter Rodney kama "HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA" katika kujenga hoja. Pia nilitumia sehemu ya nukuu za "The Dar es salaam School of thought" kuaminisha wanafunzi wangu kwamba wakoloni walikuwa watu makatili na wasiotufaa.

Leo rais kaniumbua. Kawaambia Watanzania kuwa Wakoloni walikuwa watu wema sana na waliotuletea maendeleo. Rais akafika mbali zaidi na kukiri bila Ujerumani kututawala tusingekuwa na Ikulu ya Dar es Salaam.

Sasa najiuliza kama wanafunzi wangu wamemsikiliza Rais Kikwete nitakoma maana nitaumbuka. Na kama wamemsikiliza Lazima watamuamini kwa sababu Rais wetu ni Profesa.!!

Kwa heshima ya Malisa Godlisten naomba kushirikisha hii simanzi!
 
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Profesa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa kututawala na kutuletea maendeleo wakati wa ukoloni.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ikulu jana, Rais Kikwete alimuambia Rais wa Ujerumani kwamba wakati wanatutawala walitufanyia mambo mengi sana mazuri ikiwemo kutujengea jengo la ikulu ambalo tunalitumia hadi sasa.

Rais ameniumbua. Sijui nitaficha wapi uso wangu.
Tangu mwaka 2008 nimekuwa nikiwafundisha wanafunzi wangu Historia nikiwaaminisha kwamba wakoloni hawakuwa na nia njema. Nimekua nikiwaambia wanafunzi wangu kuwa wakoloni walikuwa wakitunyonya, kutukandamiza na kutudhalilisha sana. Niliwaambia hata elimu waliyoitoa na miundombinu waliyojenga ilikuwa ya kuendeleza unyonyaji.
Niliwaambia wanafunzi wangu kuwa watu waliowapinga ukoloni na kuwapiga vita kama kina Mkwawa, Mangi Meli, Mtemi Isike na Chifu Kimweri ndio mashujaa wetu.
Niliwasema vibaya sana wakoloni huku nikitumia vitabu vya kina Walter Rodney kama "HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA" katika kujenga hoja. Pia nilitumia sehemu ya nukuu za "The Dar es salaam School of thought" kuaminisha wanafunzi wangu kwamba wakoloni walikuwa watu makatili na wasiotufaa.
Leo rais kaniumbua. Kawaambia Watanzania kuwa Wakoloni walikuwa watu wema sana na waliotuletea maendeleo. Rais akafika mbali zaidi na kukiri bila Ujerumani kututawala tusingekuwa na Ikulu ya Dar es Salaam.
Sasa najiuliza kama wanafunzi wangu wamemsikiliza Rais Kikwete nitakoma maana nitaumbuka. Na kama wamemsikiliza Lazima watamuamini kwa sababu Rais wetu ni Profesa.!!

Kwa heshima ya Malisa Godlisten naomba kushirikisha hii simanzi!

Wakati fulani tuseme na ukweli, wajerumani walitukuta hatuna hata nguo, tunauzwa sokoni kama mbuzi, je hilo jengo la ikulu kajenga nani kama sio wajerumani, reli ya kati kajenga nani kama sio wajerumani.ukweli mazuri ya wajerumani kwa miaka 35 waliyokaa hayawezi kulinganishwa na ya kwetu.
 
Did he said that!!! Maana huwa sisikilizagi hotuba zake. Alisema kwa ki- english au kwa kiswahili au kijerumani? Nahisi kuna shida hapa. Kwamba anawapongeza wakoloni kwa kututawala na kutuletea maendeleo! Kwa hiyo ndo maana kila siku yuko angani anatutafutia hawa wakoloni warudi kututawala ili watuletee maendeleo zaidi? Kwamba akina Nyerere na wenzake walifanya mapema sana harakati za kutafuta uhuru ili tuweze kujitegemea wenyewe? Kwamba Wa-Tz hatuwezi bila kuwezeshwa na wakoloni?
 
Ukiona jamii yoyote ambayo ni mateka ikimsifu na kumshangilia mtekaji eti kwa kuwa hajawaua basi si bure ujue jamii hiyo imekwisha kukata tamaa ya maisha na ni kifo tu inasubiri!
 
