Nitaendelea kuongoza CHADEMA wanachama wakiamua - Mbowe

Nitaendelea kuongoza CHADEMA wanachama wakiamua - Mbowe

Agenda ya kubadilisha uongozi wa juu ni ya maadui wa CDM ili waingie watu dhaifu wanaonunulika kirahisi, ili watumike kuimaliza CDM; wamegundua Mbowe na Dr Slaa ni visiki vya mpingo kwa hiyo wanapitisha agenda hiyo kwa Muha wetu ZZK; sasa wamekwama; hatoki mtu!demokrasia wanayosema ni tafsiri yao, sio lazima kufuata kila kitu katika vitabu vya nadharia; muhimu zaidi meli ikipigwa na mawimbi ikielekea ufukweni sio wakati mzuri kwa nahodha kubwaga manyanga! Stay put Mbowe, tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu; haya ni mapito tu na ndivyo maisha yalivyo

Umenena vema sana!
 
MaCcm yanataka Cdm wampe Uenyekiti Kizito then wakianza kutoa vithibitisho vya ule mlungula walompa, Cdm haitasimama tena.
 
Mbowe muda wako umeishapita kubali mabadiliko ya ndani ya chama. Nalazima kuwe na ukomo wa uongozi. Nakumbuka marehemu baba wa taifa ndiye aliekuwa baba yako wa kiimani. Aliuacha uenyekiti kwa wengine. Hapo unaogopa mapinduzi ya kifikra mpya ndani ya chama. Kama kweli chadema ni chama cha umma wa wanachama basi kipindi chako kimepita ila kama chama ni cha mkweo basi endelea ila.......................
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Chadema endapo kama wanachama wataendelea kumhitaji.

Kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama chake amesema kamwe chama chake hakizuii watu kutamani uenyekiti lakini akatahadharisha zitumike njia za kidemokrasia na uwazi.Amesema katu Chadema hakitaruhusu watu kutumia njia za kihuni kinyume na Katiba.

Mwenyekiti huyo ambaye ni mhimili mkuu kwa chama chake ameshangaa watu kukimbilia madaraka kwa njia ovu na za kihuni.Amesema kuongoza upinzani si lelemama na wala si wa kukimbiliwa.Amesema kuongoza upinzani ni kukubali kufungwa,kupigwa mabomu na kuzushiwa kila kashfa kila uchao.

Kiongozi huyo amesema kwamba kamwe hawatakubali Chadema kusambaratishwa kwa njia yoyote.

Kuhusu Ukomo wa uongozi amesema Katiba ya Chadema haina kipengele hicho kwa ngazi yoyote na kama mtu anafaa wanachama wataendelea kumchagua bila kujali muda atakaokuwa ametumikia chama.

Source:Nipashe Jumamosi.
Kauli hii inafanana kabisa na kauli ya Museveni kule Uganda, yeye alisema ataacha kuwa Rais wa Uganda mpaka wananchi wa Uganda watakapomkataa kwa kutomchagua. Salmin aliwahi kutoa kauli kama hii, kwamba wananchi wanataka aendelee, yaani wanataka kumchahua tena kwa awamu ya 3. Kazi ipo Afrika.
 
Magamba mtaweweseka mwisho wenu umekaribia mliwateza sana watz kwa kuweka viongoz walafi,mafisadi,majangili,wabakaji,wanaoambukiza watto ukimwi,wanaogawa nafasi za ajira kwa rushwa ya ngono.wanao watumia mamluki kama zito msaliti
 
Amenena vyema na sasa ni wakati wa kuitisha uchaguzi ili atoe nafasi kwa wanachama wa
chama chake ili kuamua nani anakubalika zaidi kuwa mwenyekiti ili kuondoa mshawasha.
 
Ni uchaguzi gani hasa unaozungumziwa hapa? CHADEMA wanaendelea na chaguzi ktk ngazi zingine kwa utaratibu wa ugatuaji madaraka waliojiwekea. Itafika ngazi ya mikoa na kanda kisha Taifa.

Kama kuna watu wanataka kugombea na wako eligible kulingana na sheria na taratibu za CHADEMA wachangamkie tenda na sio kuzusha zusha mambo tu.

Ila ukweli ni kuwa F. A. Mbowe ni tishio kwa maadui wote wa CHADEMA.
 
Back
Top Bottom