Nishati na madini Count down: Maamuzi mazito yanakuja

Tatizo la Ngereja ni kule KUROPOKA kwake mara sita kuwa MGAO WA UMEME SASA UTABAKI HISTORIA.............. WAKATI HALI HALISI HAIPO HIVYO........ Mbaya zaidi hadi sasa hata yeye hajatuambia tatizo hasa ni nini............KANYIMWA PESA ZA KUTEKEREZA MIRADI............ KANYIMWA WATAALAMU............ au nini kimetokea hadi hali imefikia hapa. HIVYO BUNGE LIKIANZA NA YEYE BASI ATAKEFUATA ATAKUWA MUWAZI MAPEMA.
 

Nategemea msimamo kama huu licha ya mbwembwe zooote zile wataishia kuchapa mninga makofi na kumumunya pipi Ivory zinazotengwa mbele ya vibakuli pale katika meza zao
 

Whichever way we want look at this issue lakini kipimo kimoja ni hiki: Magufuli akisimama either bungeni au huku uraini na akasema barabara fulani itajengwa ndani ya miezi 8 watu wanamwamini, lakini Ngeleja kila analosema i.e mgao mwisho, mafuta yamenunulia, hata wabunge wa ccm wanakataa kauli zake! why? ukweli vs porojo! Na kama Ngeleja anajuwa kuwa mambo ni tofauti kwa nini (a)anatangazia umma na hata wabunge wenzake wa ccm uwongo na (b) kwa nini anasimamia failure? As a leader anaongoza nini? Ni kwanini na kwa vipi umma wa Watanzania uendelee kumuamini kuwa ana uwezo, nia na hata mikakati ya kweli ya kutatua tatizo la umeme na mikataba mibovu ya madini?

Hivi ukibebeshwa gunia la mahindi la uzito kwa kg100 na ukaona kabisa hauwezi hata kupiga hatua moja utafanya nini?
 
Enzi za Mkapa, kipindi hiki na ishu ngumu kama hii anakuwepo pale chamwino. Hivi JK yupo wapi vile???
 

Hayo yote unawaza wewe na si mara ya kwanza wala siyo kwamba hawayaoni au kuyasikia. Hawa viongozi wetu ni wala rushwa wakutupwa labda nikuambie sasa. Huwezi kuwa na nidhamu ya kufikiria kuendeleza nchi kama una roho ya kuiba kila kukicha, hii ya kujenga barabara, shule za kata, kufanya kitu kwa ajili ya public interest ni kwa sababu wanataka waendelee kubakia madarakani.
Viongozi wengi barani Africa ndo wako hivyo, hawana shida na afya za wananchi, hawana shida na kupata mlo kwa wananchi wao, hawana shida na nchi kukosa technolojia mbadala ya kuzalisha umeme, hakuna haja ya kupeleka vijana wakasomee njia mbadala ya kuzalisha umeme kama solar, wind, Gesi, Wave energy, Microgrid, Smart grids, Micro turbines, Nuclear energy nk. Tunapozungumzia kukuza uchumi wa nchi, nishati ya umeme huwezi kuikwepa wala huwezi kujiuma uma kila kukicha kutoa majibu kama anavyofanya waziri wetu Ngereja (Mwanasheria ambaye hajui umeme unazalishwaje).
 

Huu ndio mchezo mchafu wa siasa ambao wao wenyewe sasa wanaziita Siasa Uchwara. Mara kadhaa Waziri alikuwa anatoa kauli kama hizi kusafisha njia kwa Mkuu wake pale alipokuwa anaenda kufanya ziara za Mikoani akitambua kuwa hilo litampa wakati mgumu kwa wapiga kura.

Akithibitisha hayo kutokea Malaysia na yeye kajaribu kumbeba kwa kusema ni tatizo la Serikali na si Wizara. Anasahau kuwa Msabaha na Karamagi pia walijiuzuru hapa kwa mkataba wa Umeme wa dharura na likawa Tatizo lao binafsi na wala hakusema kitu, licha ya Msabaha kuongea kwa uchungu kuwa '' HAPA KUNA WATU WANATOLEWA KAFARA''. Licha ya yeye pia kutotaja akina nani hao na nani anyewatoa kafara.

Bila Umeme wa uhakika jinamizi hili halitakwisha
 
Kwa wabongo tulivyo kuaachia Uwaziri usikute ameishaanza kuwaza mengi tu ndio maana anaona mbinde kujiuzulu
 
Nalibwaga chini na kuanza mbele.......... ya nini nipoteze uhai wakati uwezo wa kulibwaga upo mikononi mwangu.........??!!
 
Reactions: FJM
Enzi za Mkapa, kipindi hiki na ishu ngumu kama hii anakuwepo pale chamwino. Hivi JK yupo wapi vile???

Ndo kwanza walikuwa na NEC Moshi, kama walilijadili hili na si la Mvua Gamba Aziz basi italeta maana. Maana nilitazama habari kutoka Moshi ilijaa vijembe na misimamo ambayo inajidhihiri kabisa makundi huko hayatakwisha mpaka anguko kuu la kambi ya Kijani 2015
 
Wind energy, the most promising source and rapidly growing in Europe, Asia and South America. And we have enough solar radiation, lakini hutasikia hata siku moja mipango kabambe ya kutumia hii nishati zaidi ya kugeuza dili za viongozi wetu.
 

Attachments

  • modified.jpg
    18.1 KB · Views: 32
  • solarmap.png
    52.1 KB · Views: 40
Wanatengeneza episode nyingine, hawana jipya... Bado kitambo kidogo tu wataanza kuvuana nguo hadharani!!!
 
Maoni ya kambi ya upinzani Bungeni ( Mnyika) na Kamati husika na presha ya maandamano ya Chadema yanayokuja baada ya Bunge yatawalazimisha CCM wafanye maamuzi magumu watake wasitake. Wakikataa wananchi watawasaidia kuamua.
 
Hili ndio suluhisho:

PM amebebeshwa bendera

Anazungumzia Mgao ulivyotuathiri na Vyanzo

Anataja SYMBION kama chanzo muhimu kitakachopunguza tatizo japo tutakuwa bado na pungufu ya MegaWatt 65

Serikali imeamua kununua mtambo wenye kuzalisha MegaWatt 100 na kubaki na nyongeza kidogo kabla ya Desemba 2011

Anakiri licha ya jitihada hizo watakuwa bado hawajakidhi hitajio la Taifa

Kwa maana hiyo inahitajika mitambo ya MegaWatt ifikapo 2013
 
Anaandaa mazingira ya Ngeleja kupitisha bajeti yake ili kuinusuru serikali.
 
Anasisitiza kuwa serikali imezingatia maoni ya Wabunge kuhakikisha fungu la Other Chargers Zikiwemo Posho zinapunguzwa ili kumaliza Tatizo la Mgao kwa kupata mitambo ya Uhakika. Na kwa niaba ya serikali amekubali.
 
Maji yamemzidi Ngeleja amempigia pasi kwanza Pinda ili adribble kuelekea langoni kabla Ngeleja hajapokea pasi kuelekea langoni na kufunga goli, hapa wabunge kuna uwezekano wa kufungwa.
 
Wiki tatu wizara ije na majibu ya Uhakika kwa mpango unaotekelezeka.

Bunge limeahirishwa

GR is out
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…