Nisaidieni ni make ups au Mkorogo

Nisaidieni ni make ups au Mkorogo

mwathu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2012
Posts
403
Reaction score
210
Naomba msaada wenu wa ushauri kwa wenye uzoefu na haya maana mimi mgeni wa jiji hili na kila uchao naona maajabu tuu. Hapa ofisini kwetu kuna wadada kama watatu hivi ambao ni weupe sana hasa maeneo ya usoni na kwa mtazamo wangu nikiwa kama mtu wa kawaida naamini kuwa ni weupe wao ila kama ni mkorogo pia basi siwezi jua.

Leo tulikuwa na safari ndogo ya hapa mjini tukaongozana nao kweny gari ya ofisi na bahati mbaya njiani tukapata kaajali kidogo ambako kalisababisha mwenzetu mmoja (wa kiume) kupata majeraha mkononi. Sasa ikabidi tutafute angalu kitambaa kuzuia ile bleeding ya damu wakati tukiwa tunatafuta namna ya kumpeleka hospitali, Wale wakina dada wakajitolea vitambaa vyao ili jamaa afungwe mkononi lakini kwa wote watatu vitambaa vyao vilikuwa na harufu kali ya uvundo ambayo nikiilinganisha na urembo wao nashindwa kupata jibu, harufu ilikuwa kali na mgonjwa akasusa na kuamua kuvua shati lake mwenyewe na kulichana vipande ili afunge mkono wake.

Sasa anjiuliza wenzangu:-
a) Je huu ni uchafu tuu wa kawaida kwa wakina dada ila mbona vile vitambaa vina harufu moja ya kufanana ila mbaya sana?
B) au ni makeups na vipodozi wananavyotumia ila kwa nini viwe na harufu kali hivyo na je wakitoka jasho si watu watawakimbia.
c) au ni mikorogo wanatumia ndio inasababisha hivyo, Nisaidieni jamani maana nimejikuta mpaka nawachukia ghafla.

Nisaidieni watambuzi tafadhali.
 
Unajua wanawake wa mjini ni wabunifu sana mweusi km chungu ni yule tu uliyesoma nae darasa la saba akuwa Kijijini basi!!!

Huoni hata kuomba kazi cheti cha la saba muhimu maana wakati ule huwa hujui kudanganya hata kidogo sasa kukujibu hywa wanasema siyo mkorogo ni MAKEUP!
 
Mmmmh basi hatari sana maana kama anakuwa mkeo unawezaje kulala na mtu katika hali kama hiyo utahitaji uletewe mtungi wa oxygen.

Unajua wanawake wa mjini ni wabunifu sana mweusi km chungu ni yule tu uliyesoma nae darasa la saba akuwa Kijijini basi!!!

Huoni hata kuomba kazi cheti cha la saba muhimu maana wakati ule huwa hujui kudanganya hata kidogo sasa kukujibu hywa wanasema siyo mkorogo ni MAKEUP!
 
Hyo ni korogoo,carolite ina harufu mbaya afu rangi ya orange..make ups zitoe uvundo i don't think so, mhh wachafuu hao..
 
Uzuri wa mtu ni ule usionunulika kwa bei ya macho.
 
Hizo ni harufu za kemikali zinazotoka kwenye mikorogo wanayopaka.
Imechanganyika na jasho wanalotoa nalo ni hizohizo kemikali za sumu.
Bahati mbaya kabisa wanapaka mchana na kutembea juani, utawaona tu jinsi wanavyovuja jasho.
 
Kesho ukifika kazini kwako' assignment yako yakwamza fanya kuwauliza juu ya hilo swala' nadhani wao watakuwa namajibu sahihi zaid! Hapa tutabuni tu'

Ebu nibun kama wengine' labda walipaka dawa ya mvuto' ndo maana wewe unakiri kwamba warembo! Hapo vipi?
 
Back
Top Bottom