Kalolo Junior
Member
- Oct 20, 2011
- 81
- 27
Mwenzenu nimehamia Jijini Dar hivi karibuni baada ya kupata kibarua katika taasisi moja ya Serikali. Katika harakati za kutafuta makazi, nilibahatika kuunganishwa na mwenye nyumba ambaye pia ni mtumishi wa Taasisi niliyopo. Aliyeniunganisha na nyumba hii ni mtumishi mwenzangu ambaye tupo ofisi moja.
Nyumba niliyoipata ina sehemu za biashara kwa mbele na moja ya biashara hizo ni Kontena moja ambalo liliwekwa kwa ajili ya Grocery. wakati nahamia katika hii nyumba, hii grocery ilikuwa haifanyi kazi kwa kuwa aliyekuwa anaiendesha ni mwenye nyumba aliyehama. Kwa sasa Grocery inaendeshwa na yule mtumishi mwenzangu ambaye nafanya naye kazi ofisi moja.
Tatizo lililopo ni kwamba hii Grocery inavyoendeshwa imekuwa ni zaidi ya Bar kwa sababu ikifunguliwa mida ya saa 6 mchana unawashwa mziki mkubwa hadi itakapofungwa mida ya usiku mkubwa (saa 8 hadi 10). Hali hii imekuwa ikinikera na nashindwa nifanye nini maana kuhama nashindwa kwa kuwa nimelipa kodi ya mwaka na nimefanya ukarabati uliogharimu zaidi ya 1M.
Waungwana naombeni ushauri wa nini la kufanya!