Daaa pole yake huyo dada, lakini kabla sijajitaidi kushauri chochote, kuna kitu nakiona huyu dada alikosea kukiangalia kwa makini kabla ya kuamua kufunga ndoa na huyo kaka.
Alishamuona tangu mwanzo kwamba yeye sio mwaminifu, na sio mara moja kwa nini alikubali kuolewa nae? Ilitakiwa ajipime moyoni mwake tangu mwanzo kama anaweza akuchukuliana na hiyo tabia ya mume wake.
Kama alimuona sio mwaminifu tangu mwanzo na akajiona anaweza kuibeba hiyo tabia akamsamehe basi na ajitaidi kuivumilia huku akimshauri kwa upendo labda atajirekebisha.
Lakini swali kubwa hapa Kwa nini alimkubali mtu mwenye tabia mbaya kama hio ya kukosa uaminifu kwenye mahusiano hata kabla ya kufunga ndoa???
Daa tusubiri na wengine washauri lakini nasikitika kwa uamuzi wa huyu dada kukubali ndoa na mtu mwenye tabia ambayo hawezi kuibeba. Wanawake sa ingine inabidi tufikirie vizuri.
i totally agree with u it was a big mistake to marry such a guy, ingawaje kwa sasa hata yeye anakubali alifanya kosa kumwamwini kuwa atabadilika baada ya kuoana!
kosa lilikwisha fanyika,cha muhimu si kulaumu ten,ila ajaribu kukaa na dungu wa mwanaume wenye hekima kisha ajaribu kuongea tatizo la mumewe...asijaribu kuongea hiyo shida kwa marafiki za mwanaume hakuna watakalomsaidia zaidi ya kuongeza ugomvi na dharau katika ndoa.
Jamii01 utanisamehe my dear
sidhani ni sawa kabisa kuongea na ndugu wa jamaa
mambo kama haya...
borea akaongee na mama yake mzazi
kuliko ndugu yeyote wa mumeo
kumbuka damu ni nzito kuliko maji my dear
samahani ae..
My Dear AD,
Sidhani hata kama damu ni nzito kuliko maji
Mama anaweza kubadili tabia ya huyu jamaa na midevu
Hiyo ngumu hapo ni uvumilivu tu ndo cha muhimu
Na akae pembeni amwache afanye anachotaka asimfatefate
Unajua watu wenye hekima hukaa kimya na wewe mkosaji unaona aibu
na kutojua anawaza nini huyu uoga hukuingia na kuacha
Sory kama nawakwaza si nia yangu
mbona mnaogopa kushauri ???Daaa, hebu tusubiri tu mawazo ya wengine nina Imani hapa anaweza akapa ushauri mzuri, kuna watu wenye uzoefu wa aina mbalimbali katika mambo kama haya watasaidia.
mbona mnaogopa kushauri ???