Niseme na mabinti leo

Niseme na mabinti leo

Kama tu uko na akili timamu optimal health (psychological, emotional, physical, spiritual and intellectual basi ni lazima unawaza kuwa kuna siku utaolewa, au unatamani kuolewa. Sasa, hata kama umeokoka, kupata mume kunahitaji zaidi ya maombi. Yaani najaribu kusema, mbali na kuomba na kumuamini Mungu kwa ajili ya mume; wewe pia:

1. Unapaswa kujiweka kama muolewaji. Kuna jinsi unavyovaa, behave na kuongea, yaweza kuwafanaya waowaji waone kuwa wewe ni candidate au la! Kwa mfano, unapokuwa katikati ya watu, hasa wakaka how do you present yourself? Yaani, kila saa kuchimba beat, yaani mimi nikiolewa, mwanaume hawezi kunitawala, na zamu yake ya kupika nitampangia, du, na story zingine nyingiiiii? Za kuwafanya wakaka waongeze maswaliiiiiii! ha ha ha! hakuna kaka duniani anapenda kuwa na mke ninja! Usije tu kumsingizi roho mtakatifu, ati wakati bado, saa nyingine waweza kufukuza baraka mwenyewe!

2. Kuwa na ndoto zisizo halisi. Wewe ndo kwanza umemaliza chuo, wakaka wengi utawapata ndio hao mara hata degree hana, maana hajamaliza, au hata kazi hajapata. Na hujui baada ya chuo itamchukua muda gani kustabilize. Eti wewe, unataka mchumba mwenye gari, sijui mshahara milioni, hizo ni ndoto zisizo REAL! Penda tu mkaka, hata kama anavaa soksi kwenye sandle, cha msingi ona kama uwezo wake wa kufikiri unakua, muda ukifika, kazi nzuri atapata, na gari atanunua. Upendo wa kweli hauangalii materials, zinakujaga na zinaondokaga, ila nyie wawili mnabaki. Ungewaambia wadada wanoendesha magari ya waume zao wakupe shuhuda leo, wengi wangekuambia, walivyojifungua mtoto wa kwanza walipanda daladala au taxi. Clinic ya ujauzito walitembea km 3 na zaidi kila clinic.

3. Usiruhusu mkaka akung’ang’anie halafu hata hajui kwa nini yuko na wewe! Kakangu mmoja aliwaita ‘washika pembe’. Mkaka kila mara mahali mmeongozana, mara umemsindikiza kwenye huduma, mara mmeenda kunywa chai, we unassume amekuchumbia kumbe ana mastress yake, wewe ndo amekufanya stress reducer wake.

(i) Atakufukuzia wakaka wote wanaofikiri kukupropose, maana wakaka wastaarabu hawapendi kushindania binti mmoja, na wengine kama wewe watassume amekuchumbia,

(ii) Atakuachia maumivu ambayo hukustahili, maana kufuatana fuatana, kunamfanya mtu ajae kwenye nafsi yake, kumtoa utahitaji kusafisha nafsi na jiki.

4. Usispiritualize na mambo ambayo ni ya kawaida kabisa. Mkaka kaja, unamuona anakupenda kabisa, nawe unampenda, lakini unasingizia unaenda kuomba, kuomba kwenyewe huombi, au na Mungu mwenyewe hujui kwa hapo atakusemeshaje, basi unapeperusha ndegeeeeeee, halafu ……

5. Usiruhusu kukosa furaha kwa maumivu ya jana. Kwa sababu yoyote ile, ama uzembe, ama bahati mbaya, ama ulimsikia shetani ukadhani ni Mungu, ukapenda mtu, kisha mahusiano yakaishia usipopajua, basi unaanza ‘ ooh , sitakaa niamani mkaka tena’, ooh kwa sasa sitaki mchumba’, ukweli ni kwamba, you simply trusted the wrong person, there are so many nice and trustworh men out there! Issue ni unavyojiweka, unavyojiingiza kwenye mahusiaono, bila umakini, achana na habari ya jana fungua ukurasa mpya, iendee furaha ya ndoa.

6. Usichanganye utumishi na ndoa. Wadada wengi wanafikirigi mkaka mwenye jina kubwa, au mtumishi mkubwa ndio mume mzuri. TOOOO WROOOOOOONG! Utumishi ni agenda nyingine, na ndoa ni darasa lingine. Usije mpenda mkaka kwasababu ni mtumishi na kuwa na unrealistic goals. Kuna wakaka wameokoka, hawana majina makubwa, but wanampenda Mungu, na wanamtumikia kwa kiwango chao, na wapo wakaka watumishi wenye majina, walio waume wazuri, na kuna wakaka wengi tuuu ni watumishi wenye majina, na passion yao ni kuona mtu anaokoka, au huduma yake hiyo. Basi akienda door to door, akirudi ana furaha kanisa la Yesu limeongezeka na story ni shuhuda tuuuuuuu, mpaka mnalala ! So, kuolewa na mtumishi ni sawa, lakini USIASSUME KUWA KILA MTUMISHI MKUBWA NI MUME MZURI.

7. Story ni nyingiii sana lakini jumla ya mambo yote, ni kumcha Mungu. Jifunze kuwa realistic, huku ukimtanguliza Mungu katika ndoto zako, uombe, uishi ukristo na kubehave kama mke mtarajiwa.

Barikiwa

Credit - Gwandi Mwampeta
Umenena vema dadangu ,hakika mwenye macho kasoma na kuelewa wameelewa kazi kwao
Ila asante kwa ujumbe mzuri
 
Mbona kama umepagawa mkuu, take it easy ni maisha tu..
Kama una stress si uanzishe uzi wako uteme hzo pumba zako.. Kwann unaharibu uzi wa mtu bila sabab..?
Umepagawa wewe unayejibu post ya October 2017 leo January 2018.
 
Shida iko wap, uzi ungekuwa ume-expire ungefungwa

Jiangalie ww, kama umevurugwa fanya yako, si kila mtu wa kumjibu
Umevurugwa wewe unayesema mimi nimeharibu uzi kwa wewe kuendeleza mazungumzo na mimi mharibu uzi miezi kadhaa baadaye.
 
Habari nzima imeanza kwa hoja potofu. Kwa sababu si kila mwenye afya njema anataka ndoa na si kila anayetaka ndoa ana afya njema.

Jamani mnapoandika mambo msi generalize tu,kwa sababu kijijini kwenu watu wanachambia majani, basi mkafikiri dunia nzima watu wanachambia majani.

Kuna wengine wanachambia maji, mchanga, toilet paper etc.
Heheeee malumbano ya hoja
achana nae huyo
 
Ushauri mzuri ni rahisi kuupata ila ni vigumu kuufata. Hasa kwa mswahil
 
Ukiwa na akili legelege hata neno la mfano utaona lugha chafu.

Ulichoandika hapo tayari ni lugha chafu, umeiandika katika ile hali ya wanasaikolojia wanachokiita "passive aggressive".

Umenitukana kwa lugha chafu huku ukijificha nyuma ya madili ya kwamba huna lugha chafu.

Unaniambia "ubarikiwe" huku unanitukana ,unafiki gani huo?
Hii ligi haiishi leo
 
Back
Top Bottom