Nitaendelea kuongoza CHADEMA wanachama wakiamua - Mbowe

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Chadema endapo kama wanachama wataendelea kumhitaji.

Kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama chake amesema kamwe chama chake hakizuii watu kutamani uenyekiti lakini akatahadharisha zitumike njia za kidemokrasia na uwazi.Amesema katu Chadema hakitaruhusu watu kutumia njia za kihuni kinyume na Katiba.

Mwenyekiti huyo ambaye ni mhimili mkuu kwa chama chake ameshangaa watu kukimbilia madaraka kwa njia ovu na za kihuni.Amesema kuongoza upinzani si lelemama na wala si wa kukimbiliwa.Amesema kuongoza upinzani ni kukubali kufungwa,kupigwa mabomu na kuzushiwa kila kashfa kila uchao.

Kiongozi huyo amesema kwamba kamwe hawatakubali Chadema kusambaratishwa kwa njia yoyote.

Kuhusu Ukomo wa uongozi amesema Katiba ya Chadema haina kipengele hicho kwa ngazi yoyote na kama mtu anafaa wanachama wataendelea kumchagua bila kujali muda atakaokuwa ametumikia chama.

Source:Nipashe Jumamosi.
 
Vizuri sana.
Kama kamati kuu ya chama imemchagua kwa mara nyingine ni vema
 
Sauti ya simbaaaa kaunguluma vinyamkera chaliiiii,. Mbowee for chadema
 
Hivi niulize Mbona Prof. Lipumba na Maalim Self ni Mwenyekiti na katibu respectively kwa miaka mingi toka nikiwa Shule Primary na sasa Nimemaliza Chuo kikuu. Hapa Kuna kitu Kimejificha na CCM ilitaka Kusambaratisha CHADEMA.
 
MWENYEKITI WA TAIFA CHADEMA to mabadiliko ya mwili, kiroho na kiutawala ni mbowe tu na katibu wake ni dr slaa.... Kitila mkumbo pls omba msamaha gari liendele safari, acha kupoteza ndoto zako.
 
nimejitoa cdm rasmi leo kwa kuchoma kadi niliyochukua moshono arusha mwezi may mwaka jana,rip cdm nilikupenda ila udini ukabila na ukanda umekupenda zaid
Hana tofauti na idd amin, mugabe, museveni, gadafi, na madikteta wengine uwajuao
 
Back
Top Bottom