Baba Rayhaan
JF-Expert Member
- Mar 24, 2011
- 632
- 434
Nilikua na mwanamke niliemuoa na nilikua nampenda kupita kiasi, ila tumeachana miaka miwili iliyopita baada ya kuhisi eti ninatembea na rafiki yake, kiukweli sikua kabisa na uhusiano na rafiki yake na alipochukua maamuzi ya kunisubiri nitoke nyumbani kisha asombe kila kitu ndani na kuondoka, iliniuma sana nilikonda sana kwa sababu nilikua nampenda mke wangu kupita maelezo, nilijitahidi sana kumshawishi arudi tuendeleze maisha lakini cha kustaajabisha wazazi wake walimpeleka kumsomesha hotel management huko Dar es Salaam bila hata kunitaarifu na sasa hivi anafanya kazi hoteli ya kitalii huko Zanzibar, ilinichukua muda mrefu sana kumuondoa kichwani na ilibidi nikapate msaada wa daktari ambae aliniandika anti depressants nikatumia kwa miezi sita angalau nikaanza kuzoea hali halisi kwamba sipo na mke wangu anymore, msaada ninaowaomba mnisaidie ni kwamba, kwann nikiona kila kitu kinachomuhusu yeye moyo unanilipuka na kuanza kwenda mbio? Kila kitu mpaka mtoto wetu nikimuangalia namuwaza sana mama yake, sijaingia tena ktk uhusiano kwani ninaogopa sana kwa sasa, nishaurini nifanyeje niwe angalau namuona wa kawaida na moyo usiniende mbio kiasi hiki.