#COVID19 Nishaurini wakuu chanjo yaniogopesha

Habari ndugu zangu.

Nisiwachoshe niende kwenye mada

Nina SCHOLARSHIP TATU.
1. Oslo university NORWAY
2. Kenyatta univesity, Nairobi KENYA
3. Maseno university, Kisumu KENYA.

Kusoma degree ya pili.

Sasa naogopa nasikia mipakani au kusafiri ni lazima uchanjwe au uwe na certificate ya Corona.

Nawaza mno nakosa majibu, muda unazidi kwenda na vyuo vimeanza, na tayari nilipata Online orientation.

Nishaurini wakuu, ni mtumishi na mwajiriwa serikalini.

View attachment 1926728
Chanjo ni salama na wengi tumechoma na tunadunda kwa Sana. Umesikia Mtanzania gani kachoma àkapata madhara?
 
Chanja uwe huru, unaweza uka fake ukaenda huko ukapata korona ukafa ukarudishwa hapa maiti acha Uoga Chanja, Upunguze uwezekano wa kuugua Covid19.
 
Hii ndio sababu ya wasomi wa nchi hii wengi wao kuwa washirikina wapenda uchawi nawauamini kuliko hata elimu waliyoipata.
Ama kweli kuna tofauti kubwa ya kuelimika na kuwa na akili.
 
Mkuu usiwe na hofu nenda kachanje, kama kuna hila yoyote mbaya kuhusiana na hiyo chanjo haiwezi kukuathiri moja kwa moja kwa kuwa Mungu anayo namna ya kulinda watu wake regardless wamewekewa mtego gani......Mtume Paulo aling'atwa na nyoka, watu walipofikiri kwamba madhara au kifo kingemfika wakaona jamaa hana wasiwasi wowote, yeye ndo akawa anawashangaa kuona wanamkazia macho.
 
Back
Top Bottom