Mleta Mada umenivunja mbavu sana, sina hali kabsa, anyway hiyo ndio namna mtu asiyejiamin hujenga hoja anapokutana na majemedali wajenga hoja, kaona aongee hvo ili apewe misaada, hako n kalugha kengine ka kuomba omba! mkuu katuumbua hata cc wengne na taifa kwa ujumla! kwahyo tuamin kwamb bila wajeruman nji hii isingekua na ikulu? na ile reli ya tazara iliyojengwa na wachina kwa uchina ilitutawala? na wale mashujaa wetu waliowanyonga songea na iringa thaman yao inaendana na reli ya kati? daa huyo prof wetu noma
 
Did he said that!!! Maana huwa sisikilizagi hotuba zake. Alisema kwa ki- english au kwa kiswahili au kijerumani? Nahisi kuna shida hapa. Kwamba anawapongeza wakoloni kwa kututawala na kutuletea maendeleo! Kwa hiyo ndo maana kila siku yuko angani anatutafutia hawa wakoloni warudi kututawala ili watuletee maendeleo zaidi? Kwamba akina Nyerere na wenzake walifanya mapema sana harakati za kutafuta uhuru ili tuweze kujitegemea wenyewe? Kwamba Wa-Tz hatuwezi bila kuwezeshwa na wakoloni?

Nadhani kama ingezezekana huyu Mr. angetaka kukaa chini na wakoloni na kuwaomba radhi kwa kupokonywa yaliyokuwa makoloni yao '' kwa uroho wa Nyerere na waafrika wengine kutaka kuhodhi madaraka kama wazungu'' na nadhani angesema ikiwezekana wakae tena upya mezani kuangalia uwezekano wa kurudishiwa koloni lao!
 
Kama tumeshindwa kujenga IKULU yetu huko Chamwino Dodoma, hata baada ya miaka ya 54 ya uhuru, kwanini asiwapongeza Wajerumani walioweza kujenga hiyo Ikulu ya Magogoni zaidi ya miaka 100 iliyopita!

Pia angeendelea kuwasifu Wajerumani, kwani tangu walipotuletea meli ya MV Liemba, Sisi hata baada ya miaka 54 ya Uhuru tumeshindwa kuweka meli ya kiwango hicho ziwa Tanganyika.
 
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Profesa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa kututawala na kutuletea maendeleo wakati wa ukoloni.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ikulu jana, Rais Kikwete alimuambia Rais wa Ujerumani kwamba wakati wanatutawala walitufanyia mambo mengi sana mazuri ikiwemo kutujengea jengo la ikulu ambalo tunalitumia hadi sasa.

Rais ameniumbua. Sijui nitaficha wapi uso wangu.

Tangu mwaka 2008 nimekuwa nikiwafundisha wanafunzi wangu Historia nikiwaaminisha kwamba wakoloni hawakuwa na nia njema. Nimekua nikiwaambia wanafunzi wangu kuwa wakoloni walikuwa wakitunyonya, kutukandamiza na kutudhalilisha sana.

Niliwaambia hata elimu waliyoitoa na miundombinu waliyojenga ilikuwa ya kuendeleza unyonyaji.

Niliwaambia wanafunzi wangu kuwa watu waliowapinga ukoloni na kuwapiga vita kama kina Mkwawa, Mangi Meli, Mtemi Isike na Chifu Kimweri ndio mashujaa wetu. Niliwasema vibaya sana wakoloni huku nikitumia vitabu vya kina Walter Rodney kama “HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA” katika kujenga hoja. Pia nilitumia sehemu ya nukuu za “The Dar es salaam School of thought” kuaminisha wanafunzi wangu kwamba wakoloni walikuwa watu makatili na wasiotufaa.

Leo rais kaniumbua. Kawaambia Watanzania kuwa Wakoloni walikuwa watu wema sana na waliotuletea maendeleo. Rais akafika mbali zaidi na kukiri bila Ujerumani kututawala tusingekuwa na Ikulu ya Dar es Salaam.

Sasa najiuliza kama wanafunzi wangu wamemsikiliza Rais Kikwete nitakoma maana nitaumbuka. Na kama wamemsikiliza Lazima watamuamini kwa sababu Rais wetu ni Profesa.!!

Kwa heshima ya Malisa Godlisten naomba kushirikisha hii simanzi!
Oh! Oh! Nimechoka! Hiyo yote kujipembedekeza au!
 
Kama tumeshindwa kujenga IKULU yetu huko Chamwino Dodoma, hata baada ya miaka ya 54 ya uhuru, kwanini asiwapongeza Wajerumani walioweza kujenga hiyo Ikulu ya Magogoni zaidi ya miaka 100 iliyopita!

Pia angeendelea kuwasifu Wajerumani, kwani tangu walipotuletea meli ya MV Liemba, Sisi hata baada ya miaka 54 ya Uhuru tumeshindwa kuweka meli ya kiwango hicho ziwa Tanganyika.

Nashukuru sana kwa niaba ya watu wa Ujerumani!
 
duh inanikumbusha hadithi ya MUSA na waisraeli kule jangwani...eti"turudishe kwa wa misri tulikua tunakula,tuna lala"...lkn waliependa Sir.GOD aliwanyoosha.....sasa hapa presida unataka tunyooshwe na Sir.GOD
 
katika mataifa yote wajerumani pekee ndiyo ambao angalau walituachia majengo na miundo mbinu kadhaa.
 
Back
Top Bottom