Nitaendelea kuongoza CHADEMA wanachama wakiamua - Mbowe

Nitaendelea kuongoza CHADEMA wanachama wakiamua - Mbowe

Ndio tatizo hapo kwenye ukomo! Kwa nini uongozi usiwe na mwisho? Mbowe aache siasa za zamani
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Chadema endapo kama wanachama wataendelea kumhitaji.

Kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama chake amesema kamwe chama chake hakizuii watu kutamani uenyekiti lakini akatahadharisha zitumike njia za kidemokrasia na uwazi.Amesema katu Chadema hakitaruhusu watu kutumia njia za kihuni kinyume na Katiba.

Mwenyekiti huyo ambaye ni mhimili mkuu kwa chama chake ameshangaa watu kukimbilia madaraka kwa njia ovu na za kihuni.Amesema kuongoza upinzani si lelemama na wala si wa kukimbiliwa.Amesema kuongoza upinzani ni kukubali kufungwa,kupigwa mabomu na kuzushiwa kila kashfa kila uchao.

Kiongozi huyo amesema kwamba kamwe hawatakubali Chadema kusambaratishwa kwa njia yoyote.

Kuhusu Ukomo wa uongozi amesema Katiba ya Chadema haina kipengele hicho kwa ngazi yoyote na kama mtu anafaa wanachama wataendelea kumchagua bila kujali muda atakaokuwa ametumikia chama.

Source:Nipashe Jumamosi.
 
Nilishasema hapa mkanitukana na maneno yenu ya kejeli!Mbowe hafai kuwa hata wa kijiji bali mhamasishaji wa muziki!Haya sasa kazi kwenu Mugabe Huyoo ndani ya bongo
Hawa wakichukua nchi wataturudisha kule kwenye chama kimoja,dalili mbaya hizo,Watatuingiza kwenye vita hawa
 
Ila Mbowe ni mkaksi.. Nasikia Dr slaa anamuogopa sana.
 
image.jpgKama hawa wakiamua mimi ni nani hata niweze kukataa?
 
image.jpgimage.jpgWanaotoa Zawadi hizi wakiamua nani awe mimi ni nani hata niweze kuwapangia ?
 
Nilishasema hapa mkanitukana na maneno yenu ya kejeli!Mbowe hafai kuwa kiongozi hata wa kijiji bali mhamasishaji wa muziki!Haya sasa kazi kwenu Mugabe Huyoo ndani ya bongo

hivi jk nyerere miaka yote alikuwa mwenyekiti wa chama gani vile?hutu hakuwa dikteta?alifuata demokrasia?lipumba Mae ni wa chama gani?mae ni dikteta?ifike wakati tuache unafiki hata mtikila ni mwenyekiti wa do tangia ianzishwe sasa Kwanini owe nongwa kwa kamanda mboe?
 
Bora uendelee tu si unapatambeleko kutoka hapa kwa mkwe.
photo+%287%29.JPG
 
hivi Mbona Sio mrema au cheyo?wanafiki mnayenu zaidi ya uenyekiti #team mm kwisha habari yenu
 
...tunasema hatutaki uchaguzi CHADEMA- MBOWE, DR SLAA Tosha! Zito akagombee uwenyekiti CCM kama anadhani wanampenda?
 
Nasema na mkome sisi MBOWE TU Nanyinyi maccm ongeeni yenu ya kujivua GAMBA Sisi tuna uzubutu je nyinyi MAJANGILI NA UNGA
 
Hawa wakichukua nchi wataturudisha kule kwenye chama kimoja,dalili mbaya hizo,Watatuingiza kwenye vita hawa

Kufanya kosa siyo kosa kurudia kosa ndiyo kosa.Tusirudie kuwapa tena nchi CCM hawana demokrasia kabisa huu mufumo wa vyama vingi waliukubali kwa shingo upande baada ya kulazimishwa.Mpango wao uliyopo ni kutaka kuturudisha kwenye mufumo ule wa zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM ili waendelee kudumisha utawala wao wa kifamilia.Kila chama kinachoonekana kutishia masilahi ya CCM na familia zao ni lazima wakiwekee mizengwe mbalimbali ili wakiue.Nccr Mrema ilipoonekana kuwa tishio kwao waliivuruga,Cuf ikawa tishio kwao wameidhofisha Chadema imeonekana kuwa ndiyo chama pekee ambacho kinaweza kumuletea maisha bora mtz lakini kwa vile CCM hawana nia njema na wtz wamepandikiza mapandikizi yao wanataka kuiua CHADEMA na watz kwa ujumla wao.Sasa hivi hatudanganyiki tena kama ni mapandikizi yenu tumeyatoa yachukueni yakawasaidie mukayaanzishie maduka na kuyapa kazi kwenye CCM.
 
Mbowe mbona anaongea manyago tu kwani nani kamwambia kuwa hakuna mwingine anayeweza kufanya hayo anayodai aondoke zake na tamaa yake ya madaraka.
 
Back
Top Bottom