Mwanaume ninae ishi nae nilikutana nae chuoni na alinisaidia sana kuanzia kimasomo mpaka matumizi yote.Hatujafunga ndoa. Baada ya chuo tuliajiriwa kwenye mashirika tofauti kazi ambayo naifanya mpaka sasa. Mwaka mmoja baada ya yeye kuajiriwa aliachishwa kazi kwa tuhuma ambazo hajaziweka wazi kwangu.
Mimi ndiye mfanya maarifa sasa. Kuanzia tule nini mpaka tuvae nini na ela ya bia nampa.Ameitiwa kazi nyingi ila hataki anasema ana mpango wa kuwa mjasiriamali dalili sizioni.
Nikifikiria hajanioa na nikimwangalia hana dalili hata ya kunikutanisha na watu wa kwao naona napoteza wakati.pia ukimwambia suala la ndoa anakuwa mkali hataki kusikia. Naletewa habari zake nyingi mbaya naogopa kumwambia tuachane kutokana na hali aliyonayo sasa. Amenilemea jamani. Nashindwa nifanyeje. Nakumbuka alivyokuwa msaada wangu nashindwa kumuacha.Nakosa hata hamu ya mapenzi kwake. Namuona wa kawaida sana hana jipya.
Natamani apate kazi atakayoipenda(maana anachagua kazi na mahali kwa kisingizio cha ujasiriamali) ili hata nikimuacha asiwe na lawama. Kwa ukweli nilishamtoa rohoni siku nyingi nipo nae apate tu riziki yake anitoke.
Mwanaume wa kulala mpaka saa nne asubuhi!! Amenichosha jamani.!! Ananipotezea muda naona.
Naombeni ushauri ndugu zangu.